Wakuu hivi mnafikiri jose mourinho angesema nini ili aonekane bora kwa kuchukua ubingwa zaid ya kusifu ligi ya england.
hebu jiulize katika ligi ya england mwaka huu mbabe wao chelsea huko kwenye ushindani huko kafungwa mechi tatu tu kati ya mechi 37, hebu tuwe wapembuzi, hivi ni kweli kiwango cha chelsea ni cha kupoteza mechi tau tu kati ya gem 37 hadi sasa, ni kweli? hamjua kuwa pamoja na ubora barca kapoteza mechi nne, na madrid kapoteza mechi 6 na atletico pia 6, vipi hapo?
Hivi chelsea ana ubora sana wa mpira na ufundi wa kutosha au kuna tatizo uingereza, na ushindani wao wanauonyesha wapi, maana uropa alikuwa liver, tottenham na everton, hamna aliyefika robo, ndo kwanza everton anawadindia kina man U na kuwavuruga, avu mpira huo huo usio na ubunifu kaenda kucheza na timu ya ukraine akala 5, hapo mourinho pointi yake ipo wapi?
Hivi PSG si ndo kamtoa CHELSEA, msimu huu huu, pia si amekutana na barca mara nne yaani makundini na robo, si kapigwa bao 8-2 na BARCA katika mech 4, chelsea si katoa 3-3 katika mechi mbili na hao PSG. Tuwe wakweli hivi kina sevilla, valencia, vila real, athletic bilbio ni sawa na kina newcastle, sunderland, hull city n.k. hivi kule EUROPA SPAIN si walikuwa na timu tatu zikatoana zenyewe na sasa servilla anacheza final, huku waingereza ni very poor hawakufika robo ya EUROPA WALA CHAMPION LEAGUE.
Hiyo ligi yenye ushindani, katika mafanikio ya CHAMPION LEAGUE na EUROPA inashika nafasi ya tatu, wa kwanza spain wa pili italia wa tatu england-CL, EUROPA wa kwaz italia wa pili spain na wa tatu ni England, kwa over all hata baada ya majina ya mashindano kubadilishwa badilishwa.
BARCA NA MADRID kweli wanavuruga ushindani wa mpira spain, ila hawaishii huko hata mashindano makubwa ulaya kwa ujumla, wapo katika viwango vya juu mno, mana kama tano tano au saba saba wanafunga champion league na home pia.
Hivi hatuna misimu saba timu za spain lazima zitoe dozi ya magoli zaidi ya 5 ulaya, si hapa kati wameongeza kidogo katika mechi moja wamefunga funga saba saba, ukijumlisha kuna timu zimepigwa zadi ya 10, wote kwa wakati tofauti, mbona washaulifu, au soka si hobi yenu, mmetutembelea tu wadau?
MOURINHO anajua ila lazima awapumbaze waingereza, kama makocha wa ulaya wanaona barca na madrid wanatawala sana ligi yao wawastopishe kwenye CHAMPION LEAGUE basi, si kuleta porojo. Kuna zaidi ya miaka saba champion league anayemtoa BARCA au MADRID au tim ya SPAIN nyingine anakuwa bingwa, hivi hilo mourinho na ninyi mashabiki hamlioni au kiburi, kumbuka hilo. Yaani tim ikiitoa tim ya spain ndo inahakikisha high peak labda ikutane tena na hao hao, kumbuka UEFA
· MAN U aliitoa BARCA 2009 akabeba
· INTER aliitoa BARCA 2010 akabeba
· Chelsea aliitoa BARCA 2012 akabeba
· BAYERN aliitoa BARCA na DORTIMUND aliitoa Madrid 2013, fainali, BAYERN akabeba
· 2014 wenyewe kwa wenyewe, nakuhakikishia atletico angeingia na mwingine angebeba
· Leo hii waliingiza tim 3 robo afu 2 nusu, tena kwa sababu zilitoana zenyewe, hivi ni tim za kubeza hizi kama kweli tupo serious na timamu pia juu ya mpira.
Kuhusu ushindani, hata Afrika ya Mashariki ligi ya bongo ndo yenye ushindani mkubwa, vipi? tumlete TP MAZEMBE na ENYIMBA tutakuwa tunawafunga, porojo na ukweli havikai pamoja, mimi naangalia ligi ya UINGEREZA sana mana ina mvutano, ila mpira mbovu sana, hivi kwa viwango vya kina ARSERNAL miaka yote top four, angekuwa spain angemaintain kweli, hivi arsernal ndo mpiga pasi uingereza hivi anafikia kiwango cha upigaji pasi wa SERVILLA, VILA REAL, GETAFE, REAL ZARAGOZA na wengineo, na wanaleta makombe kwa zam nchini kwao.
Atletico madrid ingekuwa uingereza miaka miwli hii ingeweza chukua ubingwa, sema kule kakutana na wababe, ana bahati mbaya mno.