ALEYN safi kwa hoja yako,lakini naomba kutofautina na wewe kidogo..kwa sababu hii ni JF.
Kwanza niseme mambo ambayo Mourinho amefanya kwenye mpira wa Ulaya hakuna kocha amewahi kufanya kwa staili hiyo:
Mambo yapo hayo?
-Amechukua ubingwa wa UEFA cup akiwa na Porto.
-Amechkua UCL, akiwa na Porto pia kumbuka aliitoa Man Utd, kwenye hatua ya 16 bora, tena pale pale kwao.
-Aliwapa ubingwa Chelsea, ambao ambao hawakuwa wameupata kwa miaka karibu 50, hii ilikuwa 2004-2005 & 2005-2006!Akiwa Chelsea aliingia nusu fainali ya Champions League.
-Akawapa Inter Milan ubingwa wa Italia, na UCL.
-Akawapa Madrid ubingwa kwa rekodi ya pekee ya points nyingi sana!
-Usisahau kwamba Mourinho ni kocha ambaye ameifunga Barcelona mara nyingi sana. Kuliko idadi ambazo Barcelona imemfunga Mourinho. Jamaa amewafunga Barcelona akiwa Chelsea, akiwa Inter Milan, na hata akiwa Madrid au hajawafunga Barca?
-Kachukua ubingwa katika ligi za nchi 4 tofauti:
Ureno
Uingereza
Italia
Hispania
Ngoja nipumue kidogo!:A S 100: