Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Hakika Rais Mstaafu JAKAYA KIKWETE pamoja na kuwa NDOTO yake ya KUWAPATIA WATANZANIA KATIBA MPYA Haikutimia Bado Ataendelea kuwa BABA wa KATIBA Aliyethubutu Kutupatia KATIBA MPYA.

Mwaka 2015 Wakati wa UCHAGUZI MKUU Chama cha CCM Katika ILANI yake Ilisema Itakamilisha Upatikanaji wa KATIBA MPYA.
Baada ya MAGUFULI kushinda Kiti cha URAIS alianza KUGEUKA na Kudai Sio Kipau Mbele cha Serikali na KUDAI ANAJENGA UCHUMI.

Baada ya KIFO cha MAGUFULI Mh Rais SAMIA Amechukua UONGOZI wa NCHI.Jana Wakati Anaongea na Waandishi wa Habari Rais SAMIA Anadai Eti kwanza AJENGE UCHUMI sababu zile zile za MAGUFULI.Watanzania tunajiuliza Kwanini AWAMU ya 5 Imekuwa na Sababu Dhaifu juu ya KATIBA MPYA?

Mbona JAKAYA KIKWETE Alianzisha Mchakato Bila SABABU za UCHUMI?

Mbona KATIBA iliyopo ya 1977 UCHUMI wetu Ulikuwa Chini sana lakini KATIBA ilipatikana?

Suala la UCHUMI Kuujenga ni Suala la KILA SIKU hivyo Kusingizia TUNAJENGA UCHUMI ni Sababu DHAIFU SANA.

WATANZANIA Tumekwishaambiwa ni NCHI ya UCHUMI wa KATI.

WANANCHI TUNATAKA KATIBA MPYA HATUTAKI SABABU DHAIFU
 
Hilo suala la katiba, mpya ccm kamwe hawataweza kuliruhusu ki rahisi kwani wanajua, ni kitanzi cha kuwamaliza, MAMA, atajitahidi sana kusikiliza yote , lakini kwa hili ni gumu mno!

Kwani hata awe na nia vipi huko nyuma kuna WAHAFIDHINA, hawataliruhusu kamwe, labda vugu vugu lipambe sana, lakini wako wapi wa kulianzisha hilo vuguvugu?!!kama wakipatikana inaweza saidia!

Umeona kwa KING MSWATI?watu walikuwa pimbi tu kwa miaka lakini wamechoka, sasa kwao ni sehemu nzuri ya kuanzia.hivi kweli kuna kiongozi wa Africa anapenda kupunguziwa madaraka kirahisi tu?!!
 
Hakika Rais Mstaafu JAKAYA KIKWETE pamoja na kuwa NDOTO yake ya KUWAPATIA WATANZANIA KATIBA MPYA Haikutimia Bado Ataendelea kuwa BABA wa KATIBA Aliyethubutu Kutupatia KATIBA MPYA....
Tunatakiwa kumsaidia Rais, nyuma yake kuna Wahafidhina, walewale waliomgeuza Kikwete akaachilia mbali nia yake njema ya kuleta Katiba mpya.

Pia ni fundisho kwetu watanzania. Tunapenda vya bure. Katiba mpya kwa Kenya ilikuwa matokeo ya mapambano makali. Tunatakiwa kutambua kwamba CCM hawawezi kukubali kuondoka kwenye chama dola bila mapambano
 

..hata wana-ccm waliodhalilishwa na kudukuliwa kipindi cha mwendazake nao hawataki katiba mpya?
 
..hata wana-ccm waliodhalilishwa na kudukuliwa kipindi cha mwendazake nao hawataki katiba mpya?
Hao ndiyo wenye nchi kwa Sasa. Wanaotamani katiba mpya ni wale wanaccm waliodukuwa mazungumzo ya wazee wakati wa mwendazake.
 
Hao ndiyo wenye nchi kwa Sasa. Wanaotamani katiba mpya ni wale wanaccm waliodukuwa mazungumzo ya wazee wakati wa mwendazake.

..Nasikia wanamuombea Mama kifo.

..kwasababu wenzao waliomba na ikatokea na wenyewe wanadhani maombi yao yatatiki.
 
Hapo kinachokwepwa ni kuporomoka kwa Muungano. Hakuna Rais atakayekubali Muungano uvunjikie kwake so hizo danadana tutegemee kuziona Sana tu. Wacheni tujenge uchumi kwanza.
 
Ndio, Hawa jamaa Mimi siwaelewi wanataka nini. Mama kaingia juzi tu ikulu amesema suala la katiba mpya tumpe muda kwann tusimpe huo muda anaotaka tungemuuliza tu unataka tukupe muda gani

Ni kweli katiba yetu ya sasa ina mapungufu kibao na ni zao la ccm lkn mama anakutana na makundi mbali mbali muda wa vyama vya siasa bado tungesubiri siku ya kukutana nae tuongee nae tumweleze wapi tulipokwama na ili twende mbele tuanzie wapi badala yake mnamtisha eti tutamnyoa kama tulivomnyoa mwenda zake mmmh hii Ni hatari
 
Hivi we unadhani muda gani unamtosha rais wetu kupewa? Kwa upande wa mikutano ya kisiasa mama kakosea, yeye alipaswa kuhimiza sheria na katiba zifuatwe ndo kiapo chake
 
Reactions: BAK
Mkuu kwani tunawahi wapi tumekaa miaka 5 hakuna mikutano ya siasa huyu kaomba muda na atatuita tukae nae tuone namna ya kuyafanya haya tunaanza kumtisha
 
Reactions: BAK
Hivi we unadhani muda gani unamtosha rais wetu kupewa? Kwa upande wa mikutano ya kisiasa mama kakosea, yeye alipaswa kuhimiza sheria na katiba zifuatwe ndo kiapo chake
msaada katiba kwa ujumla inasemaje kuhusu mikutano ya kisiasa nje ya kampeni!!!!

maana mama anasema ya ndani rukhsa.
 
Kwani sheria zinasemaje juu ya mikutano ya kusiasa?
Mkuu kwani tunawahi wapi tumekaa miaka 5 hakuna mikutano ya siasa huyu kaomba muda na atatuita tukae nae tuone namna ya kuyafanya haya tunaanza kumtisha
 
Reactions: BAK
Unajua hawa jamaa wamekosa pakumshikia mama sasa wameona hapo ndio pakumshikia maana sehem zote zenye ukakasi amezilegeza wameona wapige mawe yao kwenye katiba mpya [emoji23][emoji23] maana hata wakiacha ilo swala watakuwa hawana maneno mtaani kuhisu serikali
 
Kaa kimya kama huna akili. Siasa siyo hisani ya samia ni haki ya kila raia. Ccm haiwezi kujichinja yenyewe lazima ichinjwe. Unakumbuka uchafuzi wa wa mwaka jan! Ccm walitangazana tu kushinda hata bila kushinda.
 
Umenifikirisha sana hilo neno OVYO nlikua sijapata maana yake. Sasa niliposoma main body ndio nimegundua ulimaanisha HOVYO..!

Labda kuna kitu hatukijui kwa hawa CDM. Hawa jamaa wana mission sana, hili walilokuja nalo ni propaganda, wanatest validity. Sasa serikali ikijichanganya tu jamaa wanapewa point 3 mchana kweupe. But ninachokiamini Mama yupo smart sana, plus ile timu ya ushauri wa pale kasrini hili ni dogo sana, huu mchezo ulishachezwa zamani hivyo washaujua, kwa hiyo tulieni tu mambo hayaharibiki. Kazi Iendelee.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…