Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Baada ya kusikia maneno ya viongozi wangu wa Zanzibar... nilitaka sasa kuangalia ukweli uko wapi?

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
RAIS
Rais wa Jamhuri ya Muungano Sheria ya 1984 Na.15 ib.9

33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.
 
Z`bar wagawanyika

2008-07-27 14:25:40
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Suala la Zanzibar kuwa nchi au si nchi limewagawa wananchi wa visiwani hapa wengine wakiunga mkono kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wengine wakipinga.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Zanzibar walisema umefika wakati wa kuanzishwa Mahakama ya kikatiba ili iweze kutoa tafsiri sahihi juu ya suala hilo.

Mkazi wa Chukwani, Bw. Shabani Salum, alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 126 imesema kutakuwepo na mahakama ya kikatiba ambayo haijaundwa tangu kuungana kwa nchi za Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964.

``Kwa mtazamo wangu hakuna mtu anayeweza kutoa tafsiri sahihi zaidi ya mahakama ya Katiba�suala hili si la kisiasa bali linahusu mambo ya kisheria,`` alisema Bw. Shabani.

Alisema kwamba mvutano uliojitokeza hivi sasa umesababishwa na waasisi wa muungano kutowashirikisha kwa karibu wanasheria wakati walipokuwa wakikubaliana mambo 11 ya Muungano.

Naye Bw. Said Millo (53), mkazi wa Kikwajuni, alisema ufumbuzi wa kutatua kero za muungano ni kuwepo kwa serikali tatu.

Alisema kwa maoni yake Zanzibar sio nchi kwa vile utaifa wa Zanzibar ulikufa kama wa Tanganyika ulivyokufa mara baada ya kusainiwa kwa Muungano wa nchi hizo.

``Suala hili Waziri Mkuu Pinda hakuhitaji kuulizwa, liko wazi kabisa katika Katiba yetu�wakulaumiwa hapa ni Wazanzibari wenyewe,`` alisema Millo.

Alisema kabla ya marekebisho ya 11 ya Katiba, Rais wa Zanzibar alikuwa Makamu wa pili wa Rais wa Muungano, lakini Wazanzibari kupitia vikao vya Bunge na CCM walipitisha marekebisho hayo.

``Mamlaka ya Zanzibar ilianza kupotea kuanzia hapa, sasa nani wa kulaumiwa wakati haya yalifanyika katika vikao halali,`` alisema Millo.

Naye mkazi wa Michenzani, Bw. Othman Magomba (56), alisema jambo la msingi hivi sasa ni pande mbili za Muungano kukaa na kujadili kero zinazojitokeza za kisiasa na kiuchumi.

``Zanzibar ilikuwa nchi kamili lakini sisi wenyewe Aprili 26, tukaamua kuinganisha na Tanganyika, sasa SMZ wasitutafutie mchawi ambaye anajulikana kuwa ni wao wenyewe,`` alisema Bw. Othman.

Alisema malalamiko yanayotolewa na wanasiasa hivi sasa hayana tofauti na msemo wa Kiswahili `maziwa yakimwagika hayazoleki`.

Mkazi huyo alisema ni jambo la kushangaza tangu kufikiwa Muungano huo asilimia 80 ya Wazanzibari hawaitambui Katiba ya Muungano na hivyo kushindwa kufahamu mambo ya msingi ya muungano na yasiyokuwa ya muungano.

Naye mkazi wa Mbweni, Mwajuma Shalah, alisema anaunga mkono kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bw. Iddi Pandu Hassan, kuwa Zanzibar ni nchi kwa vile baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Serikali ya Tanganyika iliingizwa katika Serikali ya Muungano wakati Serikali ya Zanzibar iliendelea kubakia hadi hivi sasa.

``Kwa kweli Waziri Mkuu atuombe radhi Wazanzibari sisi tunachagua Rais, na huwezi kuwa na Rais bila ya kuwa na nchi�sasa Rais wetu ni wanchi gani?

Alihoji Mwanajuma.
Naye Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Bw. Mohamed Raza, alisema hakuna wa kutengua kitendawili hiki zaidi ya Rais Jakaya Kikwete na Rais Amani Karume kutoa tamko la pamoja ili kuuzima mjadala huo.

Alisema CCM Zanzibar itakuwa katika wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 endapo viongozi wa CCM Bara wataendelea kusisitiza kuwa Zanzibar si nchi.

``CCM Zanzibar itakuwa katika wakati mgumu kushinda uchaguzi wa mwaka 2010 iwapo itasisitiza kuwa Zanzibar si nchi, Wazanzibari watashindwa kujua wanampigia kura Rais wa mkoa wa wilaya`` alisema Raza.

Naye Makamu Mwenyekti wa NCCR-Mageuzi, Bw. Khamis Hambar, alisema mtego huo unaweza kunasuliwa na mahakama ya katiba pekee.

Alisema kimsingi, Zanzibar ni nchi lakini haina mabawa kwa vile mamlaka yake yanaishia ndani ya Tanzania huku ikiwa haina uwezo katika nyanja za kimataifa hasa utiaji wa saini wa mikataba ya kimataifa.

Alisema pande mbili za Muungano zianzishe haraka mahakama ya katiba badala ya suala hilo kujadiliwa na CCM kwa vile linahusu wananchi na si vyama vya siasa.

Hivi karibuni Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema Zanzibar si Nchi kwa vile Tanzania ni nchi moja yenye serikali mbili ya Zanzibar na ya muungano na eneo lote la ardhi Bara na Zanzibar pamoja na eneo la usawa wa bahari ni sehemu ya Jamhuri ya muungano.

Hata hivyo, kauli ya Waziri Mkuu ilipingwa na Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Bw. Iddi Pandu Hassan, ambaye alisema baada ya Muungano Serikali ya Tanganyika, iliingizwa ndani ya muungano na SMZ ilibakia na kusisitiza kuwa haiwezekani kuwa na Serikali bila ya kuwa na nchi .
 
Yap, Kazi ipo sii mxhezo mdogo...
Kuna kila haja ya kuwepo serikali tatu laa sivyo Zanzibar wamefungashiwa Kanyaboya! tena vibaya sana.. Ndio maana siku zote wanauliza kuhusu katiba ya muungano iliundwa vipi!..Now I know, kwa sababu kama kweli kulifanyika uhuni kama vile mikataba ya madini ya kina Mkapa naweza kuona nje ya kivuli changu mwenyewe. Kupinga kwetu mikataba hii haina maana sisi Watanzania hatutaki kuwepo kwa Barricks nchini isipokuwa makubaliano yenyewe ndio yalikuwa na mashaka..

Hivyo basi Zanzibar wana kila haki ya ku question uundwaji wa Katiba hiyo mbali kabisa na kuwepo Muungano wenyewe.

Lakini wakuu mmeona jinsi ilivyo kazi kubwa kuitafsiri NCHI na SOVEREIGN..Matatizo haya yapo hadi hapa Canada ambako Quebec wanadai kila siku kwamba wana sovereign (tafsiri ya Kifaransa) jambo ambalo linakataliwa na serikali kuu (Tafsiri ya Muingereza)..
 
Kesi ya Uhaini dhidi ya Zanzibar ya Machano Ali sio yenye mamlaka hapa, wala haihusiki hapa, siyo "precedent," kwa sababu haikutoka katika mahamaka maalum ya kutatua migogoro ya tafsiri ya Katiba baina ya Zanzibar na Muungano kwa mujibu wa Ibara ya 126. Majaji wanaweza kuiangalia kupata mwongozo, "persuasive authority," lakini haihusiki, haiko "on point."

Na hata kama ingekuwa inahusika swala la Muungano bado sio "settled." Linaweza kurudi mahakamani. Mahakama ikishaamua jambo halafu bado kukawa na mtafaruku katika jamii, na kesi bado zinaletwa kuhusu ishu hiyo hiyo hiyo, basi swala hilo huwa linasemwa haliko "settled." Na majaji huwa wanajisikia hawakueleweka, na labda hata walikosea, manake legal community nzima na Wananchi bado wana maswali. Msingi mama mmoja wa Utawala wa Sheria ni kwamba sheria lazima zieleweka. Kukiwa na utata katika tafsiri fulani Mahakama huwa inajisikia kama imefeli kazi.

Katika mazingira hayo, Mahakama inaweza kuchukua kesi ya hilo swala tena na kuliamua upya, kufafanua au kukarabati vipengele tata vya uamuzi wa awali, na mara nyingine kufuta kabisa uamuzi wao wa awali. Yani, kuu-repeal au kuu-overturn.

Sio kweli kwamba Mahakama inabananwa kisheria na maamuzi yake ya nyuma. Mfumo wa kufuata "precedents," unaoitwa "stare decisis," ni utaratibu wa jadi za kisheria tu, na sio mamlaka ya kumbana Jaji. Hakuna mahala katika Katiba wala Sheria nyingine ilipoandikwa kwamba Jaji afuatishe maamuzi ya Jaji mwezake ya nyuma. Ni msingi uliojengeka kiutamaduni tu, kwamba maamuzi "yaachwe kama yalivyo" au "stare decisis." Lakini yanaweza kubadilishwa.

Juzi limeulizwa swali bungeni, Katiba na Hati za Muungano kipi kiko juu? Pinda, akachomoa. The point of the question ni kwamba Pinda aliponukuu Katiba kuhusu status ya Muungano sio ilibidi anukuu Hati ya Muungano inasemaje, ambayo ndio mkataba wenyewe? Sasa ile kesi ya Haini haikuchimbua maswala ya Hati ya Muungano v/s Katiba. Wala maswala mengine kama vile imekuwaje mambo 11 yaliyokuwemo kwenye Hati ya Muungano yameongezwa madodolisho mengine na ku mushroom kufikia 23.

Mimi swali langu binafsi ambalo nataka hizo kesi za mbele zi settle ni hili: nani kawahi kuiona hati ya Muungano yenye saini mbili? Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alipoambiwa ailete mahakamani Hati ya Muungano kwenye kesi ya Muungano ya 2003 alisema hajawahi kuiona. Ikasemekana haipo. Nakala zote mbili zimeenda wapi kati ya ile ya Karume – kama alipewa copy – na ile aliyobaki nayo Mkuu wa Wakuu wa Kaya?

Habari bado mbichi hii!
 
Kuhani
Umeongea vizuri sana kwamba suluhisho la tatizo hili la muungano litapatikana baada ya kupata hizo hati zilizo sainiwa na wale wakuu wa wakuu wa kaya wawili,yaani JKN na Karume senior,kama hilo haliwezekani basi ni kutumia multi-approach ikiwemo au kuunda interim constitutional court kwajili ya kuclea utata wote huo basing on evidence and argument presented au kwa serikali hizi zote mbili kukaa chini na kuangalia utata uko wapi huku wakihusisha wanachi katika kutatua suala hilo.

Pia nashukuru leo kwa kukubali kuwa mahakama hutumia pia legal tradition hasa hiyo doctrine of precedents au stare decisis,ila tu kwa madhumuni ya kuwekana sawa naomba nikusahihishe kidogo kwenye hili

Sio kweli kwamba Mahakama inabananwa kisheria na maamuzi yake ya nyuma. Mfumo wa kufuata precedents, unaoitwa stare decisis, ni utaratibu wa jadi za kisheria tu, na sio mamlaka ya kumbana Jaji. Hakuna mahala katika Katiba wala Sheria nyingine ilipoandikwa kwamba Jaji afuatishe maamuzi ya Jaji mwezake ya nyuma. Ni msingi uliojengeka kiutamaduni tu, kwamba maamuzi yaachwe kama yalivyo au stare decisis. Lakini yanaweza kubadilishwa

Ni kuwa mahakama ni kweli kuwa zinafungwa kufuata maamuzi yake ya nyuma,kwa maana ya kwamba mahakama ya rufaa ikitoa uamuzi uamuzi huo unaifunga mahakama hiyo,vilevile unazifunga mahakama zote za chini yake ikiwamo mahakama kuu unless uamuzi huo ukawa over rulled na mahakama hiyo hiyo ya rufani kwa kutoa practice statement.Vivyo hivyo kwa mahakama kuu na mahakama zilizoko chini yake. Mahakama ambazo hazitengenezi precedent ni zile zilizoko chini ya mahakama kuu.

Na kwa maana hiyo basi "The court of appeal of Tanzania is bound by its own decision and it is also free to epart from its own previous decision when it is right to do so". Na katika hili ndio pale uliposema kuwa ikiona kuwa ilitoa decision ambayo tayari ni precedent na baadaye decision hiyo kuonekana per incurium basi inaweze kureverse uamuzi huo katika jopo la majaji kwa kauli inayoitwa practice statement kama ilivyowahi kufanya katika kesi ya JUWATA VS.KIUTA,ikioverrule Tanzania Zambia Railway.... vs.Palangyo. Uwezo huu Mahakama yetu ya rufani imerithi kutoka iliyokuwa mahakama ya rufani ya afrika mashariki ambayo na yenyewe iliurithi kutoka Privy council ya uingereza.

Zaidi ya hapo nakubaliana na wewe kuhusu namna ya kutafuta suluhu ya Muungano.

With due respect i beg to submit
 
A strong reflection is quoted from the learned Judges, below ... and many can argue the mandate of the Judiciary on this Union issues, but check me, their arguments is mind boggling: Rich, Authoritative.

This is not an insult, but perhaps there are very few people who possess the same capacity of critical thinking in the Clove-rich Isles. This however, does not belittle their natural right to question their participation in the Union.

Ask for my opinion, I am not that in favour of the Union with Zenj... Come on, those chaps want to walk on their feet, finally, let 'em loose. Does the mainland have anything to lose if we let them go? Come on, check me... we have so much of other important business to catch up as we try to evict ourselves from abject poverty.
Let them go. Let them loose, please.:

[QUOTE]...May be this is the proper juncture to turn to the question posed by Mr. Mbwezeleni: is Zanzibar a sovereign state in international law?

After the above exposition, we have no difficulty at all to answer that question in the negative. The International Persons called Tanganyika and Zanzibar ceased to exist as from 26th April, 1964 because of the Articles of Union. The two states merged to form a new international person called the United Republic of Tanzania.

The Rt. Hon. The Earl of Birkenhead has said at page 36: "A nation cannot indefinitely surrender the treaty-making power to another, and at the same time retain its existence as a sovereign state". We concur with this contention and we wish to point out that both Tanganyika and Zanzibar, and not Zanzibar alone, surrendered their treaty-making powers to the United Republic of Tanzania.

Thus, Zanzibar, just like its sister Tanganyika, is neither a state nor is it sovereign. The state and the sovereign is the United Republic of Tanzania...
[/QUOTE]
 
Zanzibar haina uwezo wa kuingia au kuanzisha mahusiano ya kimatafa na nchi zingine kwa kuwa uwezo huo uko kwenye mamlaka ya 'Nchi" kwa mujibu wa sheria za kimataifa kama walivyosema majaji, nayo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa wao Zanzibar kama wanadhani kimataifa wanajulikana kwamba ni nchi, basi wamenoa. Ukisoma kwa makini hukumu hiyo, hoja zote zinazobishaniwa zimeongelewa kwa ufasaha pamoja na kwamba main issue was "treason".

Nadhani ili ubishi huu ufikie kikomo, suluhisho ni kulipeleka kwenye mahakama ya katiba, maana sasa imekuwa ni mgogoro, pamoja na kwamba viongozi wetu hawataki kukubaliana na hili. Kitendo cha Shamhuna kutoa tamko la kupingana na waziri mkuu, tayari ni mgogoro wa kikatiba, wanaweza kukaa kama chama wakayazungumza ndani kwa ndani, lakini suala hili sasa siyo la chama ni la wananchi wote wa Jamhuri ya muungano wa Tannzania. Kwa hiyo, ili uwazi wa kulizungumza uwepo, ni kulipeleka kwenye mahakama ya katiba.
 
Waheshimiwa,

WaZanzibar wa/tunajua kwamba kwa kufuata katiba hawa/hatuwezi kushinda... ndio maana tuna/wanashinikiza kujua lipi liko juu MOU (yaani article of association za muungano) au Katiba...

siku mkisema Katiba ya 1977 ndio ina-prevail... tuta/wata-withdraw statement.
 
...Pia nashukuru leo kwa kukubali kuwa mahakama hutumia pia legal tradition hasa hiyo doctrine of precedents au stare decisis,

Unakosea tena.

Ulipokuwa unaeleza inakuwaje Majaji wana nguvu ya kutengua sheria batili papo hapo (kama kesi ya Takrima) bila kusubiri Serikali iirekebishe ( kama Ibara ya 30 (5) inavyosema) ilidai ni “nguvu za asili” au “inherent power” za mahakama. Ninakwambia hicho kitu kama ulivyokieleza hakipo. Mahakama haiwezi kutofuata Katiba eti kwa vile ina “nguvu za asili.” Ikaonekana ulikuwa unachanganya nguvu ya asili ya kusikiliza kesi “original jurisdiction” na nguvu ya mahakama kutafsiri na kutangua sheria mbovu “Judicial Review.” Sasa hapa unachanganya tamaduni za sheria “legal tradition,” na hizo “nguvu za asili,” kitu ambacho hakipo.

Utamaduni wa Kisheria, au “legal tradition” sio “nguvu za asili” za kuipa mahakama mamlaka ya kwenda kinyume na Katiba na sheria za vitabuni. Hakuna “nguvu za asili.” Mahakama za Tanzania zinapata uwezo wa kutangua sheria batili papo hapo ( tofauti na Ibara ya 30 (5) inavyoshauri) kwa sababu kuna Ibara nyingine, ya 64 (5), inaipa hiyo nguvu, sio “nguvu za asili.” Hakuna kitu kama hicho.

...ila tu kwa madhumuni ya kuwekana sawa naomba nikusahihishe kidogo kwenye hili. Ni kuwa mahakama ni kweli kuwa zinafungwa kufuata maamuzi yake ya nyuma,kwa maana ya kwamba mahakama ya rufaa ikitoa uamuzi uamuzi huo unaifunga mahakama hiyo,vilevile unazifunga mahakama zote za chini yake ikiwamo mahakama kuu unless uamuzi huo ukawa over rulled na mahakama hiyo hiyo ya rufani kwa kutoa practice statement.Vivyo hivyo kwa mahakama kuu na mahakama zilizoko chini yake.Mahakama ambazo hazitengenezi precedent ni zile zilizoko chini ya mahakama kuu.Na kwa maana hiyo basi "The court of appeal of Tanzania is bound by its own decision and it is also free to epart from its own previous decision when it is right to do so".

Sio kweli.

Kama mahakama inaweza kutengua uamuzi wake, kama ulivyosema “and it is also free to [epart] from its own previous decision when it is right to do so" basi haifungwi. Sasa, sijui kama ni hoja zako au za wenzako, maana nukuu yako zimetoka wapi, zaidi ya kutupa sentensi yenye alama za kunukuu, lakini unajifunga funga.

Kingine, hatuongelei nguvu ya maamuzi ya Mahakama juu ya zile mahakama za chini, usichanganye habari. Tunaongelea Mahakama ile ile inapokuwa na kesi kuhusu swala lililowahi kuamuliwa na mahakama ile ile siku za nyuma. Mahakama za chini hazihusiki hapa. Ukitenganisha vitu tofauti hutajichanganya na kuvikosea.

Mahakama inao uwezo wa ku overturn uamuzi wake yenyewe, haibanwi. Na hakuna "nguvu za asili" za mahakama kwenda tofauti na Katiba ya nchi.
 
Unakosea tena.

Ulipokuwa unaeleza inakuwaje Majaji wana nguvu ya kutengua sheria batili papo hapo (kama kesi ya Takrima) bila kusubiri Serikali iirekebishe ( kama Ibara ya 30 (5) inavyosema) ilidai ni "nguvu za asili" au "inherent power" za mahakama. Ninakwambia hicho kitu kama ulivyokieleza hakipo. Mahakama haiwezi kutofuata Katiba eti kwa vile ina "nguvu za asili." Ikaonekana ulikuwa unachanganya nguvu ya asili ya kusikiliza kesi "original jurisdiction" na nguvu ya mahakama kutafsiri na kutangua sheria mbovu "Judicial Review." Sasa hapa unachanganya tamaduni za sheria "legal tradition," na hizo "nguvu za asili," kitu ambacho hakipo.

Utamaduni wa Kisheria, au "legal tradition" sio "nguvu za asili" za kuipa mahakama mamlaka ya kwenda kinyume na Katiba na sheria za vitabuni. Hakuna "nguvu za asili." Mahakama za Tanzania zinapata uwezo wa kutangua sheria batili papo hapo ( tofauti na Ibara ya 30 (5) inavyoshauri) kwa sababu kuna Ibara nyingine, ya 64 (5), inaipa hiyo nguvu, sio "nguvu za asili." Hakuna kitu kama hicho.



Sio kweli.

Kama mahakama inaweza kutengua uamuzi wake, kama ulivyosema "and it is also free to [epart] from its own previous decision when it is right to do so" basi haifungwi. Sasa, sijui kama ni hoja zako au za wenzako, maana nukuu yako zimetoka wapi, zaidi ya kutupa sentensi yenye alama za kunukuu, lakini unajifunga funga.

Kingine, hatuongelei nguvu ya maamuzi ya Mahakama juu ya zile mahakama za chini, usichanganye habari. Tunaongelea Mahakama ile ile inapokuwa na kesi kuhusu swala lililowahi kuamuliwa na mahakama ile ile siku za nyuma. Mahakama za chini hazihusiki hapa. Ukitenganisha vitu tofauti hutajichanganya na kuvikosea.

Mahakama inao uwezo wa ku overturn uamuzi wake yenyewe, haibanwi. Na hakuna "nguvu za asili" za mahakama kwenda tofauti na Katiba ya nchi.

Kuhani
Inawezekana shule ya sheria uliyosoma mwenzangu au mwenzetu ni tofauti kabisa na tuliyosoma wenzio au level ya taaluma ya sheria uliyonayo wewe ni tofauti na mimi,labda ndio maana tunadiffer sana kwenye very very fine things na wakati mwingine mbali kabisa.Kama ni Shivji huyu huyu,Kanywanyi,Mwaikusa,Makaramba na Dr.Mapunda bila kumsahu Marehemu Mkoyogo, ndio walionifundisha mimi na ndio hao wamezalisha walhadhiri wengine wa sheria nchini ndio wamekufundisha na wewe basi mmh, there must be a problem somewhere,labda wengine.Siamini kabisa wewe kama mwanasheria unakanusha general principel of law "kuwa mahakama inafungwa na maamuzi yake yenyewe".Ningeappreciate sana ungeniambia kuwa "Mahakama kufungwa na maamzui yake yenyewe" ni general principle lakini pia ina exception.Kwa taarifa yako hiyo quotation sijaitoa mimi,imo kwenye kesi ya JUWATA Vs KIUTA ambapo mahakama ya rufani ndiyo iliyoitoa,pia zipo kesi nyingine kama 5 hivi zina hiyo statement.Kama wapo first year law hapa wanaweza kutusaida zaidi.

Pili,umesema kuwa "
Kingine, hatuongelei nguvu ya maamuzi ya Mahakama juu ya zile mahakama za chini, usichanganye habari. Tunaongelea Mahakama ile ile inapokuwa na kesi kuhusu swala lililowahi kuamuliwa na mahakama ile ile siku za nyuma. Mahakama za chini hazihusiki hapa. Ukitenganisha vitu tofauti hutajichanganya na kuvikosea
Hapa ndugu yangu hakuna habari iliyochanganywa katika doctrine of precedent naomba nikukumbushe kuwa kuna verticacl binding obligation na horizontal binding obligation.Vertical binding ndio hilo unalolizungumzia yaani "nguvu za maamuzi ya mahakama juu ya zile mahakama za chini, wakati horizontal binding, ndio nguvu za maamuzi ya mahakama kuifunga mahakama yenyewe iliyotoa maamuzi hayo.Kwa maana hiyo basi, Mahakama zinazofungwa na maamuzi yake zenyewe ni mbili tu,HIGH COURT na COURT of APPEAL ,na ndio hizi pia zimepewa uwezo wa ku "depart from its own previous decision when it is right to do so".Narudia tena usemi wa "The Court of appeal of Tanzania is free to depart from its own previos decision when it appears right to do so" ulitolewa kwenye kesi ya JUWATA vs. KIUTA na pia utaikuta katika kesi ya BI HAWA MOHAMMED VS ALI SEFU.[1983]TLR 6.Na when it appears right to do so, ni wakati moja,kuna conflicting decision kuhusu jambo fulani let say kuna decision mbili za mahakama moja inasema zanzibar ni nchi,nyingine inasema sio nchi,mbili,kunapkuwa na uamuzi uliotolewa kwa kukosewa au kwa kugha ya kistaarabu kwa kupitiwa(decision per incurium).Mahakama pia ilirudia kauli hii na kujadili haya mambo ya kufungwa au kutofungwa katika kesi ya ABOUHARY AZIZI na wenzake.Hivyo ni general principle of law mahakama kufungwa na uamuzi wake yenyewe na exception ni pale inapoona yafaa kutengua uamuzi wake yenyewe wa awali.Hii ndiyo correct legal position nenda popote pale Tanzania.

Kwa kuongezea tu,kuna mahala ulitaja persuasive, decision ya mahakama ambayo sio conflicting au per incurium ni binding kwa mahakama ikiwa ilitolewa na mahakama kuu au ya rufaa(japokuwa maaamuzi ya mahakama kuu hayaifungi mahakama ya rufaa) na haijawa overrruled.Decision ambayo ni persuasive ni ile iliyotolewa nje ya geographical jurisdiction ya mahakama ya tanzania.Mfano ukichukua maamuzi ya iliyokuwa EACA,PRIVY COUNCIL,na maamuzi yoyote ya mahakama ya nchi za jumuiya ya madola ni ya kiushawishi tu,hayaifungi mahakama.Sana sana mahakama ikitaka kukwepa kutumia uamuzi fulani ambao haujawa overruled mf.hizo kesi za uhaini tulizozitaja japokuwa zinagusia zanzibar kuwa nchi au la,mahakama hiyo itafanya distinguishing.



Tatu, naomba nikanushe kuwa nilisema nguvu za asili za mahakama zinairuhusu mahakama kwenda kinyume na katiba,kama kweli nilisema na hiyo kauli ipo hapa,basi hapo naomba nikiri mbele ya wanajopo kuwa niliteleza lakini kama ni tafsiri yako wewe tu ya maneno yangu sikubaliani nayo kabisa.Nguvu za asili hata siku moja haziiruhusu mahakama kwenda kinyume na katiba ila zinairuhusu mahakama kuweza kutangua(nullify) au kubatilisha sheria inayokwenda kinyume na katiba kwa kuwa wajibu mojawapo wa mahakama ni kulinda katiba.Japo upo wakati ambapo mahakama inaweza kutumia mbinu ya interpretation kupata nguvu inayoifeva yenyewe dhidi ya kipengele fulani cha katiba, mathalani pale katiba inaposema sema "matokeo ya uchaguzi wa rais hayatahojiwa na chombo chochote ikiwemo mahakama"ibara ya 41(7)mahakama inaweza kutumia mbinu ya tafsiri kupata jurisdiction ya kusikiliza kesi hiyo japo haijawahi kutokea Tanzania ila kwingineko imewahi kutokea na kipengele kama hicho cha katiba kina athari ya kuiondole mahakama jurisdiction kusikiliza kesi ya matokeo ya uchaguzi wa Rais mara baada ya Rais kutangazwa.

Nne, hakuna kitu nilichochanganya kama ulivyosema hapa, nanukuu"
Ikaonekana ulikuwa unachanganya nguvu ya asili ya kusikiliza kesi "original jurisdiction" na nguvu ya mahakama kutafsiri na kutangua sheria mbovu "Judicial Review

Naomba nikusahihishe judicial review sio nguvu za mahakama kutafsiri na kutangua sheria mbovu,la hasha,judicial review ni nguvu au mamlaka ukipenda uwezo wa mahakama kutengua maamuzi ya viongozi wa serikali,sio sheria zilizotungwa na bunge.Hata siku moja ukitaka kuchallenge sheria iliyotungwa na bunge huwezi kwenda by judicial review,lazima uende by way of petition or originating summons.Ila ukitaka kuchallenge umauzi let say wa kukuweka ndani bila kukufungulia mashataka,uamuzi wa waziri au halmashauri kutunga by-law fulani bila kuwahusisha wananchi au kufuata procedure nk,ndio unaenda by judicial review.Hapa unachallenge mamlaka ya mtu mwenye mamlaka kufanya kitu fulani

Tano, unapozungumzia original jurisdiction, original jurisdiction sio inherent power zinazozungumziwa. Original jurisdiction ni uwezo wa kusikiliza kesi yoyote hata kama hakuna sheria inayoipa mamlaka mahakama kushughulikia kesi hiyo. Original jurisdiction tayari imeshasemwa kwenye katiba ibara ya 108(2) "
Iwapo Katiba hii au sheria nyingine yoyote haikutamka wazi
kwamba shauri la aina iliyotajwa mahususi litasikilizwa kwanza
katika Mahakama ya ngazi iliyotajwa mahsusi kwa ajili hiyo, basi
Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kila shauri la
aina hiyo.
Na hakuna mahali niliposema kuwa eti inherent power zinairuhusu mahakama kwenda kinyume na katiba,si kweli kwani katiba yenyewe ndio imeziappreciate hizo power. Hata isingekuwepo ibara ya 64(5) bado mahakama ingeweza tu kunullify sheria ambayo inapingana na katiba.Wakati, Inherent power ni power ambazo zinahusisha hata hiyo judicial review is a wide range of powers sio moja au 2.

Ulipokuwa unaeleza inakuwaje Majaji wana nguvu ya kutengua sheria batili papo hapo (kama kesi ya Takrima) bila kusubiri Serikali iirekebishe ( kama Ibara ya 30 (5) inavyosema) ilidai ni "nguvu za asili" au "inherent power" za mahakama. Ninakwambia hicho kitu kama ulivyokieleza hakipo. Mahakama haiwezi kutofuata Katiba eti kwa vile ina "nguvu za asili." Ikaonekana ulikuwa unachanganya nguvu ya asili ya kusikiliza kesi "original jurisdiction" na nguvu ya mahakama kutafsiri na kutangua sheria mbovu "Judicial Review." Sasa hapa unachanganya tamaduni za sheria "legal tradition," na hizo "nguvu za asili," kitu ambacho hakipo.

Utamaduni wa Kisheria, au "legal tradition" sio "nguvu za asili" za kuipa mahakama mamlaka ya kwenda kinyume na Katiba na sheria za vitabuni. Hakuna "nguvu za asili." Mahakama za Tanzania zinapata uwezo wa kutangua sheria batili papo hapo ( tofauti na Ibara ya 30 (5) inavyoshauri) kwa sababu kuna Ibara nyingine, ya 64 (5), inaipa hiyo nguvu, sio "nguvu za asili." Hakuna kitu kama hicho

Hapo juu kwenye maneno niliyoyafungia kuna kitu mimi na wewe hatukuelewana.Ile makala niliyoandika iligusa vitu vingi sana kwa ufupi,na pia ilieleza historia ya hizo inherent power.Haikuwa tu na lengo la kujibu kitu kimoja "kesi ya mgombea binafsi au ibara ya 30(5)" na ndio maana labda ukashindwa kunipata vyema.Nakubaliana na wewe kabisa bila kukupinga kuwa uwezo wa kufuta sheria papo hapo kama ilivyofanya kwenye kesi ya Takrima unatokana na express power zilizopo katika ibara ya 64(5) ya katiba japokuwa ibara hiyo bado haisemi kuwa "sheria hiyo itafutwa na mahakama" yenyewe inaishia kusema tu kuwa sheria iliyo kinyume na katiba itakuwa batili kwa extent ya kukinzana kwake.Na kuendelea kutumika kwa sheria ambayo ni kinyume na katiba hadi hapo serikali itakapoirekebisha au muda iliopewa na mahakama uishe inatokana na ibara ya 30(5) hivyo ndio kusema kwa kutumia ibara hiyo mahakama imepewa mamlaka ya kuifanya sheria inayopingana na katiba kuendelea kutumika kwa kipindi maalumu hadi ama kitakapoishi au kurekebishwa na serikali.Hivyo katika kipindi hicho kilichowekwa na mahakama japokuwa sheria hiyo inakinzana na katiba,bado itakuwa halali kutumika hadi muda huo upite.Sasa kwa kuwa mahakama kwa kawaida (legal tradition)kutokana na doctrine ya checks and balance ndiyo hubatilisha sheria? ndio maana neno inherent power likaja.Lengo la kusema wanayo inherent power ni kwa lengo la kuappreciate kuwa mahakama hata bila ibara hiyo ya 64(5) bado ingekuwa na huo uwezo wa kutengua unless tu kama kungekuwa kuna express provision ya katiba inayoikataza kufanya hivyo.Hivyo basi ukitaka kuelewa mamlaka ya mahakama katika kufuta sheria ama kuibakiza art.30(5) must be read together with articles 64(5) na 108(2).Nakumbuka nilikuuliza tamaduni za sheria wewe unazieleweje au ni zipi lakini hukunijibu.Na mimi kila nachokujibu najitahidi kufanya research na kukupa authority hata kama wakati mwingine unazikataa hata bila kuleta alternative authority.



Kuhusu inherent power, katiba haikuishia hapo ikaendelea katika ibara ya 108 hiyo hiyo "
Hali kadhalika Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa
kutekeleza shughuli yoyote ambayo kwa mujibu wa mila za
kisheria zinazotumika Tanzania shughuli ya aina hiyo kwa
kawaida
hutekelezwa na Mahakama Kuu

Sasa wasomi wenzio(wanasheria) hizo mila za kisheria ambazo kwa kawaida hutekelezwa na mahakama mila hizo kwa mujibu wa wanazuoni mbalimbali Shivji akiwemo zinahusisha wameziita inherent power mambo mengi zikiwemo matumizi ya precedents.Na kwa mujibu wa ibara hiyo inasemwa kuwa katiba imeziafiki hizo mila za mahakama.Kwa hiyo kama kwa kawaida mahakama kazi yake matahalani katika check and balance ni kucheck bunge,je inatekelezaje kazi hii?ni kwa kuhakikisha kuwa sheria zilizotungwa na bunge hazikinzani na katiba,basi hata kama hakuna ibara ya 64(5) kwa mujibu wa ibara hiyo ya 108 mahakama inaweza kutumia uwezo wake wa asili kubatilisha sheria.

Mfano wa pili,kazi mojawapo ya mahakama katika checks and balance ni kucheck governemnt i.e.against administrative decisions,basi itafanyaje kazi yake hiyo kwa mujibu wa legal traditions?Jibu; Kwa mujibu wa legal traditions itafanya judicial review of administrative actions.Hapa ndio itatoa mandamus,certiorari,injunctions,declarations nk.Upo hapo kaka?Hili muulize mwanazuoni yeyote wa sheria atakwambia kama nilivyosema hapao juu.Nakiri kuwa kwa level ya certificate kuyaelewa mambo haya ambayo wengine wanasoma kwa miaka 4 mwingine anasoma mwaka mmoja ni kazi mno.

Kama utaona haya niliyoyasema hapa ni uwongo,basi nakwambia andaa majibu yake yaliyotofauti na haya,yaweke hapa hoja kwa hoja bila kuongeza kitu chochote kipya kama vile unajibu submission mahakamani,halafu watu waliosoma sheria hapa jf wajudge kwa kutumia hizo submission au kama hiyo haifai basi print ipeleke kwa lecturer yeyote wa sheria akasaishe huko bongo.halafu scan copy yake iweke yapa na jina la aliyesahisha.Ningekutolea authority nyingi sana sema tu kwa kuwa sina acess ya sources mbalimbali kwa kuwa nipo nje ya nchi.
 
Last edited:
A strong reflection is quoted from the learned Judges, below ... and many can argue the mandate of the Judiciary on this Union issues, but check me, their arguments is mind boggling: Rich, Authoritative.

This is not an insult, but perhaps there are very few people who possess the same capacity of critical thinking in the Clove-rich Isles. This however, does not belittle their natural right to question their participation in the Union.

Ask for my opinion, I am not that in favour of the Union with Zenj... Come on, those chaps want to walk on their feet, finally, let 'em loose. Does the mainland have anything to lose if we let them go? Come on, check me... we have so much of other important business to catch up as we try to evict ourselves from abject poverty.
Let them go. Let them loose, please.:

[QUOTE]...May be this is the proper juncture to turn to the question posed by Mr. Mbwezeleni: is Zanzibar a sovereign state in international law?

After the above exposition, we have no difficulty at all to answer that question in the negative. The International Persons called Tanganyika and Zanzibar ceased to exist as from 26th April, 1964 because of the Articles of Union. The two states merged to form a new international person called the United Republic of Tanzania.

The Rt. Hon. The Earl of Birkenhead has said at page 36: A nation cannot indefinitely surrender the treaty-making power to another, and at the same time retain its existence as a sovereign state. We concur with this contention and we wish to point out that both Tanganyika and Zanzibar, and not Zanzibar alone, surrendered their treaty-making powers to the United Republic of Tanzania.

Thus, Zanzibar, just like its sister Tanganyika, is neither a state nor is it sovereign. The state and the sovereign is the United Republic of Tanzania
...
[/QUOTE]

Bwana,
Naomba nikupongeze sana kwa kuwa msomaji mzuri tofauti na watu wengine humu wao hukimbilia kusoma kichwa cha habari tu na kuconclude,kutokana na hilo hawayaoni mambo mengine.(Ndio kila siku tunabaki tunalalama mikataba mibovu nk,baadhi ya watu wavivu kusoma hukimbilia kusaini bila kusoma each and every word)

Sasa nadhani wewe umewafunua watu kuona kulikuwa na umuhimu gani kwetu kuweka hiyo decision hapo, tofauti na watu wengine wanavyokimbilia kuconclude kuwa haisaidii chochote. Imewekwa hapo makusudi kwa kuwa baadhi ya maswali tunayojiuliza hapa japo siyo yote yamejibiwa kwenye hiyo decision.
Big up Mkuu.
 
nafasi ya CCM katika huu muungano ni ipi? maana nasikia wamepeana majukumu ya kutatua matatizo hay
 
makamba anasema CCM haiwezi kutolea kauli suala la muungano wakati tayari tambwe hiza ameshatolea kauli. au tambwe si mwana CCM au kauli alizotoa ni zake mwenyewe?
 
Wajuzi wa katiba,
Nimejaribu kusoma katiba yetu kama alivyonisema Kuhani na nimefika point moja nimekwama kujua hii ikoje.

Katiba yetu ni RAIS anamteuwa PM na Mawaziri na yeye ndiye BOSS wa serikali hiyo. Hii kwangu haina tatizo kama tu kwa mfano Rais wa CCM na chama kilichoshinda uchaguzi na wako wengi bungeni ni CCM. Sasa ikija tokea tuseme RAIS anatoka CHADEMA au CUF au ..... na chama kilichoshinda UCHAGUZI wa WABUNGE ni CCM, je hapo itakuwaje? Rais kikatiba anachagua watu wake na tuseme wa CHADEMA. CCM wao wanamsubiri bungeni kwenye kuwapigia kura ya hapana au ndiyo PM na mawaziri wake. Hapo inakuwa mtihani wa kwanza.

Wa pili kwenye mawaziri kupitisha mambo bungeni watakuwa na shida sana kwani kila wakati watakuwa na WABUNGE wachache na huku wengi wakiwa chama cha CCM.
Sasa kikatiba hii IKOJE? Au Rais inatakiwa achague PM na Mawaziri kutoka chama kilichoshinda Uchaguzi na kuwa na wabunge wengi? Kwa nini isiwe kwamba chama kilichoshinda uchaguzi wanakuwa wao ndiyo wanaunda SERIKALI na hata kama wamepata asilimia 60 basi wanaungana na chama kingine ili kuwa na asilimia zaidi ya 75? Naomba mwenye kulielewa hili anisaidie.
 
Hii ni moja ya maeneo ambayo huleta ugumu wa kuendesha serikali kwa mfumo wa demokrasia ya kimagharibi. Miswada yote haipiti bila sahii ya rais aliyeko madarakani, hivyo atatumia turufu hii kushindana na bunge. Mfano mzuri ni Marekani ambapo Republicans na Democrats wana uwingi katika nguzo tofauti za uwakilishi yaani House of representatives na Senate. Nchi kama Italia ambako serikali kuanguka kwa kukosa uwingi ni kawaida, uchaguzi kwao ni wakati wowote, na serikali za mseto ni kawaida kwao. Katiba yetu ina upungufu wa kutokuwa wazi kuhusu serikali ya mseto!!
 
Ni kweli hiki ni moja ya vipngele vyenye utata katika katiba. Kinaweka mazingira magumu sana ya utawala.
Lakini viongozi wengi wamekuwa wakitumia njia ya mkato ya kulivunja Bunge yanapotokea mazingira kama hayo. Na kwa kuwa wabunge hawataki kukosa ulaji, huwa wanaangalia maslahi zaidi na kuanza kumpendezesha bwana mkubwa.
na ndio maana inafaa kuiangalia katiba kwa ujumla wake na kuandika mpya inayotufa kwa mazingira ya sasa
 
Ndiyo sababu watu wengi wamelilia mabadiliko makubwa katika katiba yetu ambayo kila siku utasikia bungeni hawa mawazili wetu wa Katiba na sheria wanatoa hoja kwamba hawaoni sababu ya kuibadilish katiba ili hali wanaona jinsi inavyojikanganya yenyewe. Kibaya zaidi wengi wa hawa mawaziri ni wanasheria na wanajua kujikanganya kwa sheria kunavyoleta matatizo katika utawala.

Hivi wameshawahi kufikiria inaweza kuwaje siku Tanzania bara akichaguliwa rais toka ccm na visiwani akichaguliwa cuf? wanaweza kushirikiana vipi kisera? Au tunasubiri migogoro mingine kama hii ya muungano wa kulazimishana unavyoonekana kuwapo leo? Mimi sijawaelewa viongozi wetu wasivyojali mustakabali wa nchi yetu?

Wanafanya nchi hii kama mali ya familia ya mtu furani! Ni ajabu kweli!
 
Hivi wameshawahi kufikiria inaweza kuwaje siku Tanzania bara akichaguliwa rais toka ccm na visiwani akichaguliwa cuf? wanaweza kushirikiana vipi kisera?
Hii ndio scenarioninayoiombea itokee,si kwa sababu siipend nchi yangu, bali ifungue macho ya viongozi/wabunge wetu kuona wapi tunakwenda. Sasa hivi ni tabu rais wa zanzibar kuhudhulia vikao vya baraza la mawaziri mwenyekiti akiwa si rais. Je rais wa Zanzibar chini ya chama cha upinzani ataona sababu yeyot ya maana kuhudhuria vikao hivyo? tutamlaumu akikataa, lakini mazingira ya ushirikiano kwa sasa uanategemea CCM kushinda pand zote, na ndio maana muafaka hautekelezeki na CCM watafanya kila ujuvi ili washinde Zanzibar.

Losing will be too bitter a pill to swallow.
 
Kinadharia hilo ni tatizo lakini wao walipoandika Katiba na kufanyia marekebisho kuna kitu ambacho they never took into account; kwamba Tanzania inaweza kupata chama tawala ambacho si CCM. So, tatizo unalolipata ni la kifikra zaidi kuliko la kitendaji, kwanini hawafikirii anytime soon wapinzani watakuwa in the minority.
 
Kiuhalisia Tanzania ni nchi ya chama kimoja. Chama tawala ndio kimeshika hatamu. Ndicho kinagawa ruzuku. Pia ndicho kinaamua masuala ya mwafaka. Mchezo wa kuigiza wa vyama vingi utakapoisha kikamilifu Afrika ndipo tutaelewa kuwa tulikuwa katika mfumo wa kusadikika. Mchezo huu wa kuigiza tunapigia kura vyama umeshaanza kuisha Kenya na Zimbabwe ambako sasa mambo mseto mseto. Kuna kila dalili kuwa ikifika 2010 utaisha Zanzibar na sitashangaa ukiisha Tanzania mwaka 2015!
 
Back
Top Bottom