Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Wajuzi wa katiba,
Nimejaribu kusoma katiba yetu kama alivyonisema Kuhani na nimefika point moja nimekwama kujua hii ikoje.
Katiba yetu ni RAIS anamteuwa PM na Mawaziri na yeye ndiye BOSS wa serikali hiyo. Hii kwangu haina tatizo kama tu kwa mfano Rais wa CCM na chama kilichoshinda uchaguzi na wako wengi bungeni ni CCM. Sasa ikija tokea tuseme RAIS anatoka CHADEMA au CUF au ..... na chama kilichoshinda UCHAGUZI wa WABUNGE ni CCM, je hapo itakuwaje? Rais kikatiba anachagua watu wake na tuseme wa CHADEMA. CCM wao wanamsubiri bungeni kwenye kuwapigia kura ya hapana au ndiyo PM na mawaziri wake. Hapo inakuwa mtihani wa kwanza. Wa pili kwenye mawaziri kupitisha mambo bungeni watakuwa na shida sana kwani kila wakati watakuwa na WABUNGE wachache na huku wengi wakiwa chama cha CCM.
Sasa kikatiba hii IKOJE? Au Rais inatakiwa achague PM na Mawaziri kutoka chama kilichoshinda Uchaguzi na kuwa na wabunge wengi? Kwa nini isiwe kwamba chama kilichoshinda uchaguzi wanakuwa wao ndiyo wanaunda SERIKALI na hata kama wamepata asilimia 60 basi wanaungana na chama kingine ili kuwa na asilimia zaidi ya 75? Naomba mwenye kulielewa hili anisaidie.

Usikonde Kuhani aliyekucheka mambo haya anayajua sana atakusaidia tu akija hapa.
 
Usikonde Kuhani aliyekucheka mambo haya anayajua sana atakusaidia tu akija hapa.

Augustoons,
Mie sikondi wala sina pressure yoyote. Ila ukweli ni huu, tumekuwa WAKALI kushambulia viongozi wetu kuwa HAWATAKI USHAURI au KUPEWA UKWELI. Mie maneno ya KUHANI nilichukulia kama Challenge ambayo imenifanya sasa mara kwa mara kufungua hiyo katiba na kuisoma. Kama siyo maneno ya KUHANI nafikiri nisingeisoma milele. Hii ni sawa na somo kama la chemistry. Maishani nimekuwa silipendi hili somo, ila lenyewe ndiyo linanipenda sana. Sasa huwa inabidi tu nisome kwa shida shida na nikimaliza huwa nimejifunza mengi na kufurahi kusoma hiyo chemistry. Nafikiri hata wewe ujifunze kuwa ukikosolewa kuwa hujui kitu fulani basi valia njuga hilo swala na usome. Kama viongozi wetu wangelikuwa WAKICHEKWA basi wanabadilika, leo hii tungelikuwa mbali. Ila ndiyo hao akina Mkapa, ukimsema kidogo tu ANAKUWA MKALI KAMA CHILLI.

Nashukuru kwa wote waliochangia ingawa kwa haraka haraka naona hili swala ni TATA hasa kama ambavyo mimi nililiona. Labda nimsubiri kuhani sasa anijibu maana aliniuliza "Kwani katiba inasemaje?" Na mie nimeandika inavyosema tayari ila tu kushindwa kujua huo utata.

Nyerere aliwaambia CCM kuwa ukiona mwenzio anayolewa, wewe tia maji. Kama hawataki kurekebisha haya mambo mapema ilihali tayari Kenya na Zimbabwe yameanza, basi watakuja adhilika siku moja. I hope nao watajifunza kama mimi na kubadili TABIA yao kwa kufanya mambo ambao wanafikiri MILELE hawatafanya. NEVER SAY NEVER!!!!!!
 
Augustoons,
Mie sikondi wala sina pressure yoyote. Ila ukweli ni huu, tumekuwa WAKALI kushambulia viongozi wetu kuwa HAWATAKI USHAURI au KUPEWA UKWELI. Mie maneno ya KUHANI nilichukulia kama Challenge ambayo imenifanya sasa mara kwa mara kufungua hiyo katiba na kuisoma. Kama siyo maneno ya KUHANI nafikiri nisingeisoma milele. Hii ni sawa na somo kama la chemistry. Maishani nimekuwa silipendi hili somo, ila lenyewe ndiyo linanipenda sana. Sasa huwa inabidi tu nisome kwa shida shida na nikimaliza huwa nimejifunza mengi na kufurahi kusoma hiyo chemistry. Nafikiri hata wewe ujifunze kuwa ukikosolewa kuwa hujui kitu fulani basi valia njuga hilo swala na usome. Kama viongozi wetu wangelikuwa WAKICHEKWA basi wanabadilika, leo hii tungelikuwa mbali. Ila ndiyo hao akina Mkapa, ukimsema kidogo tu ANAKUWA MKALI KAMA CHILLI.
Nashukuru kwa wote waliochangia ingawa kwa haraka haraka naona hili swala ni TATA hasa kama ambavyo mimi nililiona. Labda nimsubiri kuhani sasa anijibu maana aliniuliza "Kwani katiba inasemaje?" Na mie nimeandika inavyosema tayari ila tu kushindwa kujua huo utata.
Nyerere aliwaambia CCM kuwa ukiona mwenzio anayolewa, wewe tia maji. Kama hawataki kurekebisha haya mambo mapema ilihali tayari Kenya na Zimbabwe yameanza, basi watakuja adhilika siku moja. I hope nao watajifunza kama mimi na kubadili TABIA yao kwa kufanya mambo ambao wanafikiri MILELE hawatafanya. NEVER SAY NEVER!!!!!!

Sikonge utata uliopo katika katiba yetu hii ya sasa sio huo tu,je umewahi kufikira endapo Rais akachaguliwa kupitia chama fulani mf.CCM afu akiwa madarakani akaona hakifai akakihama kwa kuanzisha kingine?kama alivyofanya bingu wa mutharika?je,katika hilo katiba yetu inasemaje?utakuta ita loophole kubwa tu.

Na ndio maana watu wengi wanasema katiba yetu japokuwa nchi ni ya mfumo wa vyma vingi vipengele vingi vimekuwa premised as if ni ya chama kimoja.Good challenge indeed uliyotoa,we will discuss shortly.Haya ya Wangwe yametusimanzi mno kwa muda mchache tutakuja tu huko.
 
Katiba yetu haikuandikwa na watu waliokuwa wanaona mbele kwa mapana na marefu. Kuhusu muudo wa serikali, wamechukua vipande kutoka Uingereza ambako mawaziri huteuliwa kutokana na wabunge wa chama kilichoshinda, na vipande kutoka Marekani ambapo rais huchaguliwa sawa na wabunge kwa kupigiwa kura na wananchi. Kwa marekani Rais aliyechaguliwa huteua mawaziri wake kutoka popote pale, na wala mawaziri hawawezi kuwa wabunge.

Sasa wakati huko Uingereza kiongozi wa serikali (Waziri Mkuu) anatoka kwenye chama chenye wabunge wengi, kwa marekani kiongozi wa serikali (Rais) siyo lazima atoke kwenye chama chochote. Ndiyo maana Stephen Paul Adams anagombea urais wa marekani kama independent, na akishinda ataunda serikali yake bila kuwa na mbunge hata mmoja.
 
Sikonge utata uliopo katika katiba yetu hii ya sasa sio huo tu,je umewahi kufikira endapo Rais akachaguliwa kupitia chama fulani mf.CCM afu akiwa madarakani akaona hakifai akakihama kwa kuanzisha kingine?kama alivyofanya bingu wa mutharika?je,katika hilo katiba yetu inasemaje?utakuta ita loophole kubwa tu.Na ndio maana watu wengi wanasema katiba yetu japokuwa nchi ni ya mfumo wa vyma vingi vipengele vingi vimekuwa premised as if ni ya chama kimoja.Good challenge indeed uliyotoa,we will discuss shortly.Haya ya Wangwe yametusimanzi mno kwa muda mchache tutakuja tu huko.

Agustoons, nadhani hilo siyo gumu sana kwani standard ni ile ile ya Mbunge; ukiachama chama unapoteza sifa ya kuwa Mbunge; vile vile ukitoka chama unapoteza sifa ya Urais. Ili mtu awe Rais lazima awe amependekezwa na chama cha siasa.
 
Hapa Tanzania ni vigumu kuoanisha tofauti kati ya katiba na sera za chama tawala na hii imekuwa hivyo kwa makusudi kabisa. Mfano moja mzuri ni huu Muungano wetu wa serikali mbili ambao unatatewa sana kwa kutizama sera ya CCM kuliko kikatiba. Raisi wetu anatawala kwa kuzingatia sera na ilani ya uchaguzi ya CCM kuliko matakwa ya katiba.

Mtu akiichambua katiba tuliyo nayo hivi sasa ni kama vile imetungwa kulinda maslahi ya CCM kuliko ya wananchi kwa ujumla wao. Mazingira ya hii katiba hayaoani na mfumo wa vyama vingi na kwa sababu hiyo si rahisi chama chochote cha ushindani kushinda uchaguzi mkuu. Watetezi wa katiba hii wanayo mamlaka ya kukataa mabadiliko ya kweli kwa kuwa hiyo hiyo katiba inawapa fursa ya kufanya hivyo.

Kwa kifupi ukweli ni kuwa nchi inaendeshwa kwa kufuata matakwa ya CCM na si katiba. Kazi kweli kweli.
 
Mpita Njia,

Kipengele gani na kinasemaje?
Mtu aliyeshinda urais kuwa na uhuru wa kuunda serikali yeye mwenyewe.
Hii ina hatari kwa sababu haizingatii kuwa kuna uwezekano wa mshindi huyo kutoka kwenye chama chenye wabunge wachache
 
Agustoons, nadhani hilo siyo gumu sana kwani standard ni ile ile ya Mbunge; ukiachama chama unapoteza sifa ya kuwa Mbunge; vile vile ukitoka chama unapoteza sifa ya Urais. Ili mtu awe Rais lazima awe amependekezwa na chama cha siasa.

Unajua nini mkuu? Kwa wabunge kuna express provision inayosema hivyo na ina imply kwamba mbunge kachaguliwa kwa kura za wanachama wa chama kile anachokiwakilisha.Yaani presumption ni kwamba CHADEMA MEMBERS hawawezi kumpigia kura mgombea wa CCM,lakini kwa Rais hakuna hiyo express provision kama ya Wabunge na ukiangalia hata Mkuu WA KAYA kura zile alizopata sio za CCM peke yake hata baadhi ya wanachama wa upinzani walimpigia sasa,hii sijui inakuwaje,katiba yetu haina tofauti sana na hiyo ya malawi.Hii case iliwasumbua sana na wakashindwa kumng'oa bingu wa mutharika hadi leo.
 
Mtu aliyeshinda urais kuwa na uhuru wa kuunda serikali yeye mwenyewe.
Hii ina hatari kwa sababu haizingatii kuwa kuna uwezekano wa mshindi huyo kutoka kwenye chama chenye wabunge wachache

SORRY hapa nimechanganya. Kumbe inayosema hivyo ni sheria ya uchaguzi na si katiba. SORRY again
 
Kwa maoni yangu nafikiri ni vizuri sana ikatokea hivyo kwamba rais atoke chama chenye wabunge wachache na upinzani ukawa na wabunge wengi hii itasaidia serikali kuto kuburuza mambo itakavyo. Hata nchi kama Marekani inafuata sheria hizo hizo, na serikali iliyopo madarakani lazima ijadiriane na wapinzani wao kwa kila jambo kama wanataka liungwe mkono.
 
Mtu aliyeshinda urais kuwa na uhuru wa kuunda serikali yeye mwenyewe.

Hii ina hatari kwa sababu haizingatii kuwa kuna uwezekano wa mshindi huyo kutoka kwenye chama chenye wabunge wachache

Mpita njia,

Naomba uniambie kipengele hicho unachoona wewe kina hatari kinasemaje.

(It's just a matter of copying the section from a PDF of the Katiba and pasting it here. Thank you.)
 
attachment.php


Wapinzani waibua upya hoja ya mgombea binafsi

2008-08-14 12:34:17
Na Beatrice Bandawe, Dodoma
Kambi ya Upinzani imeibua upya hoja ya kuwepo kwa katiba mpya ya mgombea binafsi wa urais na kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.
Kadhalika, imetaka kuanzishwa Mahakama Maalumu ya Katiba itakayotoa tafsiri na ufafanuzi iwapo Zanzibar ni nchi au sivyo.
Msemaji Mkuu wa Upinzani Bi. Fatma Maghimbi, alitoa hoja hizo wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka huu wa fedha.
Kuhusu katiba mpya Bi. Fatma alisema kambi hiyo katika hotuba ya mwaka jana, iliainisha vipengele 12 vinavyotakiwa kupitiwa ili kupata katiba mpya, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika.
Alisema katiba mpya si ya kambi ya upinzani bali ni kilio cha Watanzania wote.

``Kambi ya upinzani inashauri kuwa suala la kuwa na katiba mpya ni la msingi, haliepukiki kwa sasa na lisifumbiwe macho.
Hivyo Katiba mpya itungwe kwa kuwashirikisha wananchi wote kwa utaratibu utakaoandaliwa na pia kupitia vikundi mbali mbali vya kijamii, vyama vya siasa na viongozi wa dini.
Kuhusu mgombea binafsi wa urais, Bi. Fatma alisema inapaswa aruhusiwe katika ngazi zote za uchaguzi, ikiwemo urais, ubunge na serikali za mitaa.

Alisema haki ya kupiga kura au kupigiwa kura ni ya msingi kikatiba kwa kila Mtanzania. Hivyo kuwalazimisha watu kujiunga na vyama vya siasa ili wawe na haki ya kuchaguliwa itakuwa sawa na kuwanyima haki yao hiyo ya msingi.

``Nchi nyingi duniani na hata za Kiafrika kwa sasa zinaruhusu mgombea binafsi kama Ghana, Namibia na Rwanda,`` alisema.

Suala Mahakama ya Kadhi, alisema kuanzisha mahakama hiyo ni hoja ya msingi na isiyoepukika kwa sasa.

``Ilani ya CCM iliona umuhimu wa mahakama hiyo. Hii ni kwa sababu kutokuwepo kwa mahakama hiyo ni kikwazo katika utatuzi wa masuala ya msingi yanayowahusu Waislam,`` alisema.

Alisema kuna mahakama za biashara, ardhi na kazi, hiyo ya Kadhi itakuwa ni sawa na kuwa na mahakama maalum kama hizo.

Alisema kuna hoja mbalimbali zilizotolewa kupinga kuwepo kwa mahakama ya kadhi, miongoni mwao ni ikiwemo kuanzishwa kwa mahakama hiyo kwa kutumia Sheria ya Bunge itakuwa ni kuvunja au kwenda kinyume na katiba ya nchi.

Alisema raia au wananchi wana dini zao na wanaruhusiwa kuabudu na kufanya mambo yao kwa mujibu wa misingi ya dini zao.

Juu ya kuwepo kwa Mahakama Maalum ya Katiba, alisema upinzani unaona haja ya kuboresha mahakama hiyo ili iwe ya juu katika mfumo wa mahakama nchini ili ishughulikie na kutafsiri mambo ya msingi ya kikatiba yanayohusu taifa.

Alisema kuna mambo ya msingi yanayohitaji mahakama hiyo yakiwemo ya tafsiri ya mambo ya Muungano/Zanzibar ni nchi.

Alisema mwezi uliopita Waziri Mkuu alitamka bungeni kwamba Zanzibar sio nchi, baadaye Bw. Iddi Pandu Hassan, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, aliliambia Baraza la Wawakilishi kuwa Zanzibar ni nchi.

``Je huu sio mgogoro wa kutosha wa kuonyesha haja ya kuwepo Mahakama ya Katiba.

Na hili sio jambo la kusema litatatuliwa na tafsiri ambayo itatolewa kwa mashirikiano ya wanasheria wakuu wawili wa Zanzibar na wa Jamhuri ya Muungano kwa sababu ni mgogoro wa kikatiba,`` alisema.

Alisema pia itashughulikia suala la Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) ambalo liliamuliwa na Mahakama Kuu.

Ilitaka kufutwa adhabu ya kifo kwa kuwa si ya kibinadamu na hakuna uthibitisho kuwa inasaidia kupunguza makosa ya jinai.

``Kwani inaonekana kuwa pamoja na kuwepo kwa adhabu hiyo idadi ya kesi za mauaji hazipungui,`` alihoji
 
Tafadhali ndugu usianze kutuboa tena na kum-name drop Shamhuna kwenye kila posting, sawa?
 
Kwanza, bila kujali vitisho vya Jakaya Kikwete, Baraza la Wawakilishi katika kikao cha mwezi wa kumi walijadili kwa kina suala la Muungano. Spika, Mhe. Pandu Ameir Kificho, aliahidi Oktoba watalijadili. Muungwana hutimiza ahadi.Pili, huu Mkataba wa Muungano, Articles of Union,umegubikwa na mambo mengine sana ambayo hayaeleweki. Sasa tunataka Articles of Union, Mkataba wa Muungano, uwekwe bayana ujadiliwe upya. Na tunataka ujadiliwe vipi? Kwamba sisi Wazanzibari kwa umoja wetu tujadili Mkataba, tukubaliane mambo yapi tunataka yawe kwenye Muungano, tukubaliane Muungano wenyewe uwe na sura gani, tukubaliane Muungano wenyewe uwe na mamlaka gani. Na Watanganyika nao wafanye hivyo hivyo, kama Watanganyika, kwa upande wao.

Hotuba ya kihistoria ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kwa Wazanzibari katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa maalum na wazee wa jimbo la Chaani, Jumamosi 30 Agosti, 2008, Kaskazini Unguja, kutoa msimamo wa hatima ya Zanzibar kwenye Muungano

Maamkizi na Shukrani
Waheshimiwa Wazanzibari wenzangu, nianze kwa kuungana na wenzangu kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Chaani wakiongozwa na wazee ambao wametualika kuja kufanya mkutano huu hapa Chaani. Nasema ahsanteni sana.

Pili, niwashukuru viongozi wa chama chetu cha CUF wa ngazi mbali mbali: wilaya, wodi, jimbo, na matawi, kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu. Nasema ahsanteni sana.
Lakini bila ya kuhudhuriwa na nyiyi tungekuwa hatuna mkutano huu. Pamoja na maandalizi mazuri, kilichofanikisha mkutano huu ni nyinyi muliohudhuria. Kwa hivyo, hakuna budi shukrani nyingi zije kwenu.

Salamu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Baada ya hilo, kama alivyosema Mhe. Salim Bimani (Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Mahusiano ya Umma), baada ya siku mbili tunatazamia tutampokea mgeni Ramadhani. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aijaalie iwe Ramadhani ya kheri kwetu sote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu, kwa barka za mwezi mtukufu wa Ramadhani, matatizo waliyonayo Wazanzibari ayaondoe. Yeye ni Muweza wa yote, yeye ni kusema jambo kuwa linakuwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu, kwa baraka za mwezi Mtukufu wa ramadhani, aulinde umoja wa Wazanzibari ili atupe nguvu kuweza kutetea nchi yetu ya Zanzibar. Tunamuomba Mwenyezi Mungu azitakabalie funga zetu na atusamehe makosa yetu kwa fadhila za mwezi wa Ramadhani.

Waheshimiwa, hali ya maisha ni ngumu na Ramadhani mara nyingi hali huwa ngumu zaidi, kwa hivyo tupeane pole. Inshallah, Mwenyezi Mungu, atatusahilishia. Inshallah. Lakini niiombe Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ioneshe mfano. Ipunguze mzigo wa gharama za maisha kwa Wazanzibari angalau kwa mwezi huu wa Ramadhani. Na kubwa, wakiweza kutupunguzia kodi katika mafuta ya petroli na dizeli na katika baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje katika mwezi huu, hali itakuwa nafuu kidogo. Waekeze na wao kwa Mwenyezi Mungu wakalipwe kesho, Akhera. Lakini pia niwaombe Wazanzibari, sisi kwa sisi, tusaidiane. Tunahimizwa kusaidiana, kupeana sadaka, na hasa katika mwezi huu wa Ramadhani.

Kwa hivyo, kila yule aliyenacho, amsaidie yule asiyenacho. Na hususan wafanyabiashara wasiutumie mwezi wa Ramadhani kuzidi kuwakamua watu ambao hawana kitu. Tunawaomba san asana, waache kuwakamua, na wao vile vile waekeze kwenye akhera zao, wasiangalie kwenye faida za duniani. Tukifanya hivyo, inshallah, ule ukali utaweza kupungua.
Udhaifu wa Hoja za Rais Kikwete na Mjadala wa Hadhi ya Zanzibar
Baada ya salamu hizo za kuikaribisha Ramadhani, sasa naomba muniruhusu kuzungumzia yale ambayo wazee wa Chaani wametualika kuja kuyazungumza hapa.

Waheshimiwa, kama munavyojuwa kwamba katika kipindi cha siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkali katika nchi yetu. Mjadala ambao chanzo chake ulianzia kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano, kule ambako Kiongozi wa Upinzani katika Bunge, Mhe. Hamad Rashid Mohamed, alipomuuliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda: Je Zanzibar ni nchi? Mhe. Pinda akajikaza, akajitutumua, akasema: Zanzibar si nchi! Mjadala ukaanza hapo. Na ulikuwa mjadala mkali.

Hatimaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akatinga Bungeni kwenda kuzungumza na Watanzania kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano. Mimi sikuwepo, lakini waliokuwepo wananiambia kwamba katika hotuba yake alianza na suala hili, kwamba je Zanzibar ni nchi ama si nchi. Na naambiwa: Wewe unamjuwa rafiki yako (Kikwete) anapenda kuchekacheka, lakini alipokuwa kazungumza suala hili hakucheka. Alikuwa kidogo kakasirika hivi!

Ningeelewa pengine ni kwa uzito wa suala lenyewe, akaona haifai kuchekewa. Kwa hivyo, Watanzania, na hususani Wazanzibari wakatazamia watapata majibu ya kuwaridhisha. Basi Mhe. Kikwete akalizungumzia suala hili na mambo mengine mengi, lakini leo ajenda yetu ni hili alilozungumza Kikwete juu ya kwamba Zanzibar ni nchi ama si nchi. Sawa sawa waheshimiwa!?

Udhaifu wa Hoja ya Kwanza: Mshangao wa Kikwete kwa Wanaohoji Muungano
Mheshimiwa Kikwete alisema mengi katika suala hili, lakini mambo matatu ndiyo ya kushika: la kwanza alisema anashangaa kwamba leo ni miaka 44 tangu Muungano huu kuasisiwa na bado kuna watu hawauelewi. Bado watu hawaelewi dhamira za waasisi kuunganisha nchi hizi. Anashangaa.

Mimi namwambia rafiki yangu, kwa heshima zote with due respect hapo Mhe. Kikwete hakutwambia jipya. Nataka nimkumbushe Mhe. Kikwete kwamba mwaka 1967, muasisi mmoja wa Muungano huu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, anasema kwamba yeye hashangazwi na wageni ambao hawauelewi Muungano wa Tanzania, lakini anashangazwa kwamba Wazanzibari na Watanganyika, Watanzania wenyewe, kwamba hawauelewi Muungano huu. Kwa hivyo alilosema Kikwete tarehe 21 Agosti, 2008, kule Bungeni tayari lilishasemwa miaka 41 iliyopita na Mwalimu Julius Kambrage Nyerere.

Mwalimu (Nyerere) alipozungumza ulikuwa Muungano una umri wa miaka mitatu tu, leo Kikwete anazungumza Muungano una miaka 44, na bado Watanzania hawauelewi. Sasa nani wa kulaumiwa? Nani wa kulaumiwa, kwamba miaka 41 imepita, bado wananchi hawaulewi Muungano wao? Huwezi kuwalaumu wananchi. Kama kuna wa kulaumiwa, ni wao watawala.
Nami nasema, ni kweli Muungano huu haueleweki. Utaeleweka vipi, na bado wananchi hawajaelezwa Muungano huu ni vipi? Bado wananchi hawajaelezwa dhamira za Mzee Karume na Mwalimu Nyerere kuunganisha nchi. Kwa kipindi chote cha utawala wa Nyerere ilikuwa wewe unaambiwa ni haini ukizungumzia masuala ya Muungano. Kwa hivyo, Muungano utaeleweka vipi na nyinyi wenye madaraka hamtaki, kwa makusudi kabisa, kuwaeleza wananchi ni nini Muungano huu? Hamtaki. Vipi wataelewa wananchi?
Mambo yenyewe yamefanywa siri siri, yamegubikwagubikwa katika guo jeusi, hujui ndani muna nini mule. Ndio ukweli wenyewe ulivyo hivyo. Lakini tulianza kuanzia mwanzo, Muungano unafanywa kwa siri kubwa.

Mwaka 1964, baada ya Mapinduzi, miezi mitatu tu baada ya hapo, tunaambiwa Mwalimu Nyerere na Mzee Karume wakazungumza, watu wawili. Watu wawili! Waheshimiwa, hata Baraza la Mapinduzi, wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, ambalo wakati huo pia lilikuwa Baraza la Mawaziri la Zanzibar, walikuwa hawajui kitu. Wao tarehe 25/26 Aprili 1964, wanasikia kama sisi wanyonge wengine kwamba nchi mbili zimeungana. Basi hata viongozi wa serikali hawaaminiki? Hata viongozi wa serikali nao hawaaminiki?

Mwanasheria mkuu wa wakati huo, Bwana (Wolfgang) Dourado, kasema wazi wazi, yeye kama ndiye mshauri mkuu wa mambo ya sheria kwa serikali ya Zanzibar, hakuambiwa, hakushirikishwa chochote katika suala hilo. Mwalimu wangu, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, anasema waziwazi kwamba pamoja na kuwa alikuwa karibu na Mzee Karume, hakujua lolote juu ya Muungano huu. Hii ndiyo hali halisi. Tumezungwazugwa na watu wawili tu, basi!

Na yule Nyerere, yeye alikuwa na wanasheria wa Kiingereza wakimshauri, lakini alimkataza Mzee Karume asimtumie mwanasheria wake. Ndiyo suala lenyewe hilo. Mpaka leo unafichwafichwa, hatujui nini Muungano huu! Sawa sawa wananchi!?

Tunaambiwa katika Mkataba wa Muungano, ambao ulitarajiwa ndio uongoze Muungano huu, ilikubaliwa baada ya maraisi wawili kuweka saini zao basi vyombo vya kutunga sheria katika nchi mbili wakati huo Tanganyika walikuwa na Bunge, Zanzibar tulikuwa na Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri kwa pamoja vyombo hivi, kila kimoja kwa upande wake, kiidhinishe Muungano. Lugha ya Kiingereza wanasema to ratify kuidhinisha sawa sawa!?
Mpaka hivi leo, 2008 miaka 44, Mhe. Kikwete kama hujuwi tunakwambia, mpaka leo Baraza la Mapinduzi la Zanzibar halijauidhinisha Muungano huu. Mpaka leo hii. Mpaka leo. Walilofanya wale wa Bara, chini ya Nyerere, kumtaka mwanasheria wa Tanganyika, mzungu mmoja shonga mmoja anaitwa Feefurt, huyu ndiye akaandika sheria yeye ya kuthibitisha Muungano, halafu akaifanya ni sheria iliyotungwa na Baraza la Mapinduzi. Lakini la ajabu, sheria ile haikutangazwa katika Gazeti Rasmi la Serikali ya Zanzibar, ilitangazwa katika Gazeti Rasmi la Tanganyika. Tazama watu walivyo wabaya hawa!

Halafu ukisema, anakwambia sakubimbi, sakubimbi wewe! Tunadai tujuwe mambo, unatwambia sakubimbi. Kama tafsiri yako ya sakubimbi ni watu wasidai haki zao, umechelewa. Yaguju! Tutadai haki yetu. Tutadai haki yetu.
Kwa hivyo, ninalosema kwa ufupi, Zanzibar mpaka leo haujathibitishwa Muungano huu. Mpaka tarehe ya leo, bado.

Makubaliano hayo hayo, au Mkataba wa Muungano, yalitaka katika kipindi cha mwaka mmoja wa kutiwa saini kuweko na Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano. Na katiba hiyo ingelipatikana vipi? Makubaliano hayo yanasema, Rais wa Muungano kwa kushirikiana na Makamo wake kutoka Zanzibar, yaani kiongozi wa Zanzibar, Mzee Karume, wangeunda tume ya kutayarisha rasimu ya katiba hiyo, halafu baada ya hapo, ukaitishwa Mkutano Maalum wa Katiba, Constituent Assembly, (ambao) ni mkutano maalum wa kuipitisha. Hapo tungekuwa na katiba ya kudumu. Mpaka hapo jua lilipofika, hilo halijafanyika wananchi. Miaka 44, hilo halijafanyika.

Walilolifanya ni nini? Ni ule ule usungurasungura tu, basi! Ule usungurasungura aloufanya Nyerere mwaka 1977. Wakati Afro-Shirazi Party na TANU zinaungana, aliteua tume ya kuunganisha vyama hivi na kutayarisha katiba ya chama kipya kitakachokuja. Kamati ile ikiongozwa na mzee wetu, Marehemu Sheikh Thabit Kombo, na upande wa pili, Katibu wa ule, alikuwa ni bwana mmoja ni mwalimu wangu vile vile wa Chuo Kikuu anaiwa Pius Msekwa. Wakakutana, wakatayarisha katiba ya CCM.

Hatuna ugomvi na hapo. (Lakini) walipomaliza, Nyerere akasema kamati hii hii, ndiyo ifanye mapendekezo ya katiba mpya. Halafu akasema Bunge hili hili la Jamhuri ya Muungano ligeuzwe tu, liitwe Bunge la Katiba, lipitishe katiba hiyo. Na mimi nasema, nasimama juu ya hoja kwamba katika hilo Serikali ya Zanzibar haikushirikishwa kabisa. Serikali ya Zanzibar haikushirikishwa. Ulaghai tu, basi! Halafu ati tusiseme. Tutasema. Tutasema.

Lakini kubwa zaidi, waheshimiwa, ni kwamba katika Mambo ya Muungano, Mkataba wa Muungano unasema ni mambo 11 tu, basi. Na mpaka leo, Mkataba ule haujarekebishwa, na ili urekebishe ni lazima upate Zanzibar kwa upande mmoja na Tanganyika kwa upande wa pili wakubaliane kurekebisha. Mpaka leo haujarekebishwa, lakini Mambo ya Muungano yametoka 11 mpaka sasa hivi tunaambiwa ni 23, lakini ukiyachambua moja moja yanafika 32.

Na sasa hivi wana mpango mpya wa kuchukua tu, hupitisha Sheria ya Bunge, kisha wakasema sheria hii itatumika Zanzibar. Kwa hivyo, hata jambo ambalo si la Muungano, sasa wao kwa utaratibu huo wanalifanya la Muungano, (maana) kwa watu wa Tanganyika kuimarisha Muungano maana yake ni kuongeza mambo kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano kuinyima Zanzibar, kuichukulia madaraka yake, na kuyapeleka katika Serikali ya Muungano. Ni ule ule utaratibu wa kijanjajanja kuhakikisha pole pole wanaimungunya Zanzibar mpaka wanaimaliza. Lakini, inshallah, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hawatofanikiwa.

Waheshimiwa, katika njama zao hizo hizo, katika Mabadiliko ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, wakamuondolea Rais wa Zanzibar nafasi yake ya kuwa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kama Mkataba wa Muungano ulivyosema. Tena wakayafanya (mabadiliko haya) kwa njia ambazo ni kinyume na taratibu walizoziweka wenyewe za kubadilisha mambo kama hayo.

Kwa hivyo, musishangae waheshimiwa wananchi, kwamba hata hii kauli ya Mhe. Pinda kwamba Zanzibar si nchi ni katika mtiririko ule ule wa kuhakikisha kuwa wanaimaliza Zanzibar. Kiasi Wazanzibari waje juu.

Kwa hivyo tunalomwambia, kwa hoja ya mwanzo ya Rais Kikwete hajasema jipya. Na pengine hajuwi dhulma iliyofanywa, hajui khiyana iliyoafanywa dhidi ya Zanzibar. bahati njema kuna profesa mmoja anaitwa Issa Shivji. Huyu si Mzanzibari, lakini kafanya utafiti wa kina na kaonesha wazi wazi dhulma ambayo Zanzibar imefanyiwa na katoa kitabu (Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika Zanzibar Union, Mkuki na Nyota Publishers - 2008). Hiki kitabu cha Shivji hiki, kaeleza mambo hayajapata kuelezwa hata siku moja. Profesa mmoja wa Bara alipokisoma kitabu hichi, tena mtu wa Bara huyo, alisema Mzanzibari yeyote akisoma kitabu hiki lazima kwanza akasirike tu kwa vile dhuluma ilivyoelezwa walivyofanyiwa Wazanzibari.

Kwa hivyo tunakwambia Mhe. Kikwete hujatupa jibu. Hilo la kwanza alilolisema.

Udhaifu wa Hoja ya Pili: Kusitisha Mjadala Mara Moja

La pili alilolisema Mhe. Kikwete tarehe 21 Agosti mwaka huu ni kuwa hapakuwa na sababu ya mjadala huu kufikia ulipofikia. Na yeye anashangaa tena yeye kazi yake ni kushangaa tu kwamba viongozi ambao wamo katika kamati zilizoundwa kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano ndio wao kwa wao wanalumbana. Kwa hivyo, akataka hilo lisite mara moja.
Mimi nasema, namwambia rafiki yangu, ndugu yangu Kikwete, kwamba nyinyi mnasema huu ni Muungano wa wananchi, au sio? Munasema si Muungano wa viongozi, ni Muungano wa wananchi. Sasa, kwa nini mukasirike wananchi wakiujadili Muungano wao? Kwa nini mukasirike? Jambo gani linakufanya Mhe. Kikwete na wenzako mukasirike kwa wananchi kuujadili Muungano wao

Mimi nasema wananchi hatuna budi tuujadili Muungano. Miaka mingi walituziba midomo, waliishona midomo: Huna ruhusa kuzungumzia mambo ya Muungano!Sasa mazingira yamebadilika. Na kwa sababu ulikuwa hauzungumzwi, matatizo yamejikusanya, sasa yanahatarisha uhai wa Muungano wenyewe. Watu wanazungumza, mnataka kuwapiga full stop. Hilo haliwezekani, No, kabisa kabisa!

Mimi nasema kuna kila sababu ya kuuzungumza, kuujadili Muungano huu. Tuuelewe, tuufahamu. Kwa kweli, mimi ni mtu ambaye nimefurahi sana, kwamba kwa mara ya mwanzo katika historia tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi (mwaka 1992), wawakilishi na wabunge kutoka Zanzibar, bila ya kujali itikadi zao, wamekuwa na msimamo mmoja juu ya suala la Muungano. Nimefurahi sana, nimefurahi sana, na napaswa kuwa hivyo.
Na hawa, Mhe. Kikwete, ni wawakilishi wa Wazanzibari waliopelekwa katika Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri ya Muungano la Wazanzibari. Wao, kwanza kabisa, wanawajibika kwa Wazanzibari wenyewe, ndio tena wawajibike kwa vyama vyao. Na Wazanzibari wanasema hawaridhiki na Muungano huu. Sasa kwa nini wawakilishi wetu, tuliowapa madaraka watusemee, wakisema muwaone wabaya?

Mimi nawapongeza sana. Nawapa hongera. Hata mawaziri katika Serikali ya Mapinduzi, nao vile vile wamekuja wazi wazi kuwatetea Wazanzibari. Mfano mzuri ni Mhe. Ali Juma Shamhuna. Ali Juma Shamhuna hajapatapo hata siku moja kuipenda CUF, lakini nasema mtu mpe haki yake. Myonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Kwa hili, Ali Juma Shamhuna, Hamza Hassan Juma, Mansour Yussuf Himidi, na wenzao wote, wamesimama upande wa Wazanzibari.

Na mimi, hasa, Mansour kanifurahisha kwa msimamo wake wa kutetea haki ya Zanzibar katika suala zima la mafuta. Sasa wawakilishi hao, na wale wa CUF wakiongozwa na Mhe. Aboubakar Khamis Bakari, akina Said Ali Mbarouk, Bi Zakia na wengine wote. Kwenye Bunge, tuna watu wa CCM, akina Hafidh Ali, wote wameutetea vizuri Muungano wetu. Akina Hamad Rashid, Ali Taarab, wote wameutetea vizuri Muungano wetu. Hatuna budi tuwashukuru, tuwapongeze waendelee na msimamo huo. Msishtushwe, msitishwe na kauli ya Kikwete. Kama nilivyosema, nyinyi mnawajibika kwa Wazanzibari wenyewe sio kwa Kikwete.
Lakini hata lile alilosema Kikwete, kwamba suala hili linajadiliwa katika vikao na watu wanaoshiriki katika vikao hawawajibiki kulizungumza, mimi nasema Kikwete kakosea. Yako mambo yanaweza yakazungumzwa katika vikao hivyo, lakini kuna mambo hayawezi kuzungumzwa katika vikao hivyo.

Vikao vile ni kuondoa tafauti masuala ya utawala juu ya mambo ya Muungano. Lakini mjadala mzima ulivyokwenda, umeonesha kuna mawazo tafauti baina ya Bara na Zanzibar, kwa hivyo hapo kunaashiria kuna mgogoro wa kikatiba. Anayeweza kuutatua mgogoro wa kikatiba si vikao hivi, bali ni Mahkama ya Katiba. Na yeye Kikwete anaogopa kuinda Mahkama ya Katiba. Kwa hivyo undeni Mahkama ya Katiba muzungumzie masuala haya. Kwa hivyo na hili, Mhe. Kikwete hakutupa jibu. Bado hajatupa jibu dhaifu wa Hoja ya Tatu: Zanzibar ni Nchi Ndani ya Jamhuri ya Muungano, lakini si Nchi nje ya Mipaka ya Muungano.

Jambo la tatu alilozungumza Mhe. Kikwete, na naomba hapa mumsikilize vizuri, kwamba anasema dunia nzima inajua kwamba mwaka 1964 Tangayika na Zanzibar ziliungana kufanya jamhuri moja ya Muungano. Akaendelea kusema Kikwete kwamba ukiwa nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano, kuna nchi moja tu ya Tanzania. Kwa maana nyengine, anavyosema Kikwete, ukiwa nje ya Tanzania, Zanzibar si nchi. Unchi wa Zanzibar unaishia Chumbe. Ndivyo anavyosema Kikwete. Na akaendelea kusema, ukiwemo ndani ya nchi, kuna nchi ya Zanzibar na kuna nchi ya Tanganyika, ambazo zote ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano. Kizungumkuti! Ukiwa Uingereza ni Tanzania tu, ukiwa Matemwe, Zanzibar ni nchi. Ukiwa Bukoba, Zanzibar ni nchi na Tanganyika ni nchi. Nasema kizungumkuti.

Mimi nasema kuna moja tu hapa: sikubaliani na uchambuzi wa Kikwete juu ya hilo. Sikubaliani. Suala ninalomuuliza ndugu yangu Kikwete ni kwamba, sisi nchi yetu ya Zanzibar, kwa hivyo unavyotaka weye, tuna serikali yetu, serikali ya nchi yako ya Tanganyika iko wapi?
Waheshimiwa, pale mwanzo Nyerere aliposema wao hawataki serikali, hoja aliyoitumia kutetea kwa nini Tanganyika isiwe na serikali, ni kwamba Zanzibar ni ndogo kieneo na ina wananchi kidogo, kwa hivyo kama hawana serikali yao watakuwa na khofu kwamba wanamezwa. Kwa hivyo, kumbe madhumuni ya kufanya serikali mbili ni kuwafanya Wazanzibari waondoe khofu kwamba watamezwa, lakini Nyerere hajapata kusema kwamba madhumuni ya (Muungano wa) serikali mbili na Zanzibar kuwa serikali yake ni kwamba haki za Zanzibar zilindwe. Hajapata kusema hilo. Kiini macho tu, muoneshwe kuwa nyinyi muna serikali yenu, lakini kumbe ni ganda tupu, hamuna kitu.

Wao waliikataa serikali kwa sababu moja kuu: kuifanya serikali ya Tanganyika iwe ndiyo serikali ya Muungano, kuifanya Tanganyika iwe ndiyo Muungano wenyewe, Jamhuri ya Muungano. Sisi Zanzibar tukae huko, lakini washayachukua madaraka yetu washayachukuwa wao chini ya mwevuli wa Serikali ya Muungano. Hawakupoteza kitu wao. Hakuna walichopoteza. Tuliopoteza ni sisi. Mambo ambayo yalikuwa chini ya mamlaka yetu yamekwenda huko. Kwa maneno mengine, kwa kifichoficho hivi, chini ya pazia ni Muungano, lakini kwa kweli ni Tanganyika.

Kwa hivyo, nasema waheshimiwa, Rais Kikwete anaposema kwamba Tanganyika ni nchi, serikali yake iko wapi? Waruke watoje ni lazima paje kuwa na serikali tatu, msimamo wa CUF.
Sasa tuangalie huu uchambuzi wa Kikwete kwamba ukiwa ndani ya nchi, Zanzibar ni nchi, ukiwa nje Zanzibar si nchi. Nasema hiyo ni kauli ya kisanii. Na nasema hilo kwa sababu Mkataba wa Muungano haujapatapo kuifuta nchi ya Zanzibar wala haukuifuta nchi ya Tanganyika. In fact, Mkataba wa Muungano unaashiria kutaka nchi hizi ziendelee kwa kusema kuwa shughuli za Muungano kwa upande wa Bara zitaongozwa na katiba ya Tanganyika, na shughuli za Muungano kwa Zanzibar zitaongozwa na sheria ya Katiba zilizotungwa na Baraza la Mapinduzi. Sasa unapokuwa na katiba, ambayo sheria ile ndiyo hatimaye ilizaa Katiba ya Zanzibar, katiba ya nini? Ya Yanga? Katiba ya Miembeni? Ile ni katiba ya nchi ya Zanzibar.
Wao katika janja janja zao, siku ya pili baada ya Muungano wakatuga sheria katika Bunge la Tanganyika kuifuta Tanganyika.

Na wameifuta kama nilivyosema ili wao wawe ni Tanzania. Sasa kama wameifuta ni shauri yao. Sisi Zanzibar haikufutwa, na kwa hivyo Zanzibar ipo.
Waheshimiwa, Mkataba wa Muungano umesema kuna mambo yatakayoshughulikiwa chini ya mamlaka chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na katika hayo, hakuna chombo chengine chochote duniani kinachoweza kuingilia Serikali ya Zanzibar. maana yake nini? Katika mambo hayo, kwa lugha ya Kiingereza Zanzibar is sovereign, ina mamlaka ya mwisho hakuna wa kuwaingilia. Mambo ya elimu, mambo ya kilimo, mambo ya afya, mambo ya mawasiliano na uchukuzi, ambayo ndiyo hasa yanayogusa maisha ya mwananchi wa Zanzibar, kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, yako chini ya Serikali ya Zanzibar; na katika hilo hakuna mtu mwengine anayeweza kuwaingilia. Katika mambo hayo, Zanzibar wana haki ya kuzungumza na nchi yoyote nyengine kutaka maendeleo ya Zanzibar.

Hii ni haki yetu, lakini wameibinyabinya. Kukiwa na mkutano wa Shirika la Afya Duniani wanakwenda wao. Haya jamani matatizo ya Zanzibar ya afya kule yatazungumzwa na nani? Kuna Shirika la Kilimo na Chakula duniani, wanakwenda wao. Sasa matatizo ya Zanzibar ya kilimo kule atayazungumza nani kule?

Kwa hivyo nasema we are a sovereign, sisi ni nchi. Mhe. Kikwete with due respectuchambuzi wako hatuukubali.

Hapa nakumbuka mimi nilipokuwemo kwenye serikali, tukizungumza na nchi mbali mbali kuhusu mambo yasiyokuwa ya Muungano na wakitusikiliza. Tulikuwa na mahusiano bila ya kupitia Dar es salaam. Wamefanyafanya mpaka sasa wamewaambia (nchi na jumuiya za kigeni): Hao jamaa (Zanzibar), mpaka mushirikiane na sisi (serikali ya Muungano). No, hiyo ni dhulma munatufanyia wenzetu. Ni dhulma.

Lakini zuri zaidi ni kuwa katika Makubaliano ya Muungano, jambo lililowekwa kama jambo la Muungano ni Mambo ya Nje (foreign affairs) mahusiano ya nchi na nchi nyengine ya kisiasa, ya kiserikali lakini suala la mashirikiano ya kimataifa (international cooperation) halijapata kuwa la Muungano hata siku moja. Wao katika ujanja wao, wamefanya na kuuita Wizara Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ili kuinyima Zanzibar haki ya kushirikiana na mashirika mbali mbali kwa maendeleo ya Zanzibar.
Kwa hivyo, mimi nasema, kwa sababu tuna haki ya mashirikiano ya kimataifa chini ya serikali ya Zanzibar, Zanzibar ilikuwa na haki na Zanzibar itaendelea kuwa na haki ya kuwa mwanachama wa OIC. Ile kulazimishwa kujitoa ni kwa sababu ya choyo chao tu, lakini haki ile tunayo. Na mashirika mengine kama hayo, Zanzibar inayo haki hiyo.
Nani Mwenye Ajenda ya Siri?

Sasa, nimwambie Mhe. Kikwete kwamba sisi hatuna ajenda ya siri, kama kuna mtu ana ajenda ya siri ni wao, sio sisi. Nimeonesha usiri wa Muungano huu ulivyokuwa, nimeonesha hata ule Mkataba wa Muungano ulivyokiukwa kabisa. Sasa yote hayo yanaashiria kuwa wenzetu wana ajenda ya siri. Lakini sisi hatuna ajenda ya siri.

Na kuthibitisha kuwa wenzetu wana ajenda ya siri, mutakumbuka wananchi, baada ya Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislam Duniani (OIC), Bara kulizuka kundi linaloitwa G55, yaani kundi la watu 55, wabunge wa Bara, wakadai serikali yao ya Tanganyika. Wakaenda kwenye Bunge na Bunge likapitisha azimio kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Agosti 1993, serikali ya Tanganyika iwe tayari imeanzishwa. Nyerere hakufurahishwa na azimio hilo halali la Bunge. Akaweka shinikizo kubwa, ikambidi Mzee Ali Hassan Mwinyi aitishe kikao cha wabunge wote wa CCM wa wakati huo kuingalia tena hoja hii. Mwisho wakaambiwa kuwa serkali tatu si sera ya CCM, wakatakiwa warudi Bungeni wakalifute azimio la 1993, wapitishe azimio jipya.

Hiyo ilikuwa ni Agosti 1994, ambapo tunangojea serikali ya Tanganyika. Haikuundwa. Kilichofanyika ni wabunge, ambao wakati huo wote walikuwa wa CCM, walikwenda kwenye Bunge wakalifuta Azimio la Kuanzishwa Serikali ya Tanganyika na badala yake wakasema katika Azimio jipya la Bunge kwamba: Lengo letu ni kuwa serikali mbili kuelekea serikali moja. Sasa ukishakuwa na serikali moja, kuna Zanzibar hapo. Kwa hivyo, nia ya kuifuta Zanzibar ipo. Wao, wenzetu, ndio wenye nia hiyo.

Na kama mmefuatilia mjadala katika Bunge, hasa walipokuwa wanajadili Wizara ya Muungano, bila ya shaka mumeona, kila mbunge wa Bara aliyekuwa akisimama anasema serikali moja. Kila mbunge wa Bara aliyekuwa akisimama, anasema serikali ya Zanzibar lazima ifutwe. Hata watu kufika pahala wakasema kwamba Waziri Mkuu yuko juu wa mawaziri wote wa Zanzibar akiwemo hata Waziri Kiongozi. Matusi ya hali ya juu!

Kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano, serikali hizi mbili ziko sawa sawa. Hakuna serikali moja iliyo juu ya nyengine. Kwa hivyo Waziri Mkuu Pinda hawezi kuwa juu ya Waziri Kiongozi Shamsi Nahodha. Isipokuwa ikiwa mwenyewe Nahodha kakubali akaliwe, shauri yake! Akikubali mwenyewe, shauri yake, lakini tunavyojuwa sisi Pindaet paar na Nahodha. Waziri wa Kilimo wa Bara ni sawa sawa na Burhani Saadat wa Zanzibar. Mwenyewe Mzee Burhani akikubali: Haya bwana, inshallah bwana! hiari yake mwenyewe, lakini constitutional arrangement iko hivyo.

Wala si kweli kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano iko juu ya Katiba ya Zanzibar. No, no, no, ni sawa sawa kabisa. Mwakyembe anafika hadi leo kusema kwamba mawaziri wa Zanzibar hawana nidhamu wanapingana na Waziri Mkuu Pinda! Ebo! Kwani ni Mungu yule hata asipingwe? Hata kama ni serikali moja, wanayo haki, sikwambii kama ni serikali tafauti.
Msimamo wa CUF: Hakuna Usakubimbi, Hakuna Vitisho, Wazanzibari Mkataba wa Muungano Ujadiliwe Upya

Sasa, tunasema waheshimiwa, Zanzibar ni nchi ndani ya mipaka ya Zanzibar, Zanzibar ni nchi nje ya mipaka ya Zanzibar.

Nimwambie rafiki yangu Kikwete, katika hotuba yake kanivunja moyo aliposema wanaozungumza suala hili na masakubimbi. Sikumtazamia hata kidogo. (Lakini) sasa tunasema Wazanzibari tunalotaka ni mambo yafuatayo:
Kwanza, bila kujali vitisho vya Jakaya Kikwete, Baraza la Wawakilishi katika kikao cha mwezi wa kumi walijadili kwa kina suala la Muungano. Spika, Mhe. Pandu Ameir Kificho, aliahidi Oktoba watalijadili. Muungwana hutimiza ahadi. Kwa hivyo, Mhe. Kificho tunakuomba waruhusu wawakilishi walijadili hili. Isijekuwa hotuba ya Kikwete, ukasema lakini Rais kasema. Rais kasema sawa, si ndio tushamsikia? Kwa hivyo, lijadiliwe.
Na kama Kificho hataki, kiongozi mkuu wa kisiasa katika CCM Zanzibar ni Mhe. Amani Karume. Mhe. Karume amdhibiti Kificho, amuamuru Kificho, suala hili lizungumzwe katika Baraza la Wawakilishi.

Wajumbe wetu wakizungumza wazungumze nini? Kwanza wadai kwamba Mkataba wa Muungano uheshimiwe kama ulivyosainiwa na Mwalimu Nyerere na Mzee Karume. Kwa maana hiyo, Mambo ya Muungano 11 tu, yale mengine yote yaliyoongezwa juu mpaka kufika 40 yatolewe yarudishwe kwenye Mamlaka ya Zanzibar.

Na hata hayo mambo 11 yanajadilika. Mimi nakumbuka, katika Kamati Kuu moja, Mwalimu Nyerere, akiwa mwenyekiti wa kikao, alisema wazi wazi mambo kama ya polisi si lazima yawe ya Muungano. Nchi mbali mbali zilizo kwenye Muungano, kila state inakuwa na polisi yake. Kwa hivyo, mambo hayo yaangaliwe na yajadiliwe.

Pili, huu Mkataba wa Muungano, Articles of Union, umegubikwa na mambo mengine sana ambayo hayaeleweki. Sasa tunataka Articles of Union, Mkataba wa Muungano, uwekwe bayana ujadiliwe upya. Na tunataka ujadiliwe vipi? Kwamba sisi Wazanzibari kwa umoja wetu tujadili Mkataba, tukubaliane mambo yapi tunataka yawe kwenye Muungano, tukubaliane Muungano wenyewe uwe na sura gani, tukubaliane Muungano wenyewe uwe na mamlaka gani. Na Watanganyika nao wafanye hivyo hivyo, kama Watanganyika, kwa upande wao.
Tukishakubaliana Wazanzibari, tutakuwa na Waraka wetu wa tunayoyataka. Na Watanganyika watakuwa na Waraka wao. Sasa Wazanzibari na Watanganyik wanateua Tume ya kwenda kukaa juu ya meza kujadiliana mpaka waafikiane. Sio waseme kwamba vikao hivi vya mawaziri ndio vijadili. No, no, no.

Tunajadili nini? Katika hali ya sasa, fikra na mawazo ya watu wa Bara kwamba Serikali ya Zanzibar iko chini yao, Waziri Kiongozi yuko chini yao, sasa unapokwenda kumpeleka Waziri Kiongozi ambaye unaamini huyu yuko chini yangu, unampeleka na Waziri Mkuu aliye juu ya Waziri Kiongozi, pana mazungumzo hapo? Si Hewallah Bwana!?

Tunataka tupate watu competent, wenye uwezo, kwa sehemu zote mbili. Wakishajadili na kukubaliana, sasa iundwe tume yenye wajumbe sawa sawa kutoka Tangayika na kutoka Zanzibar kuandika rasimu ya Katiba mpya ya Muungano.

Mwisho unaitishwa Mkutano Maalum wa Katiba, sio Bunge liliopo ulibadilishe kuwa Bunge la Katiba, hapana. Unaitisha wajumbe hasa waliochaguliwa na Wazanzibari na Watanganyika kwa madhumuni hayo ili wakatunge Katiba.

Hayo ndiyo matakwa ya Wazanzibari, na mimi nayazungumza kwa niaba yenu Wazanzibari.
Hayo ndiyo matakwa yetu, Mhe. Kikwete. Nyinyi mna tabia ya kutupuuza, Wazanzibari. Tangu wakati wa Maalim Aboud Jumbe, serikali iliandika mapendekezo kadhaa wa kadha kupeleka juu ya kuboresha Muungano, yakatiwa chini ya carpet. Wakati wa Dk. Salmin Amour, waliandika mapendekezo mbalimbali yakatiwa kwenyedustbin. Nina hakika chini ya Karume, nao wameandika hivyo hivyo. Lakini wenzetu wa Bara, mapendekezo kutoka Zanzibar hawayataki.

Na sisi wakati umefika kushikilia. Na kwa sababu sasa tumeungana, tumeshikamana, tudai. Nimwambie Kikwete aache tabia yake ya kutisha. Wakati wa kutisha umekwisha. Wakati wa kuburuzana umekwisha, hakuna anayeogopa tena. Tunalotaka ni haki itendeke.
Sasa kwa ufupi, naomba waandishi wa habari wanisikilize vizuri nitakayoyasema sasa hivi. Wanisikilize vizuri na waripoti kama nitakavyosema, na mimi nasema hivi: Muungano kama ulivyo sasa, narudia, Muungano kama ulivyo sasa, Wazanzibari hatuutaki. Haina maana kwamba hatutaki Muungano, lakini hatutaki Muungano kama ulivyo sasa. Mzee Karume alisema kwamba Muungano ni koti, likikubana unalivua. Na sisi Muungano huu wa sasa koti linatubana sana, kiasi ya kwamba ni sawa kuchukua koti la Mhe. Jussa umvishe Hamad Masoud. Litamtosha?

Tunataka sasa tushone koti jipya kwa mazingira ya karne ya 21.
Hakii.
 
Zanzibar kuitikisa NEC

na Mwandishi Wetu


WAKATI kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), kinatarajiwa kuanza keshokutwa, wajumbe wa kikao hicho kutoka visiwani Zanzibar, wamejipanga kuikabili hoja ya hadhi ya Zanzibar, kwa madai ya kutoridhishwa na majibu ya ufafanuzi yaliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete, alipolihutubia Bunge, mjini Dodoma.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa hoja ya hadhi ya Zanzubar kutinga ndani ya NEC, tangu mjadala huo ulipoanzishwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadaye kuibua mjadala mzito ndani ya Bunge, Baraza la Wawakilishi na makundi mengine ya kijamii.

Wajumbe hao kutoka Zanzibar, wamekamia kuikabili hoja hiyo kwani ni moja ya ajenda zitakazojadiliwa na kikao hicho cha kawaida cha NEC, kinachotarajia kufanyika kuanzia Septemba 9 hadi 10 mjini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.

Tayari hoja hiyo ilishajadiliwa kwa kina katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kilichofanyika bila kumalizika jijini Dar es Salaam ambacho kitaendelea tena mjini Dodoma kesho, siku moja kabla ya kikao cha NEC kuanza.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka Zanzibar na Dodoma, vinasema baadhi ya wajumbe wa NEC kutoka visiwani humo, wamekuwa katika mijadala ya faradha na kupeana misimamo wakati wa kujadili ajenda hiyo.

Habari hizo zinasema wajumbe hao ambao msimamo wao unasema Zanzibar ni nchi ndani na nje ya Muungano, wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya makada maarufu wa CCM, wazee maarufu, wafanyabiashara wenye ushawishi wa siasa za Zanzibar bila kujali itikadi zao, kupeana misimamo juu suala hilo.

“Tumefurahi sana kusikia hoja hiyo ilijadiliwa kwa kirefu na CC na sisi tunaisubiri kwa hamu. Hii ni mara yetu ya kwanza kuijadili hoja hiyo ndani ya vikao nyeti vya chama, kwani iliibuliwa bungeni, ikajadiliwa sana ndani ya Baraza la Wawakilishi na sasa inakuja NEC, tunataka mwenyekiti atupe ufafanuzi zaidi,” alisema mmoja wa wajumbe kutoka Zanzibar.

Mjumbe huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema kauli ya Rais Kikwete bungeni kuhusu hadhi ya Zanzibar, imewachanganya zaidi wananchi wa visiwa hivyo na kusisitiza kuwa wanataka kupata ufafanuzi mzuri ndani ya NEC.

Baada ya Rais Kikwete kutoa ufafanuzi bungeni kuhusu hadhi ya Zanzibar, wananchi wa visiwa hivyo waligawanyika huku baadhi yao wakiandaa maandamano ya kumuunga mkono, wengine wakimpinga.

Kama hiyo yaitoshi, baadhi yao waliamua kusambaza vikaratasi vya uchochezi kupinga kauli ya Rais Kikwete na kusisitiza kuwa Zanzibar ni nchi.

Rais Kikwete ambaye alikuwa akilihutubia Bunge kwa mara ya pili na kulifanya suala la hadhi ya Zanzibar kuwa la kwanza katika hotuba yake ndefu iliyochukua zaidi ya saa mbili, alisema mwaka 1964 nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaa nchi moja ambayo ni Tanzania.

Alisema muungano huo ambao ulifikiwa kwa hiari na waasisi wa taifa hili, ulisababisha kuzaliwa kwa mamlaka moja ya Tanzania ambayo katika medani ya kimataifa ndiyo inayotambuliwa rasmi kuwa ndiyo nchi.

Hata hivyo alisema hali hiyo haiwezi kuacha kando ukweli kwamba, katika mazingira ya ndani ya nchi, bado kuna nchi ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania na Tanganyika, ambayo pia ni sehemu ya Tanzania.

Mbali ya kutoa ufafanuzi huo, Kikwete alisema, tofauti za kimtazamo kuhusu muungano bado haziwezi kutoa fursa kwa watu aliowaita ‘machakubimbi’ kuuona umoja na mshikamano walionao Watanzania kuwa ni maambo yanayoanza kutetereka au kuyumba.

Alisema ana imani kubwa kwamba, malumbano yanayoendelea hivi sasa ni wimbi la kawaida na kama yalivyopata kupita mawimbi mengine makubwa kuliko hili la sasa nalo litapita huku likiiacha Tanzania ikiendelea kubakia imara zaidi.

Hata hivyo, aliwatahadharisha viongozi kutulia na kuviacha vyombo vilivyo na mamlaka ya kushughulikia masuala ya muungano kufanya kazi yake ili kuliepusha taifa na hatari ya kuwakoroga na kuwagawa zaidi wananchi.

Mbali ya hoja ya hadhi ya Zanzibar, ajenda nyingine zinazotarajiwa kuwasha moto mkali wakati wa kikao hicho cha NEC ni suala utata la mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM). Suala hilo liliibuliwa na Nape Nnauye, aliyekuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo ambaye jana alivuliwa uanachama wa UVCCM.

Habari zaidi zinasema kuwa huenda NEC ikaacha kujadili majina ya wanaowania uongozi ndani ya jumuiya zake ambazo ni UVCCM, UWT na Wazee. Hali hii imetokana na jumuiya nyingine, mbali ya UVCCM, kutofanya vikao vya mabaraza ya jumuiya hizo kupitisha majina wagombea wao.

‘Ukiacha UVCCM ambao baraza lao lilikutana leo (jana), UWT na Wazee, hawajafanya vikao vya mabaraza, hivyo CC na NEC haziwezi kupitia majina yao na uwezekano wa kuitisha CC na NEC ya dharura kwa ajili ya kupitia majina ya wagombea wa jumuiya hizo, ni mkubwa,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Wanaowania nafasi ya mwenyekiti wa UWT ambayo kwa sasa inashikiliwa na Anna Abdallah, ni pamoja na Janeth Kahama, Sophia Simba, Joyce Masunga, Halima Mamuya, Odina Lujaji na Zerulia Maneno.

Wanaowania nafasi ya mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ni pamoja na Nimrod Mkono, Esther Nyawazwa na John Shibuda.

Wengine ni Balozi Athuman Mhina, Andrew Masanje, Ruben Swai, Abdallah Bulembo, Joseph Yaredi, Ismail Aden Rage, Dk. Muzamil Kalokola, Julius Rwabutamize, Rebecca Mwangwasha, Richard Lukambula, Kuwayawaya S. Kuwayawaya na Estory Kasika.

Nafasi ya makamu mwenyekiti wa Wazazi, inawaniwa na Ameir Makunge, Haidary Abdallah, Dogo Mbaruku, Juma N’hunga, Omar Ameir, Ramadhani Suleiman Nzori, Suleiman Suleiman, Hamis Dadi pamoja na Abdallah Ameir.

Kwa upande wa UVCCM, mbali na Nape ambaye jana ameondolewa katika kinyang’anyiro hicho, waombaji wengine katika uchaguzi huo unaoendelea kuvuta hisa za watu kila kukicha ni Benno Malisa Zainab Kawawa, Mohammed Bashe, Said Mtanda, Suleiman Muhsein, Jerry Slaa, Hamad Masauni, Issa Haji Ussi, Anthony Mtaka, Haule Pangisa, Samuel Marero, Stephen Deya, Geofrey Mwankenja, David Manoti, Mussa Mnyeti, Edson Lubua, Mwamini Lusingu, Asmah Kalokola, Marco Zablon Allute, Harold Adamson, Adila Hilal Vuai, Ashura Ismail, Rashid Masalaka na Raha Ahamada.

Wanaowania uteuzi wa nafasi ya makamu mwenyekiti ni Happy Mahava, Raha Ahamada Ally, Riziki Pembe Juma, Michael Bundala, Rabia Hamid Shaka, Nuru Mohammed Ahamed na Twaha Ally Muhaji.
 
Tanzania tuna tatizo kuwa la kupungukiwa ma ari ya uwajibikaji na uaminifu kazini. Nina hakika kwa bunge letu tena hata kama mkataba ungekuwa na mapungufu mengi ungeweza kupitishwa tu ukizingatia wengi ni wana ccm. Kujadili bungeni labda kungesaidia isiwe siri tena lakini sio kukwamisha mkataba. Kitu muhimu ni kwa viongozi wetu kuwa na mioyo yakizarendo hasa na dhamira ya kweli ktk kuwatumikia watu. Kama viongozi wengekuwa hivyo hata mkataba ukiishia wizarani kusingekuwa na mashaka kwa sababu tunaiamini serikali yetu. I wish to replace the officials with robots.... !!!!

UWAUWUKA ni ugonjwa mbaya sana uliowaathiri watanzania wengi hasa watumishi wa umma.
 
SWALI: Kwa nini serikali haitaki mikataba ijadiriwe bungeni?

JIBU: Kazi ya bunge sio ku-run day to day activities za kuendesha serikali. kazi ya bunge ni kutunga sheria, ambazo zitasababisha serikali ifanye kazi yake ndani ya sheria hizo... wajibu wa Bunge utakuwa kuikosoa serikali au hata kuiondoa madarakani isipofuata sheria zilizotungwa na bunge...

Serikali inaweza kuwa inalega lega kwa kuwa sheria za bunge haziko timilifu kwenye mambo ya mikataba na kadhalika... sio busara bunge kujadili kazi ya mikataba... bali bunge liweke legal frame work nzuri ya kusababisha mikataba iwe na maslahi na taifa na pale ikiwa tofauti kuwe na adhabu kwa watu, taasisi itakayo kiuka... miiko.

Mwisho ni vizuri kila mhimili dola waukafanya kazi yake kulingana na katiba ya nchi... kuliko kutaka Bunge lifanye kazi za serikali... na Serikali ipende kuingilia kazi za mahakama ... itakuwa makasheshe matupu.
 
Back
Top Bottom