Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Julian, Kuna serikali mbili katika Tanzania. Kuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Serikali hiyo basi ina mihimili mitatu.

a. Utendaji - Urais
b. Utungaji Sheria - Bunge
c. Uamuzi wa sheria na kugawa haki - Mahakama

Vyombo hivyo vitatu ni sehemu ya serikali moja. Hivyo Rais (Utendaji) hawawezi kudai wao "Ndio" serikali! wao ni sehemu ya serikali na hivyo vinginve vivyo hivyo.

Tatizo tulilonalo sana ni kuwa Wabunge hawafikiri kuwa wao nao ni sehemu ya serikali. Ingawa vyombo hivyo vitatu viko huru hata hivyo haina maana uhuru huo unavifanya viwe peke. Ni kwa sababu hiyo basi kwa mujibu wa sheria vyombo hivyo vinasimamiana. Rais anateua majaji, majaji wanamwapisha Rais, Rais ana uwezo wa kuvunja Bunge, Bunge lina uwezo wa kumwondoa Rais, majaji, n.k n.k
 
MNKJJ

katika katiba yetu vitu gani vimetajwa Uraisi au Serikali.

na Raisi na balaza lake la mawaziri wanaunda Uraisi au Serikali.

na je Serikali iliyotajwa katika katiba inajumuisha Mahakama na Bunge

naomba ufafanuzi na pengine kama ungenitafsiria kwa kingereza Uraisi na Serikali
 
Julian, umeibua jambo moja muhimu sana katika mjadala huu... inawezekana kabisa mimi, mwalimu Augustine na Reverend Kishoka tumepotoka mahali fulani.. ngoja nicheki cheki Katiba kidogo...
 
Dola ya nchi imeshikwa na mihimili mitatu.
1. Utendaji
2.Bunge (Utungaji wa sheria)
3.Mahakama.

Mara nyingi tunachanganya neno Dola na Serikali. Kimsingi, serikali ni vitu vyote hivyo na sio tawi la utendaji peke yake. Lakini nadhani katika hili kiswahili hakikuwa na misamiati ya kutosha katika kulisema tawi la utendaji. Hivyo Utendaji umekuwa synonimous na Serikali. Lakini kimsingi Dola ndio yenye mihimili mitatu (yaani kwa lugha ya kigeni State pillars are executive, Legilasture and Judiciary. Combined these are called Government). Unaweze kuwa na serikali bila ya Dola, kama Zanzibar. Na hapa ndio confusion inakuja, je baraza la wawakilishi na mahakama ya Zanzibar ni mihimili ya nini? Dola au SMZ? Pia katika Halmashauri nako hakuna dola bali tawi la utendaji na kutunga sheria, yaani baraza la madiwani.

Kwa mchanganyiko huu, basi executive ni serikali na hivyo Bunge sio sehemu ya serikali. Lakini kinadharia Bunge ni sehemu ya Serikali.
Hako ndio kaCivics kangu kadogo
 
Julian, Kuna serikali mbili katika Tanzania. Kuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Serikali hiyo basi ina mihimili mitatu.

a. Utendaji - Urais
b. Utungaji Sheria - Bunge
c. Uamuzi wa sheria na kugawa haki - Mahakama

Vyombo hivyo vitatu ni sehemu ya serikali moja. Hivyo Rais (Utendaji) hawawezi kudai wao "Ndio" serikali! wao ni sehemu ya serikali na hivyo vinginve vivyo hivyo.

Tatizo tulilonalo sana ni kuwa Wabunge hawafikiri kuwa wao nao ni sehemu ya serikali. Ingawa vyombo hivyo vitatu viko huru hata hivyo haina maana uhuru huo unavifanya viwe peke. Ni kwa sababu hiyo basi kwa mujibu wa sheria vyombo hivyo vinasimamiana. Rais anateua majaji, majaji wanamwapisha Rais, Rais ana uwezo wa kuvunja Bunge, Bunge lina uwezo wa kumwondoa Rais, majaji, n.k n.k


Mwanakijiji,
Ukiisoma vizuri katiba yetu utakuta kuwa Rais ndio Dola. Utendaji ni Waziri Mkuu, kutunga sheria Spika na kutafsiri sheria Jaji Mkuu. Katiba yetu imewekwa katika hali ambayo Waziri Mkuu ndio Mkuu wa Tawi la Utendaji ingawa bado KATIBA imempa mamlaka makubwa mkuu wa Dola katika utendaji. Ukisoma vizuri katiba utaona kuwa mwenye kuunda serikali ni PM na ndio maana akiondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani, basi baraza zima la mawaziri huvunjika......

Nadhani kuna haja ya kufanyia kazi zaidi katiba yetu ili hii nafasi ya PM iwe zaidi. Rais kama Mkuu wa Dola, kinadharia haifai pia awe mkuu wa Utendaji. Tanzania Rais na PM wanashare hii executive part. Unajua Tanzania pia Rais ni sehemu ya Bunge? Hivo anashare legislative work. Uganda Rais akikataa kusaini muswada kuwa sheria, Bunge lina go ahead. Tanzania Rais anavunja Bunge baada ya Rais kukataa muswada mara ya tatu.

Mjadala mzuri huu na unatuma muda wa kusoma civics kidogo. Ngoja nami nikachimbe zaidi
 
Zitto, ndio nilikuwa napitia tena Katiba.. na ndio maana nikajikuta nimepatwa na kigugumizi cha ghafla.. inawezekana kabisa Kayombo alikuwa sawa!! that is the scary thought! kuna tatizo kubwa kweli...
 
An electronic copy of the Constitution of the United Republic of Tanzania (1998) is available on the national website:

The Tanzania National Website

The constitution declares that for us, Parliament is President + National Assembly. It identifies the Executive Branch and the Legislative Branches of government:

Section 62 (1) Sates:
“There shall be a Parliament of the United Republic of Tanzania which shall consist of two parts that is to say, the President and the National assembly”
But there were many lapses of memory in the minds of those who framed the document. Section 62 (3) states:

“Whenever any matter requires to be decided or done by both parts of Parliament in accordance with the provisions of this Constitution, or any other law, then the matter shall not be deemed to have been decided or done unless it is decided or done by members of Parliament and also by the President in accordance with their respective authority in relation to the matter”
As the President is the first part of our Parliament, the framers should have said National Assembly instead of Parliament in their second use of the word in this clause.

Getting closer to where we want to go, we read in Section 63 (3) that ;
“For the purpose of discharging its functions, the National Assembly may……. (c) deliberate upon and authorize any long or short term plan which is intended to be implemented in the United republic and enact a law to regulate the implementation of the plan”
Note carefully that this clause says the “National Assembly” and not Parliament. The national Assembly means our MPs, when gathered in session. The Constitution requires that these blokes deliberate upon, and authorize long and short term plans (such as national investment agreements,) that are intended to be implemented in Tanzania.

Subsection (e) of this same Section 63, states that the National Assembly shall:
“deliberate upon and ratify all treaties and agreements to which the United Republic is party and the provision of which require ratification”
It is thus crystal clear from the Constitution of the United Republic that the National Assembly is not only empowered but required to deliberate and vet all major agreements that are entered to between the United Republic and others.

Augustine Moshi
 
Kwa kifupi, Mwalimu Moshi, kama nimekielewa hicho kimombo ni kwamba bunge lina haki ya ku VET all major agreements that are entered to bet. UR and others. Bunge linayo haki ya kupitia na kuidhinisha mikataba. Au siyo?
 
Nimeandika makala ndefu kidogo (itatoka kesho) kuelezea jambo hili kwa mantiki. Tatizo moja tulilonalo ni wabunge kutokujua uwezo wao huu.
 
Jasusi,

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri yetu, Bunge sio kwamba lina haki ya kupitia na kukubali au kukataa mikataba tu, bali lina wajibu wa kufanya hivyo
 
lakini pamoja na kuwa bunge linauwezo huo,bado tunarudi palepale mwenye kutaka nini kijadiliwe bungeni ni spika, tena wa ccm bila kusahau kiongozi wa shughuli za bunge ni pm na ndiye anayewadhibiti wabunge wote wa chama chake ccm.kwa hiyo uwezo wa bunge kama bunge unaishia kwa hao watu wawili tu.sheria zetu zinagongana kila mahali na kutumika kwa maslahi ya watawala.
 
Katibu Tarafa,
Inabidi wabunge wetu wawe wajasiri na watundu. Wasikubali kuendeshwa kimzobamzoba na waziri mkuu au spika. Watumie madaraka yao waliyopewa kikatiba.
 
Ibara 63(2) Katiba inasema hivi:

Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha
Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa
niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri
ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa
majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.


Madai ya kuwa kile ambacho wabunge wanachoweza kufanza zaidi ni "kuishauri" serikali ni uongo wa mchana. Bunge lina jukumu la kusimamia serikali.

Na katika kufanya hivyo kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (e) cha Ibara hiyo Bunge linaweza:

"kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri
ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji
kuridhiwa."

Sasa mikataba ya serikali ni ipi basi? Kwa kutumia mwanga wa Ibara ya 67(8)

Mikataba ya Serikali ni "mapatano yoyote ya
mkataba ambayo mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali ya
Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Idara
yoyote ya Serikali hiyo au mtumishi yeyote wa Serikali aliyeshiriki
kwa niaba ya Serikali."

Sasa, Wabunge wasitishwe na maneno matupu watumie uwezo wao wa kutunga sheria na kulazimisha mikataba mikubwa iangaliwe na wawakilishi wa watu siyo kuitolea mamuzi

Mzee Mwanakijiji, Heshima yako ndugu yangu,

Duhu! Huu ni Msumari kwelikweli. Naona umegonga mfupa haswa!
Hata hivyo, katiba ya nchi yetu imejaa viraka, yaani, baadhi ya vifungu vimebadilishwa mara kwa mara na vingine kuchomekwa kiholela ndani ya katiba. Baadhi ya viraka vimajaa mizengwe, vinakanganya, na kufanya msomaji avurugikwe kimawazo. Si haba kukuta kifungu fulani katika ibara moja kinaifanya ibara nyingine ionekane ni mapambo kwa kuikosesha maana nzima ya kuwemo ndani ya katiba.

Katiba, Serikali na Bunge

Ni kweli, ibara ya 63(2) kifungu kidogo (e) inalipa bunge mamlaka ya kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu jamuhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa. Kumbuka, wanaotaka kuiona hiyo mikataba ni wabunge wa kawaida ambao hawana kofia mbili za Uwaziri na Ubunge. Mawaziri ambao pia ni Wabunge, ndio walioiridhia hii mikataba, na ndio wanaokwamisha hili zoezi. Je, Mbunge asiye na kofia mbili aliyekataliwa kuiona hiyo mikataba na Mheshimiwa Waziri Gaudence Kayombo, afanye nini?

Binafsi, nadhani anaweza kuipeleka Serikali Mahakamani kwa mgongo wa ibara ya 30 (3) inayompa mtu uwezo wa kufungua shauri Mahakamani. Ama, anaweza kuwashawishi wabunge ili watunge sheria ya kulazimisha mikataba yote ipelekwe bungeni, au wakatunga sheria ya kusitisha utekelezaji wa mikataba yote mpaka waione na kuijadili. Hii inawezekana chini ya kivuri cha ibara ya 64 (1) inayowapa wabunge mamlaka yote ya kutunga sheria. Hata hivyo, tusidharau ukweli kuwa utaratibu mzima wa kuanzisha muswada mpaka ukawa sheria unaratibiwa na ibara ya 97 (1), ambapo lazima miswada ya sheria ipate kibali cha Rais.

Ugumu unakuja pale ambapo, katiba yetu haikuainisha mahala popote, utaratibu unaotakiwa kufuatwa wakati wa kuanzisha Muswada. Suala la nani ndani ya Bunge mwenye mamlaka ya kuanzisha Muswada limeachwa likielea ndani ya katiba. Ingawa ibara ya 63 (2) inalipa mamlaka Bunge ya kuisimamia na kuishauri Serikali kwa niaba ya wananchi, lakini Bunge letu ni la mseto, kwa maana kuwa, hata Serikali inayosimamiwa imo ndani ya Bunge. Ibara ya 53 (1) inasema wazi kuwa Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais. Ibara 53 (2) inampa mamlaka Rais ya kufanya maamuzi ya sera za Serikali kwa ujumla, na wakati huohuo, inawapa Mamlaka Mawaziri chini ya uongozi wa Waziri Mkuu kuwajibika kwa pamoja Bungeni. Ibara ya 97 (1) inatoa mwongozo wa utaratibu wa Bunge kupitisha Miswada kwa njia ya mijadala. Kwa mantiki hii, Serikali inaweza katika mijadala kupiga kushauriwa, au kusimamiwa, hivyo kufanya jambo lolote la msingi kufa kifo cha kawaida ndani ya Bunge kitu ambacho kinafanyika sasa hivi.

Katika mseto wa namna hii ndani ya Bunge letu, Katiba yetu imefanya makosa makubwa kutokuanisha kwa kinaga ubaga kuwa ni wepi ndani ya huo mseto wana mamlaka ya kuanzisha Muswada na kuupeleka Bungeni ili ujadiliwe, na ni wepi hawana hayo mamlaka. Kosa hili ndilo limetutia kilema na kulifedhehesha taifa kwa jinsi ilivyo sasa hivi. Waziri Mkuu, Mawaziri na Manaibu wao, ambao wote ni wabunge kwa mujibu wa ibara za 51 (1) na 55 (4), hawawezi kuanzisha muswada wa kujisimamia wenyewe, alafu wakapiga kura ya kuupitisha ili uwe sheria, kwani wao ndio Serikali yenyewe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wabunge wa kuteuliwa na Rais kwa mujibu wa ibara za 59 (1) na 66 (1) (e), hawawakilishi wananchi Bungeni, hivyo ni vihoja kuwashirikisha katika mijadala na hata kupiga kura za kupitisha Miswada ya kuisimamia Serikali Bungeni.

Ni rahisi kuongea kwamba mfumo wetu umeundwa na mihimili mitatu, kwa maana ya Serikali, Bunge, na Mahakama. Hata hivyo, naufananisha mfumo huu na mafundisho ya sisi wakatoliki yanayosema kuwa Mungu ni mmoja, lakini amegawanyika katika Utatu Mtakatifu, yaani, Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Inaniwia vigumu kumtenganisha Mungu Roho mtakatifu na Mungu mwenyewe. Hivyo, naamini kuwa Mungu ni mmoja. Katiba yetu imeweka mazingira ya utata kiasi kwamba napata ugumu wa namna hiyo kutenganisha Bunge na Serikali yetu. Katika muingiliano wa namna hii, labda kama katiba ingeainisha wazi, ni vigumu kutenganisha majukumu na utendaji kazi wa Bunge na ule wa Serikali. Si rahisi kujua ni wakati gani Bunge linakuwa Bunge, na ni wakati upi Bunge linakuwa Serikali, pia ni wakati gani Serikali inakuwa Bunge, na niwakati gani Serikali inakuwa Serikali. Hapa sijaongelea ni wakati gani Bunge linakuwa tawi la chama cha siasa.

Katiba, Mikataba, Madaraka ya Bunge, na Ulaghai wa Serikali

Hata hivyo, ibara ya 89 (1), imelipa mamlaka Bunge jukumu la kujiamulia utaratibu wa kutekeleza shughuli zake. Hapa ndipo wanaweza kuunda kamati za Bunge na mambo mengine. Kutokana na katiba kutokutamka wazi kuhusu nani hasa miongoni mwa huu mseto wa Wabunge anapashwa kuanzisha Muswada, Serikali ambayo iko ndani ya Bunge, imetumia mwanya huu wa kisheria kujipendelea na kuwabagua wabunge wengine waliobaki ambao hasa ndio wawakilishi wa wananchi. Bahati mbaya, walijiwekea utaratibu wa kudumu wa Bunge kwamba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mawaziri, pamoja na Manaibu wao, ndio tu wenye haki ya kupeleka Miswada bungeni. Wabunge waliobaki ambao hawana kofia mbili, kazi yao ni kuuliza maswali, kupiga makofi na vigeregere, kujadili, na kupitisha Miswada tu.

Kumbuka, kabla Muswada haujapelekwa Bungeni, unapitishwa kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri. Kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 54 (2), Rais ndiye anaongoza mikutano yote ya Baraza la Mawaziri. Kwa minajili hii, hakuna Muswada unaoweza kupenya Baraza la Mawaziri na kupelekwa Bungeni bila ridhaa ya Rais. Ndio maana toka Bunge letu lianzishwe, haijawahi kutokea Rais akakataa Muswada uliopitishwa na Bunge, kwasababu yeye ndiye anaridhia Miswada yote kabla haijaenda Bungeni kupitia Baraza la Mawaziri. Kwa maana hii, ngonjera zote katika ibara ya 97 kifungu (2) mpaka cha (4), zinazo elezea danadana baina ya Bunge na Rais, endapo Rais atakataa Muswada kutoka bungeni, hazina maana yoyote. Ni mapambo. Kwa mantiki hii, nitakuwa sijakosea nikisema kuwa wabunge wetu ni vikaragozi, kwa maana kwamba wanamtumikia Rais ambaye sera zake nyingi zinatungwa na Mabeberu kwa manufaa ya Mabeberu.

Ibara ya 97 (5) inaliwezesha Bunge kumpa mtu yoyote au taasisi yoyote ya Serikali madaraka ya kuweka kanuni za nguvu ya Kisheria. Binafsi, naona Serikali imekuwa ikitumia vifungu kama hivi ndani ya katiba, kuanzisha taasisi na kulitumia Bunge kuzipa madaraka yasiyo na mipaka, kadhalika, Mawaziri wamekuwa wakitumia huu upenyo kuhodhi na kujilimbikizia madaraka yasiyo na kifani. Ufidhuli huu wa Serikali, umefichama ndani ya taratibu za kujipendelea kuwa wao ndio pekee wanaoweza kupeleka Muswada wa sheria Bungeni na wala si wabunge wa kawaida waliochaguliwa na wananchi.

Mfano, mnamo Aprili 1992, Serikali ilipeleka Muswada Bungeni wa kubadilisha sheria ya mwaka 1969 ya Mashirika ya Umma ili kuruhusu ushiriki wa watu na makampuni binafsi katika uendeshaji na umiliki wa hayo Mashirika. Ndani ya huo Muswada, lilikuwepo pendekezo la kuanzisha taasisi ya Serikali ya kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC), ambapo Bunge liliridhia. Vilevile, Novemba 1993, Serikali ilipeleka Muswada Bungeni wa kuliomba Bunge liiongezee (PSRC) madaraka zaidi, ambapo Bunge liliridhia pia. Kwa maelezo zaidi kuhusu huu Muswada ambao unaweza kutoa majibu kwa wabunge wetu, chungulia (New Public Corporation Act 1993).

Katika Muswada huo mpya wa 1993 ambayo ndiyo sheria inayoendesha utaratibu wa kuingia mikataba yote ya kuyauza mashirika yetu ya Umma, Bunge liliainisha kwa kinaga ubaga utaratibu mzima wa kuuza Mashirika ya Umma kwa kuipa mamlaka PSRC. Bunge lilitoa maelekezo kwamba, uamuzi wa kulibinafsisha Shirika la Umma husika unafanywa na na Waziri ambaye hilo Shirika la Umma liko chini yake. Kwamba inaundwa timu (Divestiture Technical Team – DTT), inayojumuisha Maofisa kutoka Wizara ya Shirika linalobinafshishwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hazina, Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji), Wizara ya Ardhi, PSRC, na Shirika lenyewe linalobinafsishwa. Katika kutekeleza majukumu, yanatakiwa yawepo mawasiliano baina ya hao maofisa, na Mawaziri wa hizo Wizara.

Baada ya taratibu zote kukamilika, DTT inapeleka mapendekezo yake ya mwisho kwa PSRC. Mapendekezo yanapitiwa na kufanyiwa marekebisho kama yanahitajika, alafu yanapelekwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri. Kama mapendekezo hayo yatapitishwa na Baraza la Mawaziri kwa maana ya kuridhia, basi makaratasi yote yanapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kabla ya mnunuzi wa Shirika la Umma na mwakilishi wa Serikali hawajatia saihi.

Kama mambo yote yako shwari, basi PSRC wanapewa "Power of Attorney” kusaini mkataba kwa niaba ya Serikali. Hii sheria ilitungwa na Bunge mwaka 1993. Hakuna mahala Wabunge walisema kabla mkataba haujasainiwa, waulete Bungeni ujadiliwe na kuridhiwa. Hata upande wa uwekezaji wa moja kwa moja (direct fresh investment) mambo ni yaleyale, utaratibu kama huu ulifanywa na Serikali. Chungulia Tanzania Investment Act No. 26 ya mwaka 1997, ambapo Bunge liliipa Mamlaka taasisi ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) kuratibu shughuli nzima za uwekezaji wa moja kwa moja.

TIC haikupewa madaraka makubwa kama ilivyopewa PSRC. Badala yake, Bunge limepitisha sheria tofauti zinazowapa Mawaziri wa Wizara husika madaraka yasiyo na mipaka. Mfano, Mining Act ya mwaka 1998, ibara ya 10 vifungu (1) na (2) vifungu vidogo (a), (b), na (c), vinampa Waziri wa Madini uwezo wa kusamehe au kuhairisha kodi, pamoja na mauzauza mengine.

Kumbuka katiba ya nchi yetu kupitia ibara ya 99 (1) na (2) (a)kifungu kidogo (i), inalipiga marufuku Bunge kutunga sheria za kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza. Badala yake, ibara ya 99 (1) inampa mamlaka Rais kupeleka pendekezo Bungeni linalohusu mambo ya fedha kwa kumtuma Waziri. Ni katika ibara hii peke yake iliyoainisha wazi kuwa Muswada wa mambo ya kodi na mengine yahusianayo na fedha unaweza kupelekwa Bungeni na Waziri likiwa kama pendekezo kutoka kwa Rais.

Nakubali kuwa Katiba inalipa Bunge mamlaka ya kuiona hiyo mikataba baada ya kusainiwa, lakini lilijivua lenyewe madaraka ya kuijadili na kuiridhia mikataba mingi kabla haijasainiwa. Hii inachangiwa na mapungufu ndani ya katiba yetu, ulaghai na undava wa Serikali, na ukweli kuwa Miswada mingi inaandikwa kwa makusudi kiufundi kwa lugha ya Kiingereza, na wabunge hawataki kushauriana na wananchi kabla ya kuipitisha. Vilevile tumeona picha za Wabunge mbalimbali wakiwa wamelala usingizi mzito wa fofofo wakati wa vikao vya Bunge, na wengine wanaendekeza tabia za utoro, hivyo, Miswada inapita bila wao kuwa na taarifa.

Hata kama udhaifu huu usingekuwepo, bado udhoofu wa katiba yetu unaowalazimisha Wabunge kuajiliwa na Vyama vya siasa ndio unaosababisha Bunge letu lisiwe na nguvu. Hakuna Mbunge mwenye ubavu wa kupinga wakubwa wake wa chama ndani ya Bunge alafu akaendelea kuwa Mbunge. Walijaribu akina Ngunangwa, lakini jamii imekwisha wasahau.
Hakuna Mbunge ndani ya chama tawala mwenye uwezo wa kumpeleka mwajili wake Mahakamani, alafu akaendelea kuwa Mbunge. Dawa ya ugonjwa ya ufidhuli wa Serikali ni kuhakikisha kwamba wabunge wote wameajiliwa na wananchi. Hii italifanya Bunge liwe na ubavu wa kuisimamia na kuishauri Serikali. Sasa hivi Serikali ni mwajili wa Wabunge kwa kupitia mtambo wa vyama vya siasa. Unaweza kushauri, lakini huwezi kusimamia mwajili wako. Haiwezekani.
 
Mzee Kyoma, nimeweka jembe chini, nimepangusa jasho, na kujikuta natikisa kichwa kukubaliana na wewe! Haya ni maneno mazito ukweli wake hata hivyo ni mzito zaidi na wenye kufungua mawazo!
 
Hiyo civics yako Kyoma ni nzito. Binafsi sikuwahi kuitazama katiba kwa jcho kali kama lako. Umenifanya nami nianze kuichimba katiba yetu zaidi na zaidi. Inabidi niigawanye katiba yetu katika module ili niikamate sawasawa. Hiyo ni shule kamili. Ushukuriwe na kubarikiwe pia.

Lakini, hebu piga hatua kidogo mbele na kuchangia pia katika mazingira hayo tuliyo nayo na wabunge wetu hao vikaragosi, tufanyeje? Kuna mada pia nimeanzisha kule kuhusu matatizo ye demokrasia yetu, maana naona haya matatizo yote ya katiba yanatokana na sisi wananchi na viongozi wetu kuikataa demokrasia. Hivi tufanyeje katika kuishamirisha demokrasia yetu?
 
Kyoma!
Tunaposema tunahitaji Katiba ni kwaajili ya mashimo makubwa kuwa mengi ,BARABARA Haitufikishi kule tuendako kwasababu ya uwepo wa mashimo haya makubwa.Hata marekebisho kadhaa ya katiba yaliyowahi kufanyika ni kujenga mianya ya watawala kuamua bila ya kuulizwa.
 
Mwanakijiji: Nimesoma article yako, ni shule nzito hasa kwa hawa waheshimiwa wabunge. Ahsante sana.

Wakikuita mwezi wa sita bungeni kujieleza usisite kututaarifu hapa bodini, maana wabunge wetu huwa hawapendi kuguswa. Wanafikiri wanajua kila kitu kumbe wengi wao hamnazo kabisa.
 
mwanasiasa, nilipokuwa chipukizi moyo wa kizalendo ulipandikizwa na kile kiapo cha "nitaitumikia nchi yangu, saa yoyote, wakati wowote, na mahali popote nitakoamriwa". anyway, they better have msn or something...!!
 
mwanasiasa, nilipokuwa chipukizi moyo wa kizalendo ulipandikizwa na kile kiapo cha "nitaitumikia nchi yangu, saa yoyote, wakati wowote, na mahali popote nitakoamriwa". anyway, they better have msn or something...!!

Watoto wa siku hizi kiapo hiki hawana. Umenikumbusha mbali sana. Unajua wakati ule kulikuwa na mambo madogo madogo ambayo yalitupa ujasiri wa uzalendo. Siku hizi nasikia hata wimbo wa taifa vijana hawaimbi mashuleni.

Hivi wabunge tunasoma na kuilewa katiba? Sijui..... maana kama ingekuwa hivyo hata katiba hii hii na ubaya wake tungekuwa mbali sana katika utawala bora. Kumbukeni bunge la chama kimoja.Why lilikuwa imara?
 
Suala hili la katiba ni muhimu sana, nimenufaika na mengi sana ktk mada hii. Thanx Kyoma.

Ombi

Mh Zitto wahamasishe waheshimiwa wabunge wenzio wawe wanapitia humu wajifunze. Badala ya kung'ang'ania kusoma Ijumaa, Sani, Kasheshe and the like.
 
Back
Top Bottom