bm21
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 774
- 36
Sasa tufanyeje?
Bulesi, katoa jibu hapo juu. Msome vizuri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa tufanyeje?
Madiliko ya katiba sio kitu ambacho hufanywa bila ma referendum and other consultative procedures. Na wazo lakusema kwamba mtu ikifika 2010 na tukabadili katiba CCM haitashinda uchaguzi, that is foolishness. I see no other party that is capable of running the country. Not for another 10-15 years. Wapinzani imewachukua election ya 95,2000,2005 (3) kurealize that they should be focusing on parliamentary elections, getting more seats and enough political experience in the eyes of the people then eventually wagombee Urais... It was obvious from the onset so the fact that they are sooo slow not to have seen it goes to show that they wont really be any better..
Mapinduzi yakimawazo nakisiasa yanachuku muda jamani, haka kanchi hakana ata 50 years. We are ayoung nation.. surely if we build on what we have taratibu, tutafikia point ambapo tutakua na vyama ambavyo vinaweza kupeana challenge. Lakini ata iweje hilo haliwezi kutokea 2010 na anaesema hivyo ni muongo.
Ibara ya 7(2)...ina maana gani?SEHEMU YA PILI
MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO
WA SHUGHULI ZA SERIKALI
6. Katika Sehemu hii ya Sura hii, isipokuwa kama maelezo
yahitaji vinginevyo, neno "Serikali" maana yake ni pamoja na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka
au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote.
7.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali,
vyombo vyake vyote na watu wote au mamlaka yoyote yenye
kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria
au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa
kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya
Sehemu hii ya Sura hii.
(2) Masharti ya Sehemu hii ya Sura hii hayatatiliwa nguvu ya
kisheria na Mahakama yoyote. Mahakama yoyote nchini
haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda au
kukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote, au kama
sheria, au hukumu yoyote, inaambatana na masharti ya
Sehemu hii ya Sura hii.
8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(2) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vyombo
vyake na uendeshaji wa shughuli zake, utatekelezwa kwa
kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya kukuza
umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
9. Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa
chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na
kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitiza
utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira
yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya
Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na
shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-
(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu
zinaheshimiwa na kuthaminiwa;
(b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
(c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia
ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa
unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa
manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia
mtu kumyonya mtu mwingine;
(d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa
na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi
anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli
yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;
(f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na
kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la
Dunia kuhusu Haki za Binadamu;
(g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma
vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa
waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya
mtu;
(h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi,
rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
(i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo
maendeleo ya wananchi na hasa zaidi
yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha
umaskini, ujinga na maradhi;
(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia
zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia
kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache
binafsi;
(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya
demokrasia na ujamaa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
10. [Ibara ya 10 ya Katiba imefutwa na Sheria Na.4 ya
1992].
11.-(1) Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili
ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya
kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii
wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali
nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi. Na bila kuathiri haki hizo,
Mamlaka ya Nchii itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba
kila mtu anaishi kwa jasho lake.
(2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia
atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia
upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.
(3) Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu
wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata
elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo
vinginevyo vya mafunzo.
Mkamap, Katiba ya Tanzania inapatikana kwenye tovuti ya http://www.tanzania.go.tz
Asante
Lakini kwanini ni peruzi wakati wenda jibu watu hapa wanalo kirahisi. Harafu link yenyewe ina wadudu
Naomba kufahamishwa katiba yetu inaongea nini ktk uteuzi wa waziri mkuu. Je anateuliwa na Rais ama ni chama ndo kinamteua baada ya kupata viti vya bunge vya kutosha. Na kama anateuliwa na Rais je ikitokea Rais katoka chama kingine na chama chenye viti vingi ni kingine je Rais ata apoint waziri mkuu wa chama kingine.?
Nauliza hivi maana sasa nimelekeza mashambulizi yangu ktk Wikipedia.Org kwa kurekebisha mambo kule, kwa maana nimechoka na wazungu kutuandikia mambo yao. Kuna sehemu nimekuta wanasema tuna university mbili ila nimesharekebisha japo si kwa usahihi sana.
Watanzania naomba tuwe wazalendo kwa kutoa taarifa muafaka hasa ktk hizi mitandao, maana wenzetu ndo source zao za habari.
MkamaP
Ikisemwa kuwa tunahitaji katiba mpya haieleweki kwenye masikio ya watawala wetu.
Lakini kuna mambo mengi sana yatatutatiza siku sisi m wakipoteza uhalali wa kututawala tena.
Watawala wetu wanafahamu jambo hili na wanajifanya wataendelea kututawala milele, hizi ndoto siku zikikoma tumeingia kwenye mgogoro mkubwa.
Kuna maswali kama hayo unayouliza mengi tu, na hayana majibu mbali na kuambiwa kuwa katiba yetu haina matatizo.
Kuhusu vyuo vikuu nenda www.tcu.go.tzNaomba kufahamishwa katiba yetu inaongea nini ktk uteuzi wa waziri mkuu. Je anateuliwa na Rais ama ni chama ndo kinamteua baada ya kupata viti vya bunge vya kutosha. Na kama anateuliwa na Rais je ikitokea Rais katoka chama kingine na chama chenye viti vingi ni kingine je Rais ata apoint waziri mkuu wa chama kingine.?
Nauliza hivi maana sasa nimelekeza mashambulizi yangu ktk Wikipedia.Org kwa kurekebisha mambo kule, kwa maana nimechoka na wazungu kutuandikia mambo yao. Kuna sehemu nimekuta wanasema tuna university mbili ila nimesharekebisha japo si kwa usahihi sana.
Watanzania naomba tuwe wazalendo kwa kutoa taarifa muafaka hasa ktk hizi mitandao, maana wenzetu ndo source zao za habari.