Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Babu yangu(RIP) aliwahi kuniambia kuwa hakuna marehemu mbaya. Yaani mtu akishafariki ni ngumu na ni mara chache mno kuzungumziwa mabaya yake. Kinachotawala huwa ni mema ya marehemu tu!
Mowzey Radio jina halisi ni Moses Ssekibogo kaicha dunia akiwa bado kijana kabisa miaka 33. Alikuwa na kipaji cha sanaa na kupendwa pia. Inawezekana kabisa kama ni mashindano ya kupendwa Kampala angeweza kuchukua number moja. Alipendwa sana yeye na nyimbo zake pia kupendwa huku hasa na mabinti na wanawake ilimpelekea kuwachakaza hasa.
Alikuwa anaelekea kwenye kilele cha mafanikio kupendwa, utajiri na umaarufu kifo kilipomkuta kwenye ugomvi uliotokea kilabuni kwa kupokea kipondo kilichosababisha alazwe hospital siku kadhaa.
Mowzey Radio msanii huyu maarufu akifanya kazi zake na Weasel licha ya kipaji mafanikio na kupendwa kwake alikuwa ni kijana mkorofi sana na mwenye jazba sana. Hali hii ilimpelekea kugombana na kuwa na mitafaruku ya mara kwa mara na watu wake wa karibu, wasanii wenzake na wana jamii.
Magomvi yake ni mengi lakini kwa uchache yanayokumbukwa zaidi ni kati yake na
1. Khalifa Aganaga. Huyu waliwahi kufanya kazi pamoja Goodlyf
2. Bebe cool msanii mwenzake
3. Jeff Kiwa manager
4. Traffic police. Huyu mama akitaka kumkamata kwa makosa ya kuendesha gari kwa fujo na ulevi
5. Huu wa mwisho ulioondoka na roho yake inasemekana alimuita bouncer wa bar husika BOOZER ambayo maana yake kwa kiswahili ni mlevi mbwa.
Mowzey alikuwa anapenda kujiona star na kutaka kupewa VIP treatment kila alipokuwa hali iliyomfanya agombane na watu kila mara. Kwenye msiba wa Ivan alichukua laptop ya DJ na kuitumbukiza kwenye maji kwa kisa kidogo tu.
Waganda wanamlilia sana. Museveni Kaguta alichangia dola 8300 kwenye Matibabu yake lakini hakuweza Kupona. Kaondoka ni msiba mkubwa kwenye tasnia ya usanii Afrika mashariki lakini huo ndio ulikuwa upande wake wa pili.
RIP Mowzey Radio