Moyo wangu unaungua, Akili inaharibika, Mwili unakonda, Mapenzi yanatesa sana

Pole sana mapenzi hayatabirikagi yani hayana fomula!
 
Mbona wewe hujaelezea upande wako ? Wewe ulikua kama malaika hukuwahi kumkosea hata mara moja ndani ya kipindi chote icho? Wanawake mnapenda sana kutafuta huruma mda mwingine
 
Pole SANA maam!

" Ni nyakati nzuri maishani ambazo hugeuka GHAFLA na kuwa nyakati mbaya bila HATA kutegemea"

Nakupa somo

Sisi wanaume tuliowengi tukiwa na fedha halafu tukiwa mbali na mke au wapenzi wetu,mchepuko au michepuko huwa natural solution!

YAANI wanawake kama mna akili usikubali kuishi mbali na mpenzi wako au mke kisa Biashara au kazi!YAANI pambana KILA siku moja mbili au tatu uwepo eneo husika!

Kwanini!!?

Coz mwiba ukisimama na kuchachamaa USIKU wa manane utachoma nani!!?!


Huyo JAMAA alipata pressure ya hela na pressure ya kukosa liwazo la KILA siku kitandani!

Mwambie umemsamehe japo hajaomba msamaha halafu mwambie asijali nyakati zitapita tu na mambo yatakaa sawa hata asijali!!!

Chukua hiyo!!
 
Nimeishia kusoma hapa “…tulilia sana..” . smh [emoji23][emoji23][emoji23]
 
hadi huzuni dada rudi kwa Mungu sali sana kula vyema jichanganye na watu wenye maadili sikiliza nyimbo za furaha utapata mwingine wa kukupenda tena sana kwa Mungu linawezekana
 
Najitahidi sana, mwanzoni ilikua nalazwa sana na presha ila sasa hata presha zimepungua ila ni moyo tu bado unauma na akili haijakubali, naishukuru pia family yangu kwa kua na mie bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu [emoji120]
Natamani kujua unaendeleaje, ulishajifungua na mumeo alifanikiwa kurudi??
 
Natamani kujua unaendeleaje, ulishajifungua na mumeo alifanikiwa kurudi??
Ndio Dada nilifanikiwa kujifungua salama mwezi Disemba alhamdulillah mtoto mzuri wa kiume,
Mume bado hajarudi na hata kumuona mtoto hajaja, niliacha kulia sasa nina furaha na amani kila nikimuangalia Simba wangu ananipa sana nguvu na ujasiri,

Allah anikuzie kwenye maadili mema, amiin
 
hongera sana , hongera.
salamu nyingi kwa mtoto, namtakia kukua vizuri nawe ujaliwe kila uwezo wa kumlea vizuri.
 
Wow! Hongera sana nimefarijika kwa ujasiri wako, hakika watoto ni zawadi kubwa sana, angalia PM yako tuyajenge huko.
 
Pole sana dada,jitahid uwezavyo kumsamehe na kujisamehe pia,then muombee yeye,familia Yako na ww mwenyewe . Kwenye maisha mitihan ipo japo inapita
 
Pole sana mkuu Ila usiishi na Sonona Muziki ni Dawa

Weka Muziki & enjoy your 'Past' is gone
🎶
Sisi sio Milima tutakutana
Sisi ni Pipo tutaonana
Sisi sio Visima tutasomana
Tukiwa km Pipo kitaumana umana
🎶
Nikiwa kwenye low vibe hua na-tune hio sounds vibe ya abha & remix-killer then life goes on nikiwa na high vibe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…