Moyo wangu unaungua, Akili inaharibika, Mwili unakonda, Mapenzi yanatesa sana

Ahsante sana, kwa sasa namuombea sana hasa kesi yake iishe, bado nina asilimia chache atarudi labda nikijifungua na akiiona damu yake
Usiache kumuombe huyo bado ni mumeo na baba mtarajiwa wa mwanao. Akiharibikiwa bado watu watakaoumia ni wewe na mwanao mtarajiwa.
Kikubwa msamehe na jisamehe mwenyewe upate amani ya moyo, kuna muda nao wanapitia majaribu hawajakamilika.
Na mali zinatafutwa mtapata zingine, na km unavyosema zilikuwa za umma. Endelea kuomba Mungu
 
Ahsante sana Mwanamke mwenzangu kwa kunitia moyo, hakika nahitaji hii faraja mnoooooo,
Ubarikiwe sana
 
Nyie wanawake hamtabiriki. Unaweza kuta wewe ndio chanzo cha matatizo. Domo reeeefu lisiloisha maneno. Shuwain sana wanawake

Mke wangu akiwa anajieleza kwa mama yangu unaeza sema malaika mtiifu anazungumza, lakini balaa la mke wangu nalifahamu mimi na wanangu ambao nao wamejazwa sumu na mama yao

Pmbv sana wanawake. Na kwa taarifa yako sirudi tena. Lea mwenyewe hiyo mimba wa Shabani Mapesa
 
Nakushauri jambo la kiutuzima ngoja nipaki.
Pole sana maisha bila mapito Sio maisha hayanogi,wewe sio wa kwanza wengi Wana mazito zito yako na wamesimama.
Huyo ndio mmeo wala usimuache
Upaki nini tena mkuu. Ama nguo kwenye shangazi kaja?
 
Pole sana kikubwa anza kubeti yani kamari ni kama utani lakin wallahi hutakaa umfkrie kiumbe mwngne pia zngatia lishe na kusali mengn yapo tuh
 
Time heals nothing dear, jitahidi kuishi nalo ili uokoe hiko kiumbe tumboni kisizaliwe na stress.....sometimes tunapenda watu wasiosahihi en shukuru hata kajiengua mapema
Shukrani sana dear, najitahidi sana stress zisinitawale zikaathiri kiumbe changu, naimani Mola atanivusha salama kwenye hili πŸ™
 
Japo hadithi ni ya kutunga lakini kama tabia zake ni hizo hafai. Hata asikupe talaka achana naye. Asante kwa hadithi yako ya kutunga.
Na kweli mkuu. Halafu kinachotatiza, upande wote wa madhaifu kaweka kwa mwanaume kana kwamba yeye hakuwahi kurusha hata tusi. Hawa wanawake bhana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…