Moyo wangu unaungua, Akili inaharibika, Mwili unakonda, Mapenzi yanatesa sana

Na alipoharibu ni pale alipoanza kuongelea habari za kununua viwanja na kujenga misauzi ndani ya wiki mbili tokea kuanza kazi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Salaam waungwana wote,
Kwa kweli katika kitu najuta maishani ni kumpenda huyu mtu, nimekua nae kwa miaka 7 sasa, niseme tu nilimkuta hana kitu kabisa sikujali kitu nilijali mapenzi, tukaanza mapenzi na yalikua moto moto, alikua anafanya kazi sehemu kwa mshahara mdogo sana, wakati huo mie nipo chuo,

Nikaanza mizinga home jumlisha na mshahara wake tukaanza kununua vitu vya ndani, ndani ya miezi kadhaa chumba kilijaa, nikamshawishi tuhame ile nyumba na kuhamia eneo lingine tukapata chumba self na sebule,

Kufupisha story, nilivyomaliza chuo, tukafunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mke na mume, upendo ulikua mkubwa sana, mimi nikiwa nimejiajiri na yeye alikua bado na ajira yake ile ambayo hakua anaifurahia,

Nakumbuka siku moja, kaka yangu akanambia kuna ajira zimetoka ila ni mkoa X nimjulishe mume wangu ili amfanyie mpango , nikamjulisha alivyorudi jioni akampigia shemeji yake, kwa kweli ilikua shangwe maana mshahara ulikua mnono na marupu rupu tele, baada ya kufurahi, mwenzangu akabadilika ghafla, kumuuliza kisa akasema ataniacha peke yangu na hajazoea kua mbali na mimi, tulihuzunika lakini nilimpa moyo kua aende akatafute, kikubwa akumbuke familia aliyoiacha ambayo ni mimi (hatukua na mtoto) akaniahidi vitu vingi vya kunitia moyo na kunifariji...

Siku ya safari ikawadia, ilikua ni siku ngumu sana kwetu, tulilia sana hatimae akaondoka, nikaanza maisha rasmi ya upweke,

Ndani ya miezi sita akanitumia pesa ninunue kiwanja tuanze ujenzi chap, nilifurahi sana na tukaanza ujenzi wa nyumba yetu hadi ikaisha, alirudi baada ya mwaka mmoja, kipindi chote hicho hatukuwahi kukwaruzana, tulishirikiana kwa kila jambo, kurudi kwake ilikua ni likizo ya miezi miwili, akanunua tena kiwanja kingine akajenga foundation, kiufupi maisha yalikua mazuri, siku anaondoka tukaondoka wote nikapaone anapoishi, nilikaa kwa wiki 2 ila nikagundua anapata pesa nyingi sana na wala hatagemei mshahara, nikamuuliza akasema anapiga madili, nikamuonya awe makini asije akaishia jela na jasho lote likapotea akanijia juu na kudai Wanawake ndio tulivyo, tunapenda kuwaza negative muda wote ndio maana hua hatushirikishwi, basi nikamtaka radhi na maisha yakaendelea,

Nilivyorudi, akabadilika sana, akawa busy, anaweza asipokee simu hata wiki anadai busy, ila whatsapp anaonekana na kupost, akawa bata kwa sana, kampan ya kutosha, akanunua na gari ya kutembelea, nilikua naumia sana na mabadiliko yake siku moja nikaenda ghafla mkoa X, nilivyofika nyumba anayoishi nikamtumia msg kua nipo nje kama anaweza mtuma mtu aniletee funguo, akapiga video call akashtuka kuona ni kweli, akaja mbio mbio na lawama kibao kwann nimekuja ghafla, kufungua ndani nikakuta kusafi na nguo za mwanamke zimepangwa vema, kumuuliza akadai kuna mfanyakazi mwenzie aliomba hifadhi yeye alimpisha akaenda kulala hotel, sikutaka malumbano nikazitoa na kuziweka kwenye mfuko, nikamwambia atampatia akimuona, nilikaa pale nikagundua ana wanawake wanne na wote hufika pale kwake, akawastopisha eti mke wake amekuja, niweke wazi sikushiriki nae tendo nilimwambia hadi tupime magonjwa ya zinaa ikiwemo HIV akagoma, basi tuliishi kama marafiki tu hadi siku alipochoka tukaenda kupima wote tukawa poa, mimi nikaondoka, ila Moyo wangu alikua ameshaurarua sana, nikajikuta namchukia hata zile dua njema nilizokua namuombea mume wangu nikaacha, nikaamua kufocus na biashara yangu, nikawa simtafuti kama zamani hadi siku mwenyewe anikumbuke,

Mwaka jana akarudi likizo ya miezi mitatu, kumbe kasimamishwa kazi asiseme, mara akauza bajaji, mara piki piki kumbe anaenda kwa waganga mie khabari sina,

Mwaka huu ndio napata kujua na hasa baada ya miezi mitatu kuisha mtu haondoki, kumbana ndio anasema ukweli wote, wanajadiliwa wakikutwa na hatia wafukuzwe kazi ama washtakiwe, nikamwambia asiwaze amuombe tu Mungu amvushe ila aachane na Waganga wanammalizia pesa, nashukuru alinielewa, ila sasa akaanza kua mlevi yaan analewa hadi analala huko huko Bar, nikajaribu kuwashirikisha familia yake ikawa kazi bure, na mie kuja kushtuka ni mjamzito, kwa kweli ilitupasa tufurahi maana ni ujauzito wetu wa kwanza lakini kwa yanayoendelea tuliishiwa furaha kabisa,

Ujauzito ulikua unaniendesha sana ikanibidi niende kwa wazazi wangu, mwenzangu akauza kiwanja kile alichoanza kujenga foundation, nakumbuka alikuja kuniona na kunipa hizo taarifa, alikaa kwa siku 3 ujauzito ukiwa na miezi miwili tu, siku anaondoka akanipa laki 6 na kuahidi angerejea tena baada ya mwezi,

Mwezi ukapita na mawasiliano yalikua yakusua sua sana, siku moja akaniandikia waraka kua tuachane anahisi amefeli maisha na hawezi kunipa maisha aliyoniahidi na ujio wa mtoto ndio umemchanganya zaidi, anaona hawezi kua baba bora kwa hiyo nipambane mwenyewe, nilivyopata huo ujumbe ilikua mwezi wa tano, niliumia sana, nikampigia sana simu hakupokea, nikawashirikisha wazazi wetu wote, wa upande wangu hapokei simu, kwa mama ake anapokea na kumwambia yupo busy atakuja kuniona,

Mwezi wa saba familia yangu ikanambia niishi tu home, nimwambie anipe talaka nijiandae kwa kujifungua na maisha mengine, nikimwambia anipe talaka hajibu,

Kwa sasa najitahidi kuizoea hii hali ila nashindwa hasa nikiwaza kulea mtoto peke yangu, najiuliza nini kimempata hata kufikia kunifanyia hayo, natamani niondoke niende sehemu mbali sana, sehemu ambayo hakuna mtu ananijua nianze maisha upya ila sasa nina kiumbe kipo tumboni na soon kitazaliwa na kunitegemea,

Mapenzi haya sijui yalitoka wapi na sijui kwanini yanaumiza namna hii, natamani nisingeyajua 😭😭😭

Poleni kwa gazeti.
Hii ndoa sio ya kikristo
 
Na alipoharibu ni pale alipoanza kuongelea habari za kununua viwanja na kujenga misauzi ndani ya wiki mbili tokea kuanza kazi
We nae hebu tutolee kichaa chako, umeona uzi wa mwenzio ndio wa kutolea nyongo, pambana na hali yako usitafute kiki kwa wengine,

Amesema pesa ilitumwa baada ya miezi sita wakanunua kiwanja na kuanza ujenzi, kinachokuuma nini sasa, na wewe tafuta hela ufanye maendeleo chap.
 
Nimesoma yootee......
Mlipoanza kufika kilele cha mafanikio mkaachana na Mungu akaelekeza nguvu zenu huyu kwenye starehe yule akaacha kumuombea mwenzake aache pombe na wanawake
Unajua mahusiano na ndoa nyingi zinavunjwa kwa uchawi na ushirikina wa watu wa karibu.
Walina mmeanza kufanikiwa wakaona wawatenganishe tuu
 
Tusiwe na maneno negative na hii story, inaweza kumpa depression ndugu yetu. Tuchukuliwe katoa tu hali ya dunia, tunaweza rudia siku moja hii thread.
Sometimes the best way is to talk it out na kusikia watu wanasemaje.
Dada yangu pole pole pole sana pole tena. Ila niseme,
DONOT EVER GIVE UP ON YOURSELF.

Watu watakusema, Watu watakufanyia mabaya, ila kamwe hutakiwi jifanyia wala kujiwazia mabaya.
You have to go on with your Life. Haya ndio maisha. Usijutie, umedondoka inuka jipukute.
Wenzio wengi tu waliachwa na watoto inauma ila nakuomba Tuliza moyo. Utawaza sana mapenzi yanaumaaa saaana. Ila tafadhari. Embu jikaze. Jione wewe ni mzuri kuliko wote sisi au yeye anaokutana nao. MUNGU AKULINDE NDUGU YANGU
 
Lagertha pole sana dada yangu.
Maisha ya mwanadamu na pengine kiumbe yeyote hamna njia iliyo nyoofu ya moja kwa moja, kuna kupanda na kushuka kwingi.
Unachopitia muda huu ni moja wapo ya mlima wa kupanda,sio muda utaumaliza na kukutana na njia nyoofu, mbele kidogo utakutana tena na mteremko ,bonde, mlima ,kona nk.
Yote hii ni kawaida ya maisha.

Unachopitia kwa sasa kuna wengine wamepitia tena kubwa kuliko hilo lako lakini walivuka na kwa sasa wapo sehemu ya kusema asante Mungu .

Hivyo nawe kesho utasema asante Mungu, kwa sababu nyakati hazidumu iwe nyakati ngumu ama nyepesi.

Kwa sasa binafsi naona usizingatie kabisa kilicho tokea japo ngumu lakini ukijaribu utaweza, mzingatie mtoto mtarajiwa, muwekee malengo na nia njema, muandalie mazingira rafiki yanayo leta furaha.

Naamini hatutashindwa kabisa kujihudumia wakati wa kujifungua na uzazi, kwa sababu kuna ndugu upande wako hawatakuacha moja kwa moja.

Puuzia kabisa lililotokea, puuzia kabisa huyu baba , zingatia mambo mengine kabisa, toa hisia za maumivu , ikiwezekana liwaze sana hilo tukio, ukiweza lia machozi kabisa, ukimaliza kulia futa machozi nawa uso maji , jipake mafuta , lala kidogo , ukiamka liwe limefutika iwe mwanzo mpya wa amani.

Nimesikitika pamoja nawe, pole sana , yote ya yote maisha yanaendelea hivyo usijali sana .
 
We nae hebu tutolee kichaa chako, umeona uzi wa mwenzio ndio wa kutolea nyongo, pambana na hali yako usitafute kiki kwa wengine,

Amesema pesa ilitumwa baada ya miezi sita wakanunua kiwanja na kuanza ujenzi, kinachokuuma nini sasa, na wewe tafuta hela ufanye maendeleo chap.
[emoji851][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
We nae hebu tutolee kichaa chako, umeona uzi wa mwenzio ndio wa kutolea nyongo, pambana na hali yako usitafute kiki kwa wengine,

Amesema pesa ilitumwa baada ya miezi sita wakanunua kiwanja na kuanza ujenzi, kinachokuuma nini sasa, na wewe tafuta hela ufanye maendeleo chap.
🤣🤣🤣 umechamba kwa sound ya mama wema. Safi sana
 
Salaam waungwana wote,
Kwa kweli katika kitu najuta maishani ni kumpenda huyu mtu, nimekua nae kwa miaka 7 sasa, niseme tu nilimkuta hana kitu kabisa sikujali kitu nilijali mapenzi, tukaanza mapenzi na yalikua moto moto, alikua anafanya kazi sehemu kwa mshahara mdogo sana, wakati huo mie nipo chuo,

Nikaanza mizinga home jumlisha na mshahara wake tukaanza kununua vitu vya ndani, ndani ya miezi kadhaa chumba kilijaa, nikamshawishi tuhame ile nyumba na kuhamia eneo lingine tukapata chumba self na sebule,

Kufupisha story, nilivyomaliza chuo, tukafunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mke na mume, upendo ulikua mkubwa sana, mimi nikiwa nimejiajiri na yeye alikua bado na ajira yake ile ambayo hakua anaifurahia,

Nakumbuka siku moja, kaka yangu akanambia kuna ajira zimetoka ila ni mkoa X nimjulishe mume wangu ili amfanyie mpango , nikamjulisha alivyorudi jioni akampigia shemeji yake, kwa kweli ilikua shangwe maana mshahara ulikua mnono na marupu rupu tele, baada ya kufurahi, mwenzangu akabadilika ghafla, kumuuliza kisa akasema ataniacha peke yangu na hajazoea kua mbali na mimi, tulihuzunika lakini nilimpa moyo kua aende akatafute, kikubwa akumbuke familia aliyoiacha ambayo ni mimi (hatukua na mtoto) akaniahidi vitu vingi vya kunitia moyo na kunifariji...

Siku ya safari ikawadia, ilikua ni siku ngumu sana kwetu, tulilia sana hatimae akaondoka, nikaanza maisha rasmi ya upweke,

Ndani ya miezi sita akanitumia pesa ninunue kiwanja tuanze ujenzi chap, nilifurahi sana na tukaanza ujenzi wa nyumba yetu hadi ikaisha, alirudi baada ya mwaka mmoja, kipindi chote hicho hatukuwahi kukwaruzana, tulishirikiana kwa kila jambo, kurudi kwake ilikua ni likizo ya miezi miwili, akanunua tena kiwanja kingine akajenga foundation, kiufupi maisha yalikua mazuri, siku anaondoka tukaondoka wote nikapaone anapoishi, nilikaa kwa wiki 2 ila nikagundua anapata pesa nyingi sana na wala hatagemei mshahara, nikamuuliza akasema anapiga madili, nikamuonya awe makini asije akaishia jela na jasho lote likapotea akanijia juu na kudai Wanawake ndio tulivyo, tunapenda kuwaza negative muda wote ndio maana hua hatushirikishwi, basi nikamtaka radhi na maisha yakaendelea,

Nilivyorudi, akabadilika sana, akawa busy, anaweza asipokee simu hata wiki anadai busy, ila whatsapp anaonekana na kupost, akawa bata kwa sana, kampan ya kutosha, akanunua na gari ya kutembelea, nilikua naumia sana na mabadiliko yake siku moja nikaenda ghafla mkoa X, nilivyofika nyumba anayoishi nikamtumia msg kua nipo nje kama anaweza mtuma mtu aniletee funguo, akapiga video call akashtuka kuona ni kweli, akaja mbio mbio na lawama kibao kwann nimekuja ghafla, kufungua ndani nikakuta kusafi na nguo za mwanamke zimepangwa vema, kumuuliza akadai kuna mfanyakazi mwenzie aliomba hifadhi yeye alimpisha akaenda kulala hotel, sikutaka malumbano nikazitoa na kuziweka kwenye mfuko, nikamwambia atampatia akimuona, nilikaa pale nikagundua ana wanawake wanne na wote hufika pale kwake, akawastopisha eti mke wake amekuja, niweke wazi sikushiriki nae tendo nilimwambia hadi tupime magonjwa ya zinaa ikiwemo HIV akagoma, basi tuliishi kama marafiki tu hadi siku alipochoka tukaenda kupima wote tukawa poa, mimi nikaondoka, ila Moyo wangu alikua ameshaurarua sana, nikajikuta namchukia hata zile dua njema nilizokua namuombea mume wangu nikaacha, nikaamua kufocus na biashara yangu, nikawa simtafuti kama zamani hadi siku mwenyewe anikumbuke,

Mwaka jana akarudi likizo ya miezi mitatu, kumbe kasimamishwa kazi asiseme, mara akauza bajaji, mara piki piki kumbe anaenda kwa waganga mie khabari sina,

Mwaka huu ndio napata kujua na hasa baada ya miezi mitatu kuisha mtu haondoki, kumbana ndio anasema ukweli wote, wanajadiliwa wakikutwa na hatia wafukuzwe kazi ama washtakiwe, nikamwambia asiwaze amuombe tu Mungu amvushe ila aachane na Waganga wanammalizia pesa, nashukuru alinielewa, ila sasa akaanza kua mlevi yaan analewa hadi analala huko huko Bar, nikajaribu kuwashirikisha familia yake ikawa kazi bure, na mie kuja kushtuka ni mjamzito, kwa kweli ilitupasa tufurahi maana ni ujauzito wetu wa kwanza lakini kwa yanayoendelea tuliishiwa furaha kabisa,

Ujauzito ulikua unaniendesha sana ikanibidi niende kwa wazazi wangu, mwenzangu akauza kiwanja kile alichoanza kujenga foundation, nakumbuka alikuja kuniona na kunipa hizo taarifa, alikaa kwa siku 3 ujauzito ukiwa na miezi miwili tu, siku anaondoka akanipa laki 6 na kuahidi angerejea tena baada ya mwezi,

Mwezi ukapita na mawasiliano yalikua yakusua sua sana, siku moja akaniandikia waraka kua tuachane anahisi amefeli maisha na hawezi kunipa maisha aliyoniahidi na ujio wa mtoto ndio umemchanganya zaidi, anaona hawezi kua baba bora kwa hiyo nipambane mwenyewe, nilivyopata huo ujumbe ilikua mwezi wa tano, niliumia sana, nikampigia sana simu hakupokea, nikawashirikisha wazazi wetu wote, wa upande wangu hapokei simu, kwa mama ake anapokea na kumwambia yupo busy atakuja kuniona,

Mwezi wa saba familia yangu ikanambia niishi tu home, nimwambie anipe talaka nijiandae kwa kujifungua na maisha mengine, nikimwambia anipe talaka hajibu,

Kwa sasa najitahidi kuizoea hii hali ila nashindwa hasa nikiwaza kulea mtoto peke yangu, najiuliza nini kimempata hata kufikia kunifanyia hayo, natamani niondoke niende sehemu mbali sana, sehemu ambayo hakuna mtu ananijua nianze maisha upya ila sasa nina kiumbe kipo tumboni na soon kitazaliwa na kunitegemea,

Mapenzi haya sijui yalitoka wapi na sijui kwanini yanaumiza namna hii, natamani nisingeyajua [emoji24][emoji24][emoji24]

Poleni kwa gazeti.
Pole sana dada,Mungu atakusaidia,na maumivu hayo yatafikia ukomo wake,pia mshukuru Mungu huenda kakuepusha na jambo kubwa ambalo lingegharimu hata maisha yako.Huwa kila jambo hutokea kwa sababu,endelea kuomba Dua Mungu atakusimamia[emoji120]
 
Naona hapo unatumia I'd ya Lagartha nafhani ni yule character was series wa Viking, hivyo basi pambana kama yule Dada alivyopambana.Life is full of shit lisipotokea kwako litatatokea kwa yule but yote is part of the game.
 
Ningepata mtu kama wewe unayejua kupenda hata nisingehangaika.
mkuu hata ukpata wa style hii huwezi jua kua ndiye..watu wa style hii wana drama zsoisha usmchukulie kama alivyoeleza hapa,amini usiamini ana tabia ambazo usingeweza kuvumilia bila nguvu ya mungu..
but mtu sahihi ni ngumu kumjua had pale utakapompoteza.!
 
Kuna mengi nahis umetuficha umeruhusu tujue front end ila back end umeficha!

Tuliza akili kula vzr pumzika lea mimba yako vzr kbs naamini mungu atakusaidia utajifungua salama, mtunzs mwanao mpaka miezi sita plus, then rudi kwenye drawboard pambana kwa maelezo yako una back up nzuri ya familia angalia cha kufanya
 
Back
Top Bottom