Moyo wangu unavuja damu

Moyo wangu unavuja damu

Kanashimi

Sijui ni kwa Nini Daktari alikueleza wewe hizo habari badala ya mama.

Ninavyojua utaratibu mgonjwa ndio anatakiwa kuwa mtu wa kwanza kujua afya yake isipokuwa kama ana hali mbaya sana.
Yeye ndio ataamua kuwajulisha wengine.

Kwa kuwa imeshatokea mimi Nakushauri, usimwambie.
Mchukue mpeleke hospitali, Mueleze Mtoa huduma, amupime then ikithibitika anao yeye ndio amueleze.

DR Mambo Jambo unasemaje.
Usimwambie CHOCHOTE MAMA..

Imeniumiza Sana kuona Unethical Acts Imefanywa ambayo Inaweza Kugharimu Afya ya Kufikiri Na akili ya Familia Nzima..

Udaktari Ni Mzuri ila One Mistake Inaweza kugharimu the Whole society..

Kuna miongozo kwa ajili Ya Upimaji,Utoaji Majibu na Hata Ushauri wa Mgonjwa (Nasaha)..

Na naomba Niseme Si sawa kumuachia Layman ashughulike na swala la Kitaaluma..

Daktaria hakuwa sawa hata kidogo...
Sidhani hata kama huduma hiyo ya Upimaji imepimwa inavyostahili..Maana Hakukuwa na Pretest wala Post testing counselling Only imefanyika Testing "Kama Unapima magonjwa ya U.T.I?"

Hio ni Hatari sana..
Sitaki kuujudge kuhusu elimu Ya daktari ila Ninachoamini kuna wakati Sisi Madaktari tunajikuta Tunaacha taaluma zetu na kuamua kufanya Vitu kwa mazoea.."Thats sad"

My TAKE
Daktari kafanya makosa makubwa Sana "Grave mistakes", Ilipaswa afanye PITC au CITC (Provider Initiated HIV Test and Counselling) au (Client Initiated HIV Test and Counselling)...

Kosa Dogo kwenye Afya linaweza Kugharimy Maisha..

Kwa Mujibu ya Sheria ya usiri na Upimaji wa HIV/AIDS ya mwaka 2008, Kifungu cha 13 kifungu kidogo cha 2 (a) na (b)..

Testing process (Iliyopo kwenye Miongozo ya CITC na PITC) haitakiwi kuwa na error wala kurukwa process zozote..
Screenshot_20240411_121151_Adobe Acrobat.jpg


Kifungu cha 15 kifungu kidogo cha 6,7 na 8cha sheria hiyo Hakiruhusu Kabisa kupima Bila Mpimwaji wa HIV kuwa na Knowledge ya alichofanyiwa na hairuhusiwi kutoa majibu kwa yoyote isipokuwa Mpimwaji labda aamue kushirikisha Ndugu..."Disclosure"

Kifungu cha 16 hakiruhusu Majibu kupewa Mtu mwingine Bila Ridhaa ya Mpimwaji na kufanya hivyo ni kinyume cha sheria..
Screenshot_20240411_121514_Adobe Acrobat.jpg


Maana naamini Ukimpa wewe anaweza akapatwa na Mshtuko na Kushindwa Kujizuia kufanya kitu chochote ambacho kinaweza kupelekea Yeye kupoteza uhai..

Je, wewe unajua kumtuliza Kwenye hizo hali?, Unaweza kutoa ushauri wa kumridhisha ili hali ya wasiwasi upweke na hasira aliyo nayo na denial kushuka?? Mwenyr Uwezo ni daktari ambaye yeye kasomea kufanya hivyo...

KWA KUWA MAJI YAMEMWAGIKA SASA NINI KIFANYIKE?..

Kazi ya ushauri nasaha sio Nyepesi kama udhaniavyo kwamba utamueleza tu mama Yako na yeye ataipokea Hiyo Taarifa kwa furaha..
ni process na ni ngumu sana..maana inadeal na Emotional na how to neutralise Emotional hizo..

Sasa nakushauri Bila woga wala kuonyesha unajua Chochote mwambie mama Kuwa Daktari alikuambia Kuwa atapona hiyo Typhoid ndani ya siku moja ila unaona maendeleo bado mabaya kwa hiyo wewe umeamua Kumpeleka kwa Daktari wa hospitali Nyingine Labda utapata Suluhisho..

Akikubali Mpeleke Hospitali Huko Na toa Taarifa hiyo kwa Daktari mwambie na mwambie uko pale kwa ajili ya yeye Kupima na kuambiwa majibu yake na kupata Ushauri (Ila umwambie Daktari maneno hayo mama yako yeye Akiwa hayupo)..

baada ya kumaliza kazi Hiyo ya kumwambia Daktari atamwita atafata Miongozo yote ya upimaji Ikiwa ni pamoja na Ushauri na kama mama ataamua kukushirikisha majibu atamwambia Daktari..

Na mwambie daktari Asimwambie mama chochite kuhusu Wewe kujua majibu Yake (Itakuwa Relief kwa mama), Kuliko yeye akijua hivyo Mpe time mama Kama anakuamini atakuambia Mwenyewe Majibu yake na hata kukuchagua kuwa Msaidizi wake wa Kimatibabu "Treatment Supporter" TS..
Na akishapatiwa Majibu hakikisha anajiunga CTC kwa ajili ya Huduma ya matibabu na Matunzo..


Shukrani na Pole kwa mzigo kwenye moyo wako

CC: Kanashimi
 
Nilipoona tu mahali umesema mama alikuwa mzuri kupindukia nikajua hapa lazima JITU lenyewe lihusike.
Nikutie moyo sana dunia ya leo ukimwi ni kama mafua tafuta mshauri Mzuri aje aongee na mama amtie moyo washirikishe wadogo zako pia wote kwa pamoja muwe nae karibu kwa hakika atakuwa sawa..
 
Back
Top Bottom