Mozambique = Msumbiji?

Mozambique = Msumbiji?

Hivi hii tafsir ya Mozambique ilitoka wapi na kuwa Msumbiji?

Sasa Kenya itakuwa nini kwa kidhungu?

Au neno Zanzibar ni kiswahili kweli?

Mozambique: Modern day Mozambique, itself a derivative of the name of the Arab Shiekh who ruled the area at the time when the Portuguese arrived, Musa bin Ba'ik.

Zanzibar inasemekana ilianza kukaliwa na watu tangia enzi ya Paleolithic (750,000 to 500,000 years BC).

Lakini ni Wairan (Persian) haswa wa Shiraz ndio waliotoa jina Zangibār: ikimaanisha bār "coast" na Zangi: "bruin" (iron after rust) tafasiri nyingine inasema ni Pwani ya watu Weusi (coast of the black people).

Wengine wanasema jina lilikuwa ni Zingiber.... (derives from the spice ginger) na kujulikana kama spice islands.
 
Moreno=dark skinned,dark haired.
Wareno=wazungu dark.
Au wao walivyotuita watu wa pwani ya mashariki na sisi tukawageuzia kibao.
Egypt=misri(the right way)

Mureno = swarthy = Weusi
 
Granted kuna majina kama Ureno na Portugal ambayo hayana uhusiano (ningependa kujua historia yake, najua ipo).

Lakini utakataa kwamba Marenani na America hamna uhusiano? Ufaransa na France hamna uhusiano? Ujerumani na Germany hamna uhusiano?
ninaposema hakuna uhusiano namaanisha hakuna uhusiano wa kimaana na siyo wa neno. ie. "france" tungeweza kuiita karata na hakuna ambaye angebisha. america "bweha" nk.
 
Wamakonde asilia wanatamka (msambiki) labda ndiyo huko jina la msumbiji lilikotokea!
Moçambique ndio kireno kwahiyo wanalitamka hivyo labda kwasababu ya lafudhi,wewe unasikia "Msambiki"
 
hizi kesi zipo nyingi sana..............mfano mji mkuu wa kuba / cuba ni LA HABANA kama wanavyoandika wao , sisi tumechukua jina la kingereza HAVANA... wakati hili HAVANA CLUB (RON) ni aina ya pombe inayotengenezwa huko Kuba/Cuba.

MOROKO kama tunavyijua ila kwa wao wenyewe waniita MAGHRIB na mji wao wa BAYT L ABYADH ambao hutafsiriwa kama KASABLANKA


haya ni mambo ya kawaida tu katika lugha yoyote ile.
 
Mimi naona ni majina tu na pengine hayana mausiano yoyote lakini bora unaelewa ukiambiwa EGYPT mind yako unajua hii ni misri na vingne mbembe tu
 
Mnapojadili haya mambo ya majina ya nchi, hebu jifurahisheni kidogo kwa hili - je, mnafahmu kuwa maneno yote ya lugha ya Kiswahili yanaishia na aidha A, E, I, O au U yaani vowels tu?
 
Waulizeni wamakonde kwa nini walipindisha neno mpaka likawa msumbiji. Sidhani kama kuna uhitaji wa uchambuzi wa kisayansi kwa hili.
 
Mnapojadili haya mambo ya majina ya nchi, hebu jifurahisheni kidogo kwa hili - je, mnafahmu kuwa maneno yote ya lugha ya Kiswahili yanaishia na aidha A, E, I, O au U yaani vowels tu?

we mkali, nilikuwa sijanote hicho kitu.
 
Wamakonde asilia wanatamka "msambiki" labda ndiyo huko jina la msumbiji lilikotokea!
Kuna mtu mmoja alitokea arabuni anaitwa Mussa Mbiki alifia
Msumbiji na ndio asili hasa ya jina hilo.
 
Tanzania je, imetokana na Lugha gani?.
 
hata asili yeno kiswahili limekosewa kama ilivo bagamoyo na oldivai gorge.
 
Back
Top Bottom