MP yenye maumivu

MP yenye maumivu

dadazuu

Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
46
Reaction score
8
Naomba maaada kwa tatizo alilonalo binti yangu. Anapofika wakati wa MP anaumwa sana kichwa. Anapata homa kali anatapika na wakati mwingine kupoteza fahamu kwa muda. Nilishampeleka Hospital wakamuwekea drip yenye dawa ya kupunguza maumivu na kuzuia kutapika. Wanasema tatizo litaisha polepole ila kiukweli anateseka na ni mwanafunzi . Nahofia kuwa hali hii itamfanya azorote ktk masomo. Msaada wenu nausubiria...
 
Dysmenorhea huwapata wanawake wengi wanapokuwa katika siku zao. Wengine hupata maumivu makali sana kiasi cha kushindwa hata kufanya kazi. Wapo wengine huathirika kisaikolojia kwani siku zinapokaribia huanza kufikiria kuhusu maumivu wanayopataga na kuwafanya wawe kama wamewehuka. Kuna primary dysmenorhea ambayo chanzo chake hakieleweki na secondary dysmenorhea ambayo kuna chanzo kinachosababisha mwanamke kupata maumivu mfano uambukizo kwenye via vya uzazi uvimbe nk. Kama mtu ana secondary dysmenorhea anahitaji kutibiwa chanzo ili tatizo lipungue kama sio kuondoka kabisa. Maandishi yanasema wanawake wengi baada ya kuzaa haya maumivu hupungua. Na ni vizuri akawa anatumia dawa za kupunguza maumivu wakati wa hedhi. Mf mefenamic acid husaidia sana kwa watu hawa.
 
Tatizo km hili analo mpenz wangu,nae aliambiwa hosptali kua akizaa litaisha,anaumia sana kpnd cha mp.

Mpo pole mkuu, kinachotakiwa kujulikana lilimuanza toka anavunja ungo(primary) au limemuanzia njiani(secondary)? Hiyo ya pili inahitaji kufanyiwa evaluation ili kupata chanzo chake ikiwezekana na matibabu ya chanzo. Hope my mupenzi mtarajiwa amu hana hili tatizo, teh,teh!
 
Last edited by a moderator:
Embu jaribu kwa Dr. Mwaka wa Foreplan Clinic, Ilala

Angalizo tu: hawa waganga, drs wanaojitia kudeal na matatizo ya wanawake tu wakati sio gynaecologists wanatu..tombea sana dada zetu na wapenzi wetu. Nimeshapata confessions za kutosha kusema hivi, hasa waganga wa dawa za mitishamba!
 
Lol, no pun intended ila ungemuuliza mumewe wa sasa hivi akakuhakikishia kama ana tatizo ama la lol.
Hope my mupenzi mtarajiwa amu hana hili tatizo, teh,teh!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hlo linaweza kutibika na asipate maumivu tena wengi wamepona kabsa nikiwepo

Tiririka kama great thinker, sasa umeshauri nini hapa. Halafu we unajiuzisha na masuala ya tiba while hata namna ya kutoa ushauri uankushinda embu Acha Ushamba!
 
Last edited by a moderator:
Mpo pole mkuu, kinachotakiwa kujulikana lilimuanza toka anavunja ungo(primary) au limemuanzia njiani(secondary)? Hiyo ya pili inahitaji kufanyiwa evaluation ili kupata chanzo chake ikiwezekana na matibabu ya chanzo. Hope my mupenzi mtarajiwa amu hana hili tatizo, teh,teh!

heheh did she say Yes???nichague colour saizi jaman
 
Last edited by a moderator:
Tatizo km hili analo mpenz wangu,nae aliambiwa hosptali kua akizaa litaisha,anaumia sana kpnd cha mp.

Mke wangu pia ana tatizo hili, lilianza tangu alipovunja ungo na kwa wakati huo wazazi wake walimpeleka hospital akaambiwa litaisha akizaa. Kwa sasa ni mjamzito, natumaini baada ya kujifungua atapata ahuweni.

Pole mkuu, nikikumbuka hayo maumivu wanayoyapata ni hatari hadi nyumbani furaha hutoweka kwa siku kadhaa.
 
Hapo kaka jitahidi tu kumpeleka kwenye hosptal kubwa ufumbuzi utapatikana tu usiofu atapona
 
Mpo pole mkuu, kinachotakiwa kujulikana lilimuanza toka anavunja ungo(primary) au limemuanzia njiani(secondary)? Hiyo ya pili inahitaji kufanyiwa evaluation ili kupata chanzo chake ikiwezekana na matibabu ya chanzo. Hope my mupenzi mtarajiwa

Huyu binti alivunja ungo akiwa na 13 yrs na Tatizo hili la maumivu lilianza akiwa na 15 yrs mkuu
 
Back
Top Bottom