Ukiangalia mpango mzima wa Serikali kuhamia Dodoma mpaka mwaka huu wa 2020 ukiwa unaenda ukingoni kuna taasisi nyingi za Umma bado zinaendesha shughuli zake zikiwa nje ya makao ya serikali wengi wao wakiwa Dar es Salaam wakati mkuu wa nchi tayari yeye alishafuta makazi yake ya Dar es Salaam .
Mtu unaweza kujiuliza je, ni jeuri ya wakuu wa hizo Taasisi za umma mpaka leo kuendelea kuwepo mahari ambapo hata muhimili Bunge umeisha tangaza kuwa makao ya serikali ni Dodoma? au wana maslahi binafsi na taasisi hizo kiasi cha kugomea kuhamia Dodoma?
Ukiangalia katika wizara wakati wanahamia Dodoma baadhi ya wizara zilikaa hata katika mabanda ya mabati mfano wizara ya TAMISEMI, sasa hawa ambao bado wapo Dar es Salaam wanasingizia nini? Kama ni ofisi Dodoma kuna majengo mengi tu ya kuhamia
Rais, Katibu MKUU KIONGOZI waulizeni hao ambao bado wapo nje ya Dodoma wanatafuta nini ? mfano wa taasisi hizo ni kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) , BRELA, WAKALA WA VIPIMO, BARAZA LA MAZINGIRA LA TAIFA, TBS, TRA, kuna baadhi ya Taasisi au Mamlaka zinakuwa Dar es salamm kwa sababu ya nature ya kazi zake mfano Bandari, TAA, TCCIA
Kuna haja ya waziri mkuu au katibu mkuu kiongozi kuwaita watendaji wakuu wa taasisi za Umma na kuwaeleza dhima kuu ya serikali kuhamia Dodoma.