Mpaka leo Serikali bado haijakamilisha kuhamishia Ofisi zake Dodoma (Makao Makuu ya Serikali)

Mpaka leo Serikali bado haijakamilisha kuhamishia Ofisi zake Dodoma (Makao Makuu ya Serikali)

Mleta maada tambua kua TBS wanadhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia kupitia bandari ambazo ni nyingi na pia bidhaa za viwandani ambapo viwanda vingi vipo Dar, hasa hao waende Dodoma Kufanya nini?
Pakiwepo ofisi za kanda kwa hayo maofisi yoote kuna shida? Halafu mimi napenda hao wakurugenzi wote taasisi zoote wahamie Dodoma tu mjini vibaki vi-IST vyetu.
 
TIC lazima iwe Dar kwani Dar ni lango la kuingilia hivo mwekezaji ashuke Uwanja wa ndege aanze kupanga kwenda Dodoma kupata maelezo anayohitaji?
Siku hizi kuna video conference hata akiwa hotelin kwake atapewa maelezo tu.
Nimeona kama balance ya maendeleo inaonekana kwa mji kuhamia Dodoma.
 
Mtoa mada una jambo lako sio bure
Uhamisho ni kichaka tu
 
Hahaha waambie wahame haraka, wakumbushe na mabalozi walihimizwa kuhamia dodoma miaka sita iliyopita bado wanasuasua, akiweza awafukuze ateua na aapishe mabalozi wengine hasa hawa mabeberu tunataka kuwakuwaona dodoma haraka wasitucheleweshe.

Unafikiri kuhamia Dodoma ni kama kuhamia Buza?
 
Ukiangalia mpango mzima wa Serikali kuhamia Dodoma mpaka mwaka huu wa 2020 ukiwa unaenda ukingoni kuna taasisi nyingi za Umma bado zinaendesha shughuli zake zikiwa nje ya makao ya serikali wengi wao wakiwa Dar es Salaam wakati mkuu wa nchi tayari yeye alishafuta makazi yake ya Dar es salaam .

Mtu unaweza kujiuliza je , ni jeuri ya wakuu wa hizo Taasisi za umma mpaka leo kuendelea kuwepo mahari ambapo hata muhimili Bunge umeisha tangaza kuwa makao ya serikali ni Dodoma ? au wana maslahi binafsi na taasisi hizo kiasi cha kugomea kuhamia Dodoma?

Ukiangalia katika wizara wakati wanahamia Dodoma baadhi ya wizara zilikaa hata katika mabanda ya mabati mfano wizara ya TAMISEMI ,sasa hawa ambao bado wapo Dar es Salaam wanasingizia nini ? kama ni ofisi Dodoma kuna majengo mengi tu ya kuhamia .

Rais , Kaibu MKUU KIONGOZI waulizeni hao ambao bado wapo nje ya dodoma wanatafuta nini ? mfano wa taasisi hizo ni kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) , BRELA ,WAKALA WA VIPIMO , BARAZA LA MAZINGIRA LA TAIFA , TBS , TRA , kuna baadhi ya Taasisi au Mamlaka zinakuwa Dar es salamm kwa sababu ya nature ya kazi zake mfano Bandari , TAA , TCCIA .

Kuna haja ya waziri mkuu au katibu mkuu kiongozi kuwaita watendaji wakuu wa taasisi za Umma na kuwaeleza dhima kuu ya serikali kuhamia Dodoma.
ACHA UKUADA WEWE
 
JIWE MUONGO SANA....

TBC TU WAMESHONDWA KUHAMIA DODOMA

wajinga ndio wanaamini selikali imehamia Dodoma.
Ni kweli kabisa mkuu serikali bado iko Dar. Binafsi sijawahi kusafiria Dodoma huduma yoyote ya serikali tangu wahamie huko.
 
Moja ya sifa ambazo watanzania miaka yote watamkumbuka Magufuli ni uamuzi wa kijasiri wa kuhamia Dodoma.
 
Kama uamini serikali imeshahama subiri mwakani zamu ya kufungwa kwa baadhi ya English school za Dar au kushuka kwa Ada.

Wana Dar es Salaam wajiandae zaidi ya trillion shillings+ ya uchumi wao unaamia Dodoma kuna biashara zitaathirika alikadhalika kuna sector za biashara Dodoma zitakuwa kwa kasi.

Kazi kwao wajasariliamali ujanja kuwahi; akili kumkichwa.
Kamwe Dar haitazidiwa mapato na Dodoma

Lagos japo sio mji mkuu imeacha mbali Abuja nchini Nigeria

New York imeiacha mbali Washington.

Mifano Mingi tu
 
mleta mada kwa hiyo unataka na mamlaka ya bandari Tanzania yahamie Dodoma?
Anataka mpaka mkuu wa mkoa wa Dar ahamie Dodoma. Ila sishangai ndo akili za maccm zilivyo
 
mleta mada kwa hiyo unataka na mamlaka ya bandari Tanzania yahamie Dodoma?
Mtoa uzikaelezea vizuri tu hapa .

"kuna baadhi ya Taasisi au Mamlaka zinakuwa Dar es salamm kwa sababu ya nature ya kazi zake mfano Bandari , TAA , TCCIA ."
 
Bado nyingi
NECTA
TEA
TIE
TEWW
TTCL
TFDA
NIMR
e.t.c
Ukiangalia mpango mzima wa Serikali kuhamia Dodoma mpaka mwaka huu wa 2020 ukiwa unaenda ukingoni kuna taasisi nyingi za Umma bado zinaendesha shughuli zake zikiwa nje ya makao ya serikali wengi wao wakiwa Dar es Salaam wakati mkuu wa nchi tayari yeye alishafuta makazi yake ya Dar es salaam .

Mtu unaweza kujiuliza je , ni jeuri ya wakuu wa hizo Taasisi za umma mpaka leo kuendelea kuwepo mahari ambapo hata muhimili Bunge umeisha tangaza kuwa makao ya serikali ni Dodoma ? au wana maslahi binafsi na taasisi hizo kiasi cha kugomea kuhamia Dodoma?

Ukiangalia katika wizara wakati wanahamia Dodoma baadhi ya wizara zilikaa hata katika mabanda ya mabati mfano wizara ya TAMISEMI ,sasa hawa ambao bado wapo Dar es Salaam wanasingizia nini ? kama ni ofisi Dodoma kuna majengo mengi tu ya kuhamia .

Rais , Kaibu MKUU KIONGOZI waulizeni hao ambao bado wapo nje ya dodoma wanatafuta nini ? mfano wa taasisi hizo ni kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) , BRELA ,WAKALA WA VIPIMO , BARAZA LA MAZINGIRA LA TAIFA , TBS , TRA , kuna baadhi ya Taasisi au Mamlaka zinakuwa Dar es salamm kwa sababu ya nature ya kazi zake mfano Bandari , TAA , TCCIA .

Kuna haja ya waziri mkuu au katibu mkuu kiongozi kuwaita watendaji wakuu wa taasisi za Umma na kuwaeleza dhima kuu ya serikali kuhamia Dodoma.
 
Kama umewahi isji dodoma utaelewa. Dodoma badooo na ndo maana sijaona balozi dodoma, mashirika ya kimataifa nk.
Ukiforce sana haooo wanahamia nairobi.
Hakuna nyumba, hoteli zenye hadhi ya wengine. We kama umezoea kufanyia kazi kwenye ofisi za container sio wote.
Hakuna malls, soko chafuuuuuu, inzi na ombaomba ndo usisene.

Hata mahali nadhifu pa kulia chakula kwa standard ni chache mnoooo.
Hata gesti zenye hadhi zipo chache, zingine kwakweli ni bora pakuche tu,

Ila Dodoma patapendeza sana ndani ya miaka 10 ijayo
 
mleta mada kwa hiyo unataka na mamlaka ya bandari Tanzania yahamie Dodoma?
Hujui kutafakari wewe ukishasoma kitu! Hivi huko Lumumba akili huwa mnaweka wapi? Wapi kaandika kwamba hata TPA ihamie Dodoma?
 
Back
Top Bottom