Kuwa na kiongozi ndio operation yenyewe, sasa huyo kiongozi akaeje Dodoma halafu operation zifanyike DSM, Serikali inafanya kazi kwa mfumo wa nyaraka katika hizo nyaraka ndio kunakuwa na maelekezo, maagizo, na shughuli zinazotikiwa kufanyika katika siku, wiki, mwezi na mwaka.Sijaona shida ikiwa operation za bandari zikawa DSM lakini viongozi wakawa DODOMA.
Siku hizi ni mifumo tu sio lazima viongozi woote muwepo hapo hapo.
Kama kila mfanyakazi anafanya kazi kwa niaba ya mkurugenzi mkuu na anafanya kulingana na miongozo iliopo kuna haja ya viongozi waandamizi kuwepo eneo husika?.
Kwanza viongozi wenyewe kila siku wapo kwenye vikao mikoani.
JPM amepiga kambi akisubiri kukabidhiwa IKULU yake mpya hao wasioenda wanasubiri nini?
Acheni mji upumue nendeni DODOMA.
TCCIA inahusika vipi na serikali?Ukiangalia mpango mzima wa Serikali kuhamia Dodoma mpaka mwaka huu wa 2020 ukiwa unaenda ukingoni kuna taasisi nyingi za Umma bado zinaendesha shughuli zake zikiwa nje ya makao ya serikali wengi wao wakiwa Dar es Salaam wakati mkuu wa nchi tayari yeye alishafuta makazi yake ya Dar es salaam .
Mtu unaweza kujiuliza je , ni jeuri ya wakuu wa hizo Taasisi za umma mpaka leo kuendelea kuwepo mahari ambapo hata muhimili Bunge umeisha tangaza kuwa makao ya serikali ni Dodoma ? au wana maslahi binafsi na taasisi hizo kiasi cha kugomea kuhamia Dodoma?
Ukiangalia katika wizara wakati wanahamia Dodoma baadhi ya wizara zilikaa hata katika mabanda ya mabati mfano wizara ya TAMISEMI ,sasa hawa ambao bado wapo Dar es Salaam wanasingizia nini ? kama ni ofisi Dodoma kuna majengo mengi tu ya kuhamia .
Rais , Kaibu MKUU KIONGOZI waulizeni hao ambao bado wapo nje ya dodoma wanatafuta nini ? mfano wa taasisi hizo ni kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) , BRELA ,WAKALA WA VIPIMO , BARAZA LA MAZINGIRA LA TAIFA , TBS , TRA , kuna baadhi ya Taasisi au Mamlaka zinakuwa Dar es salamm kwa sababu ya nature ya kazi zake mfano Bandari , TAA , TCCIA .
Kuna haja ya waziri mkuu au katibu mkuu kiongozi kuwaita watendaji wakuu wa taasisi za Umma na kuwaeleza dhima kuu ya serikali kuhamia Dodoma.
Kama uamini serikali imeshahama subiri mwakani zamu ya kufungwa kwa baadhi ya English school za Dar au kushuka kwa Ada.
Wana Dar es Salaam wajiandae zaidi ya trillion shillings+ ya uchumi wao unaamia Dodoma kuna biashara zitaathirika alikadhalika kuna sector za biashara Dodoma zitakuwa kwa kasi.
Kazi kwao wajasariliamali ujanja kuwahi; akili kumkichwa.
Yoyote ambayo wanafunzi wake 40% wazazi walikuwa wafanyakazi wa serikali, hiyo hela imeamia Dodoma.Shule gani itafungwa DSM?
mleta mada kwa hiyo unataka na mamlaka ya bandari Tanzania yahamie Dodoma?