Mpaka leo Serikali bado haijakamilisha kuhamishia Ofisi zake Dodoma (Makao Makuu ya Serikali)

Kwani huwa wakiwa huko Dar es salaam wanawezaje kusimamia operations za bandari za Tanga, Mtwara, Bagamoyo, Kigoma, Mwanza, Nyasa etc? Kama wanaweza kuzisimamia wakiwa Dar basi waende tu Dodoma hawatoshindwa kuzisimamia wakiwa mbali
 
Sijaona tija yoyote kwa kuhamia Dodoma zaidi ya wizi mkubwa na matumizi mabaya ya mali za serikali. Totally hovyooo
 
Sijaona tija yoyote kwa kuhamia Dodoma zaidi ya wizi mkubwa na matumizi mabayaya mali za serikali. Totally hovyooo
Kusema tu haitoshi , jenga hoja kwa kutumia mifano na kuelezea juu ya uwizi unaosema ..... sio kusema tu kama mlevi
 
TIC lazima iwe Dar kwani Dar ni lango la kuingilia hivo mwekezaji ashuke Uwanja wa ndege aanze kupanga kwenda Dodoma kupata maelezo anayohitaji?
Sio lazima iwe Dar siku hizi asillimia kubwa mifumo inafanya kazi , sasa mwekezaji atawekeza bila kuonana na wizara husika au mamlaka husika ambazo tayari zipo Dodoma ...
 
Sio lazima iwe Dar siku hizi asillimia kubwa mifumo inafanya kazi , sasa mwekezaji atawekeza bila kuonana na wizara husika au mamlaka husika ambazo tayari zipo Dodoma ...
Halafu Dodoma kwa ndege ni pafupi tu kwa mwekezaji mwenye nia
 
Naona hata TRA, waendelee kuwepo Dar, kwa vile Kuna biashara na Taasisi kubwa.
Mtoa uzikaelezea vizuri tu hapa .

"kuna baadhi ya Taasisi au Mamlaka zinakuwa Dar es salamm kwa sababu ya nature ya kazi zake mfano Bandari , TAA , TCCIA ."
 
Duh! Ahahahahah nongwa
 
Nawaangalia Halafu Nasema Hii Bhaghoshaa
😅😄😃🤣😂😁😀
 
Msiwasahau wale LATRA sijui wanafanya nini DSM hadi leo wakati wao wanasimamia barabara!
waziri na Katibu Mkuu Mawasiliano na Ujenzi tunaomba kujua hili.
 
Nafikiri mtoa mada ana inclination za kisiasa badala ya kulitazama kiuchumi. Unaposema Mamlaka ya bandari ihamie Dodoma au viongozi wake wahamie Dodoma simwelewi hata kidogo. Nchi inaendeshwa kisayansi zaidi hasa kipindi hiki cha mtandao, sio lazima uwepo Dodoma ili utekeleze majukumu ya Tasisi yako. Pili kwa kiasi kikubwa Dodoma imeweza kuwa makao makuu ya nchi kwani mhimili yote ipo Dodoma. Taasisi za kiserikali sio lazima ziwe Dodoma ila ziwe pale zinapoweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi kwa kuwafikia wateja wake kwa urahisi zaidi.
 
Reactions: Bob
Kwani huwa wakiwa huko Dar es salaam wanawezaje kusimamia operations za bandari za Tanga, Mtwara, Bagamoyo, Kigoma, Mwanza, Nyasa etc? Kama wanaweza kuzisimamia wakiwa Dar basi waende tu Dodoma hawatoshindwa kuzisimamia wakiwa mbali
LAZIMA WASIMAMIE KUTOKA MAHALI PALIPO NA MOJAWAPO YA CHANZO CHANZO WE BOYA!
HUWEZI KUONDOKA PORT OF DSM HALAFU UKAWE DODOMA NA KUISIMAMIA UKIWA KULE.
 
Watu wanafanya siasa hata kwenye masuala yanayohitaji umakini na utaalamu, kwanza mpaka saa hizi hakuna sababu ya kitaalamu na makini ya kuhamia Dodoma,.zaidi ya Ile Dodoma ni katikati ya nchi.
 
Eti wazazi wao wamehamia Dodoma dah, Jambo usilolijua sawa na usiku wa giza
 
Mleta maada tambua kua TBS wanadhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia kupitia bandari ambazo ni nyingi na pia bidhaa za viwandani ambapo viwanda vingi vipo Dar, hasa hao waende Dodoma Kufanya nini?
Huyo buku Sana Hana uwezo wa kujadili level hiyo, ni kugonga meza na kusema ndioooo
 
Watu wanafanya siasa hata kwenye masuala yanayohitaji umakini na utaalamu, kwanza mpaka saa hizi hakuna sababu ya kitaalamu na makini ya kuhamia Dodoma,.zaidi ya Ile Dodoma ni katikati ya nchi.

Hilo ni swala lingine sasa la kama kuna umuhimu au hakuna, nilikuwa tu najaribu kuelezea kwamba siyo kazi rahisi kuhamisha makao makuu ya nchi na nikatoa mifano ya nchi tajiri ambayo miaka 30 baadaye tangia walipoamua kuhama bado hawajahamisha kila kitu, sasa hoja yako ya kwamba hakuna umuhimu nafikiri imeshachelewa kwani Serikali walishaamua kufanya hivyo na ndio maana hata Mzee Mkapa alijenga Bunge jipya Dodoma, CDA ilianzishwa hivyo kusema kwamba hakuna umuhimu ina maana ulitaka tujenge Bunge lingine Dar badala ya Dodoma, au ? Ulitaka Mihimili mitatu ya Serikali iwe sehemu tofauti tofauti kwa maana tayari Bunge liko Dodoma, ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…