Mpaka lini tutavumilia juu ya Vituko vya Marefa wanaochezesha Ligi Mbalimbali Tanzania?

Magema Jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2020
Posts
1,299
Reaction score
1,197
Sote tumekuwa Mashuhuda wa matukio mbalimbali katika soka yanayofanywa na marefaree wetu hapa Bongo. Imefika mahala mechi zinaharibika kutokana na utashi mdogo wa watu hawa katika kuchezesha soka. Watu hawa muhimu kabisa katika soka ndo wamekuwa vinara wa kutuharibia soka letu.

Ukianza kuchambua ni matukio mengi sana ya ajabu yanayofanywa na waamuzi wa soka kote nchini. Swali ni je,hawana uelewa na sheria za mchezo huu? Je ni wageni katika mchezo huu?

Kwa uchunguzi wa haraka haraka ,nimekuja kugundua kuwa wengi wao wanamahaba na timu flani flani hapa Bongo,ndio maana wakipewa dhamana ya kuendesha michezo inayoambatana na timu zao wanaambulia kuharibu mechi, kwa mbeleko za mbao.

Je, hiyo ni sababu tosha kwako mpenda soka? Je, Unahisi nini chanzo cha uhaini huu katika soka letu?

Nini mchango wako (Tuchukue hatua gani kwa vilaza hawa).

#jr
 
Mi nilishangaa refa aliyewapa penati yanga dhidi ya kmc alipewa onyo badala ya kufungiwa.
Marefa waliotoa penati nje ya box siku yanga na simba na kuwanyima simba penati zaidi ya mbili mpaka leo hawajapewa adhabu kwa mtindo huu marefa wamulikwe
 
si hivyo tu ,hata jana mkuu,hawa marefaree ni too much,kwanini wasichukuliwe hatua stahiki?? Au ni maagizo kutoka juu??
 
Wewe unawaona wanakosea kwasababu kuna matukio unakuja kuyaona yakiwa yamerekodiwa na camera ila kwa uwezo wa kawaida wa macho wakati move ya tukio linafanyika ni ngumu kuyaona ndo maana wenzetu baada yakugundua ilo wakaja na teknolojia kama VAR.Sasa nawewe badala yakulalamika njoo na suluhisho lakudumu lisilohathiri mapungufu ya ubinadamu wa waamuzi.Vinginevyo mnataka kuifanya kazi ya uamuzi wa soka iwe ngumu kisa tu wewe unakuja kukosoa kitu kilichorecodiwa.
 
Sawa,mfano tukio la Morrison kumpiga ngumi Nyoso mechi ya jkt na simba,na penyewe hadi VAR??
 
Hapa wahusika ni TFF hawatoi adhabu kali ambazo zitawatisha waamuzi wenye mahaba na timu

anafungiwa mechi 3 au faini unategemea nn aklafu timu imeondoka na point 3 unategemea nn nadhani hata kama ni mechi kufutwa matokeo itasaidia sana lakini ya haya kuwa makosa ya kibinadamu kila siku mmhhh
 
nafikiri ni mpaka siki mtu afe ndo maamuzi yatatolewa hivihvi mhh
 
anafungiwa mechi 3 au faini unategemea nn aklafu timu imeondoka na point 3 unategemea nn nadhani hata kama ni mechi kufutwa matokeo itasaidia sana lakini ya haya kuwa makosa ya kibinadamu kila siku mmhhh
mechi irudiwe
 
Sote tumekuwa Mashuhuda wa matukio mbalimbali katika soka yanayofanywa na marefaree wetu hapa Bongo. Imefika mahala mechi zinaharibika kutokana na utashi mdogo wa watu hawa katika kuchezesha soka. Watu hawa muhimu kabisa katika soka ndo wamekuwa vinara wa kutuharibia soka letu.

Ukianza kuchambua ni matukio mengi sana ya ajabu yanayofanywa na waamuzi wa soka kote nchini. Swali ni je,hawana uelewa na sheria za mchezo huu? Je ni wageni katika mchezo huu?

Kwa uchunguzi wa haraka haraka ,nimekuja kugundua kuwa wengi wao wanamahaba na timu flani flani hapa Bongo,ndio maana wakipewa dhamana ya kuendesha michezo inayoambatana na timu zao wanaambulia kuharibu mechi, kwa mbeleko za mbao.

Je, hiyo ni sababu tosha kwako mpenda soka? Je, Unahisi nini chanzo cha uhaini huu katika soka letu?

Nini mchango wako (Tuchukue hatua gani kwa vilaza hawa).

#jr
Ukiwalaumu waamuzi peke unakosea.Kifupi sisi watanzania "tumeoza"wengi.
Kuna maeneo mengi mambo hayako sawa.TRA ,Polisi,Bunge,Ikulu,Halmashauri,Mashuleni,Vyuoni,n.k.ni ubatili tupu.Iweje waamuzi wawe tofauti?

Hiyo ni taswira ya jamii tunayoishi na kuitengeneza. Nitajie taasisi hata 1 tu iliyo "smart".
 
1608194831940.png
 
Back
Top Bottom