ni Chama Cha Mapinduzi CCM...
sera zake za kusisimua na kuimarisha uchumi bado zinahitajika na kuaminika zaidi ndani na nje ya nchi, kwani kwa kiasi kikubwa zimebadili hali ya vipato na kuongeza hali za viwango vya maisha ya waTanzania kwa kiwango cha kuridhisha na kutia moyo sana...
sera zake za kuchochea demokrasia usawa, uhuru, haki na uwazi zimefanya siasa kua jukwaa muhimu sana kwa wananchi na wadau wa maendeleo kutoa maoni yanayoongeza uwajibikaji kwa wenye dhamana na mamlaka kwenye jamii...
sera zake kwenye upatikanaji wa huduma za kijamii kwa mfano maji, elimu, afya, miundombinu, mazingira bora ya biashara, uwekezaji, kilimo, ufugaji, usafirishaji, viwanda, ulinzi na usalama, amani na utulivu, vimefanya wananchi na waTanzania kukosa chaguo mbadala wa CCM, na kwa hivyo Imani na matumaini yao yapo katika uongozi madhubuti wa chama cha Mapinduzi...
sera zake za mambo ya nje zimekua rafiki na kivutio cha kipekee sana kwa mataifa ya dunia. ni sera ambazo zinazozingatia sana kwa kiasi kikubwa maslahi mapana ya waTanzania kwanza kiuchumi, kisiasa na kijamii, na zimekua kichocheo kikubwa sana kinachokuza biashara za nje, usafiri wa anga, utalii na uwekezaji nchini..
zaidi sana,
uongozi makini na madhubuti wa chama na serikali ya CCM ndio pekee chama cha kizalendo kinachojitegemea chenyewe, ukilinganisha na vyama vingine ambavyo kwa kiasi kikubwa vinategemea usaidizi wa hali na mali wa mataifa ya ng'ambo..
hayo ni kwa uchache tu, tena kwa lugha rahisi sana kwa sisi sote kuelewa....
hivyo basi,
chaguo pekee la waTanzania katika umoja na mshikamano wao mpaka sasa ni CCM pekee. ndiyo pekee amani na uhakika wa usalama na utulivu wao kiuchumi, kijamii na kisiasa
