Gwajima hafai kuwa kiongozi kwa kipimo cha namna yoyote ile.
Gwajima ndiye aliyehamasisha ukabila akisema kuwa huu ni wakati wa wasukuma, na kwamba kuwe na program ya wasukuma kusaidiana.
Lakini amewahi kutoa kauli za kuubeza uislam. Tanzania ni ya watu wa dini mbalimbali. Lakini sote tunaheshimiana na kila mmoja anaheshimu dini ya mwenzake. Hivi mimi ni nani eti kwa vile ni Mkristo, nimwone Kikwete si chochote kwa sababu siyo wa dini yangu? Yaani nimwone tajiri Bakhresa si chochote kwa sababu yeye siyo wa dini yangu? Hivi kweli tunaamini kuwa Mungu anashindwa kuwaadhibu au kuwaangamiza wasio wake? Kama kila asiye mkristo hafai mbele za Mungu, kwa nini watu hao hao tunaodhani hawafai mbele za Mungu, wakawe na mafanikio mengi katika mengi, na wakati mwingine kutuzidi tunaoamini ni wana wa Mungu kuliko wao?
Hivi kweli unaweza kuamini kuwa Mkristo Magufuli ni mwana wa Mungu zaidi kuliko Kikwete au Mzee Mwinyi? Hivi wakristo na wengine hawajafaidika katika mambo mengi kutokana na juhudi za watu wa dini tofauti na yetu?
Ukitafakari haya yote, ukimsikia mtu anawabagua watu kwa dini zao, makabila yao au maeneo yale wanayotoka au kuishi, unajua kabisa kwamba kuna mahali kichwani na rohoni hakujakaa vizuri. Kauli ya Gwajima juu ya ubaguzi wa dini na kabila haina tofauti na ile kauli ya Rais Maguguli kuwa watu wa Mwanza wasibomolewe nyumba zao kwa sababu ndio waliomchagua (ila wa Kimara Dar, tena kukiwa na order ya mahakama ya kuzuia ubomoaji, wabomolewe tu kwa vile wao siyo watu wa Mwanza)
Uchaguzi huu, tuwakatae kwa kila hali wabaguzi wote, tuwakatae wafanya upendeleo wote, tuwakatae wanaoonea watu, tuwakatae wanaoteka na kuua au kupoteza watu, tuwakatae wanaogawa vyeo kikanda, tuwakatae wanaotaka kudumisha utawala wa hofu na kuphopwa.
Tunamtaka kiongozi wa kuwaunganisha watamzania wote ili kila mmoja afurahie uwepo wake kwenye nchi yake ya Tanzania. Ambapo Mungu alimtaka aishi, afurahie maisha, amtumikie, na mwishowe amrudie.
WABAGUZI NA WENYE KUFANYA UPENDELEO HATUWATAKI, HATUWATAKI KABISA.
Sent using
Jamii Forums mobile app