Uchaguzi 2020 Mpaka sasa Halima Mdee ameshashinda Jimbo la Kawe, Dar-es-Salaam

Uchaguzi 2020 Mpaka sasa Halima Mdee ameshashinda Jimbo la Kawe, Dar-es-Salaam

Salary Slip,

Kwisha habari ya mdee. Hapa hachomiki. Nilivyowaza ndivyo imekua, wangemuacha yule dogo ambaye hata madale hajulokani mdee angepita ila sasa kawekewa chuma cha moto.
 
Atleast wewe umeweka ushabiki pembeni na huo ndiyo ukweli japo na mimi binafisi nimeweka ushabiki huku nilijua Kuna mziki hatari.
Ila Bora Halima mdee gwajima anaropoka mno, nadhani yeye na msukuma hawatofautiani, Ila kwa kawe awe makini sana
 
Jimbo la kawe ukamuhonge nani
Hivi watu wanawaona wakazi wa Kawe ni kama wa Mtera kuwa wanahitaji mtu bungeni wa vijembe na kusifia sifia watu?

Watu wa Kawe wanataka mbunge mtetezi anayeshuka na hoja za msingi zihusuzo maslahi ya Watanzania.

Kawe ni moja ya majimbo yanayoaminika yako katika kitovu cha elimu hivyo hata kama hukusoma lakini unaishi Kawe huwezi kuishi na "Utapeli wa kufufua misukule" na kujitapa Mtu wa Mungu huku unawakung'uta kondoo na kujipiga video. Kiongozi gani huyo wa kumwamini awawakilishe bungeni
 
Unataka kuniambia lile nyomi analojaza kila jumapili hakuna mwenye smartphone pale? Inamaana Hizo clip hawazioni? Hoja mufilisi kabisa hiyo.

Gwajiboy is untouchable.
Ile nyomi ni from the whole of Dar, very few from Kawe
 
Na ndio alikuwa mshenga wa Lowasa Chadema.

Ndio ujuwe huyu jamaa ni taasisi, hili ni pigo kwa Halima, nadhani advantage ya Halima ni mwenyekiti wa Bawacha vyovyote itakavyokuwa ataingia bungeni hata kupitia viti maalum.

..Gwajima ni mtaalamu wa kutoa mapepo, na kufufua "waliokufa."

..hizo siyo taalum zinazohitajika kwa mtu anayewakilisha wananchi BUNGENI.
 
Alipokuwa anasema akiwa kiongozi atazigeuza madrasa kuwa Sunday school alikuwa na maana gani?.
Maneno tu sheikh wangu yale. Hivi unajua kama ndio dhamira yake angeomba ukuu wa Wilaya kwani huyo anamamlaka hadi ya kufunga nyumba za ibada kwa mwavuli wa usalama?
 
 
Unamsema Gwaji boy yupi???

Huyu aliyeanzisha siasa za kikabila za kuhamasisha wasukuma waunde vikundi vya kikabila kumkampenia Magufuli???!!

Huyu anayefanya uzinzi na washarika wake huku akijirekodi???

Labda ashinde Kawe ya Mwanza, sio Kawe hii ya Wasomi na watu wenye fedha wanaojielewa ya Dar es Salaam!!!
Ndio huyo huyo gwajiboy aliyefanya porn na kondoo wake na ni msukuma mkabila. mapema mno halima ajiandae, kuna kaa la moto anakuja kulikalia.
 
..Gwajima is divisive, ni mdini.

..vilevile alishindwa ktk kura za maoni.

..hayo mambo mawili yanawapa ukakasi wapiga kura.
Mkuu nikupe facts chache, kabla hata haijulikani CCM watamsimamisha nani watu wa Kawe hasa vijiwe vya vijana hawamtaki tena Mdee.

Mimi nipo Kawe na nimeshiriki chaguzi zote na sijawahi kumuacha Mdee ila joto la mtaani kwa Mdee si zuri. Kama tupo hapa kupiga propaganda sawa ila Mdee hana cha kuwaambia watu wa Kawe! Unajua amekuwa mbunge kwa muda gani, sasa watu hawataki tena kura za huruma, wanataka kazi!

Tatizo kuu la Mdee ni kutoa hesabu ya kazi zake! Haeleweki yaani! Hauziki!
 
Gwajima haijui siasa, akumbuke huu mpambano aliouingia sio wa kuwaambia wale waumini wake Corona haitafika Tanzania halafu wanamshangilia, ghafla Corona hiyo, anageuka anasema haitanipata mimi then waumini wake wanamshangilia tena! huku ni tofauti, KAWE haitaki story za kijani, regardless of who you are.

Kawe ni ya Mdee, na Mdee ni mtoto wa Kawe, nothing more. Gwajima rudi madhabahuni ukatubu umepotoka.

Gwajima ataaminiwa na nani, mwanzo aliamua kumtumikia Yesu akamkimbia, je, akipewa ubunge akipata dili jingine lenye pesa zaidi hataukimbia?!

Kawe sio ya majaribio, Mdee atosha.
Gwajima atashinda kwa kura nyingi kuwahi kutokea, ndipo mtakapojua hamjui
 
Wafia chama mpo...tuliwaambia mkatubishia!!

Haya mzee kashafika hapo mbebeni....!! Atakayegoma tume ya maadili ina mkono mrefu.

Huyo ndiye msemaji mkuu wetu wakati wa uchaguzi, kumpinga ni kukipinga chama!!
 
Back
Top Bottom