Mpaka sasa najiuliza why she doesn’t care

Mpaka sasa najiuliza why she doesn’t care

Pole sana Mkuu
Ipo ivi mwanzo alikuwa anakujali sana na kukupa kipaombele Yani ulikuwa kama green light kwake kwa Kila jambo ambalo alitegemea kufanya au kukufanyia lakini baada ya kufanya yote ayo bado ukujali Wala kuthamini ivyo akajitaid sana kukuelewesha na kukusamehe ukuweza kutega sikio na kukubari makosa Yako ivyo ikafika wakati ukatengeneza usugu wa kutokujali ndani ya moyo wake ndio maana Kila kitu ukifanya yeye anaona ni sawa tuu ata kama ukikosea au ukipatia mbaya zaidi umebadirika kwenye kipindi ambacho mwenzako ayupo tayari kukupa attention kama zamani lakini sio kama akupendi hapana anakupenda sema tuu ameamua ajiweke pembeni maana alijitoa kama Sargent akiwe mstari wa mbele vitani lkn Amna alicho kipata

Sasa Mimi nakushauri Fanya ivi
1. Una sababu ya kuwa play boy maana utajiumiza mwenyewe tuu na kupata Magonjwa ambayo ya tagharimu maisha Yako

2. Mwanamke huwa anasamehe lkn asahau ivyo anza kumpenda kana kwamba unamuona Leo ukifanya ivyo ndani ya mwezi Kila kitu kitakuwa poa

3. Usiache kumtafuta na kumjulia hali tena ongeza Kasi kama internet ya Star Link

4. Usiwe na mawazo hasi juu yake maana unaweza ukazani anachepuka kumbe mwenzio yupo clean kabisa

5. Kaa nae chini Kisha muombe msamaha kama Kuna sehemu ulimkosea
kwani mnalazimishwa kuandika kiingereza? she don't care is grammatically wrong. it should be she doesn't care. kama hamjui kingereza tumieni lugha mnayoifahamu.
 
Back
Top Bottom