Tangu niijue hii biashara ya forex kupitia Uzi wa Ontario, ni takribani miezi 7. Sikuwahi kusoma wala kupitia mafunzo yoyote Yale. Wala sinaga mentor.
Nilipoona Uzi wa jamaa na nikajua kuna uwezekano wa kupiga hela, nilienda moja kwa moja google kusearch nilichokisoma kutoka jf. Nilikutana na maelezo mengi sana. Nili download plattform na nikaanza kufanya demo. Japo nilikua sijui una place vipi order, lakini kwa kupitia video za YouTube, niliweza kujua. Nilinda na demo kwa takribani wiki mbili, nikaona napoteza muda. Nikaamua kufungua real acc ambayo nilianza nayo kwa kupata hasara. Kadri nilivyokua napata hasara, ndivyo nilivyokua najifunza.
Naweza sema nimejifunza vingi kwa muda huo wa miezi 7 hadi sasa. Nimeshaunguza acc si chini ya 10. Ambazo kwa jumla ni kama $300. Siwezi ongopa, mpaka sasa bado sijaanza kula faida za forex japo naamini baada ya miezi 2 nitakua nimerudisha hela zote kwasababu nimefikia hatua nzuri.
Nilivyojifunza kuhusu forex ni
1. Sio lazima Ku trade kama silielewi soko la wakati huo
2. Nifungue trade nikiwa na uhakika wa ninachokifanya.
3. Nibalance lot size kutokana na kiasi cha mtaji wangu
4. Nisifungue trade zaidi ya 1
5. Nisisahau kuweka SL
6. Nisiwe na tamaa na niweze kucontrol emotion
7. Sio kila pair naweza Ku trade
8. Hiyo loss ya $300, ni gharama ya kujifunza forex
Ahsanteni sana