Mpaka sasa Royal Tour haijaleta manufaa yoyote nchini

Mpaka sasa Royal Tour haijaleta manufaa yoyote nchini

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Tusidanganyike kirahisi wakuu, Kuna watu maarufu sana duniani kama David Beckham na mke wake walisha wahi kuja kula good time hapa nchini na wakazungukia vivutio vyetu miaka ya nyuma.

Pia kuna ma Rais wastaafu wa nchi kubwa kama US wamewahi kuja kula good time na kusepa, wasanii pia wamekuja wengi tu kabla ya Royal Tour.

Pia Kuna watalii toka nchi mbalimbali wamewahi kuja kwa makundi kupitia ndege na wengine toka Israel walikuja kupitia treni ya TAZARA wakianzia South Africa, Zambia na wakaja hapa zaidi ya 300 kwa mara 1.

Kwahiyo hii nchi na vivutio vyake vinajulikana kuliko hata hiyo filamu ya Royal Tour, kwa maoni yangu utalii wetu huchochewa sana na majarida kama Forbes, The Guinness World Records nk.

Ni bora zile pesa wangepewa wamiliki wa majarida hayo yanayo aminiwa na mamilioni ya wanadamu ili waweke vijitangazo katika kurasa zao za mitandaoni hata kwa dakika 15 tu.

Binafsi royal tour naona ni upigaji na namwelekeza CAG afanye special auditing na alete ripoti maramoja kuhusu chanzo cha zile fedha, matumizi yake, hao waliotoa walizipata wapi na wanategemea nini toka kwa steringi wa movie ile.
 
Ungetuletea takwimu za mapato ya fedha za utalii angalau kwa miezi 6 iliyopita alafu uringanishe na miaka iliyopita kwa miezi sita sita ya mwanzoni mwa mwaka ungeonekana ni miongoni mwa Great thinkers.

Bila takwimu utaipa vipi nguvu hoja yako?

Kwavile wewe ndo mleta mada, tuletee na takwimu, Wanaume wa nguvu sisi usituletee maneno matupu.
 
Tusidanganyike kirahisi wakuu, Kuna watu maarufu sana duniani kama David Beckham na mke wake walisha wahi kuja kula good time hapa nchini na wakazungukia vivutio vyetu miaka ya nyuma...
Wewe kama nani umwelekeze CAG afanye special auditing? Hujaweka statistics wageni na mapato miez sita ya nyuma kulinganisha na miaka miwili iliyopita.

CAG hafanyi kaz kwa matamshi. Mpelekee supporting documents, sio maneno
 
Mama alichoka kujitazama kwenye ma taarifa ya Habari Kila siku akaona sio kesi Sasa awe Rambo wa unguja, Basi na ikawa hivo

She was both The Director,actress and Driver,na Bado akitizama Ana furahi Sana 😀 Movie aliyotengeneza mwenyewe
 
Mama alichoka kujitazama kwenye ma taarifa ya Habari Kila siku akaona sio kesi Sasa awe Rambo wa unguja, Basi na ikawa hivo

She was both The Director,actress and Driver,na Bado akitizama Ana furahi Sana 😀 Movie aliyotengeneza mwenyewe
😂😂😂 ila Peter sina imani naye kabisa.
 
Ungetuletea takwimu za mapato ya fedha za utalii angalau kwa miezi 6 iliyopita alafu uringanishe na miaka iliyopita kwa miezi sita sita ya mwanzoni mwa mwaka ungeonekana ni miongoni mwa Great thinkers...
Alichokisema mtoa mada ni kweeli maana royal tour ni ya juzi tuu ila vivutio vya utalii vimekuwepo miaka na miaka ivyo iyo movie sio maarufu kuliko vivutio vyetu wala iyo movie sio kongwe kuliko vivutio vyetu.

Kwa tunaojua sekta ya utalii kwa sasa tupo kwenye high peak ambacho uwa ipo miaka yote kabla hata ya movie, na kwenye high peak wageni uwa ni wengi alafu baadae low season so ayo makelelee ya movie ni mbwembwee na chumvi nyingi ndani yake.
 
Alichokisema mtoa mada ni kweeli maana royal tour ni ya juzi tuu ila vivutio vya utalii vimekuwepo miaka na miaka

Sasa mkuu kuna shida gani ukamsaidia mleta mada kuweka takwimu hapa ilihali wewe upo huko huko jikoni.

Kwanini waafrica tunazidi kujiaibisha kama hatujaelimika.

Mtu akikwambia Mbeya kuna baridi kali kuzidi Mbulu, si unampa Celcius za Mbeya aringanishe na za Mbulu, Simple tu. Maneno mengi ya nini
 
Sasa mkuu kuna shida gani ukamsaidia mleta mada kuweka takwimu hapa ilihali wewe upo huko huko jikoni.

Kwanini waafrica tunazidi kujiaibisha kama hatujaelimika.

Mtu akikwambia Mbeya kuna baridi kali kuzidi Mbulu, si unampa Celcius za Mbeya aringanishe na za Mbulu, Simple tu. Maneno mengi ya nini
Aingie ktk tovuti ya nbs ata ona taarifa ya may ktk sekta ya utalii
 
Mleta mada manufaa yapo maana naona hapa Hyyat Regency Dar es salaam - The Kilimanjaro hotel prado za The royal tour zipo kibao...
 
Back
Top Bottom