Mpaka sasa sijaona mchezaji Kama Ronaldinho (GAUCHO)

Mpaka sasa sijaona mchezaji Kama Ronaldinho (GAUCHO)

Habari Wakuu!

Tokea ninakua mpaka sasa bado sijawahi ona ona mchezaji Mpira anayemfikia GAUCHO kwa ubora.

kwa wanaomjua Gaucho wataungana na Mimi na hawatanishangaa nikimkubali huyu mchezaji ambaye wataalamu tunamuita Mchawi wa Soccer.

Gaucho alikuwa mahiri kwa kuukontroli Mpira. Alikuwa anauwezo wa kuuweka mpira sehemu yoyote ya mwili.

Aidha Mbrazili huyu kwenye swala za dribbling bado hakuna anayemkamata.

Hutotamani mpira uondoke mguuni mwake pindi afanyapo mambo yake.

Gaucho ni miongoni mwa Wachezaji wakali kuwahi kutokea duniani.

Je wewe unadhani ni nani anayemkaribia huyu Mchawi wa Soccer kwa maana kwa wakumzidi bado hayupo.
Kwangu binafsi sidhani kama kuna mchezaji atatokea kama Messi
 
Kwangu binafsi sidhani kama kuna mchezaji atatokea kama Messi

Hakuna na hatatokea mwingine.ni mchezaji wakipekee kuwahi kutokea, yani anasifa nyingi sana tofauti na any players mkuu!
  1. Sio muhuni
  2. Sio shoga
  3. Sio sharobaro
  4. Havai hereni
  5. Anapenda watu hususan teamates
  6. Sio mchoyo wala mbinafsi kila mchezaji anampa assist afunge.
  7. Ni mpole sana na hapendi kuongea ongea
  8. Hajisifu
  9. Ana nidhamu ya hali ya juu tofauti na players wengine
  10. Hapendi ugomvi "Peace man"
  11. Ni mchezaji ambae hana makuu na mtu..
Kwakweli sizani kama kutatokea mwenye sifa nyingi kama za huyu Kiumbe/mchezaji. God bless him!

So wanaomkataa ni baadhi tu ya wabongo,, hivyo wachukulie kawaida tu kiongozi..kuna ambao wanamchukia bila sababu yeyote na wapo ambao wanakiri moyoni kuwa Messi hana mpinzani mpaka now,, hao ndio wanaumia zaidi kusikia jina lake "MESSI" ndiomaana wanatumia kila njia kumfananisha na wakina Diego mara pele mara zidane mara requelme mara gaucho mara di lima mara Dybala. Wote hao kawapiga chini....Inshort wanalo jibu kuwa "MESSI HANA MPINZANI"
 
wengi humu wamezaliwa juzi.

nataka waliowaona hawa wachezaji waje tuzungumze...zidane..stephen efernberg...dinho..
figo ...luis enrique...raul...rivaldo...nedved..batistuta....
Wote hawa nimewaona lakini hakuna aliyemfikia Gaucho. Alikuwa ni master footballing artist. Alikuwa anaweza kuuchezesha mwili wake kisha wapinzani wakampisha akapita. Au kukimbia na mpira ukiwa kifuani kama umebandikwa na gundi. Simply Marvellous.
 
wanaomkataa dino wamezaliwa miaka kumi iliyopita yaani baada ya leo kuanza kuvaa jezi namba 10 mmiliki wa jezi amestaafu
 
Unapoongelea mafaninkio ya ya kazi ni kweli mesi amefanikiwa kushinda gaucho,

lakini kwa upande wa kuutiisha Mpira, ronadinho mpira ulikuwa unamtii bwana, anauambia mpira ufanye anachotaka yeye, ronadino alikuwa anaburudisha bwana
 
Akuna kama Gaucho
 
Hakuna na hatatokea mwingine.ni mchezaji wakipekee kuwahi kutokea, yani anasifa nyingi sana tofauti na any players mkuu!
  1. Sio muhuni
  2. Sio shoga
  3. Sio sharobaro
  4. Havai hereni
  5. Anapenda watu hususan teamates
  6. Sio mchoyo wala mbinafsi kila mchezaji anampa assist afunge.
  7. Ni mpole sana na hapendi kuongea ongea
  8. Hajisifu
  9. Ana nidhamu ya hali ya juu tofauti na players wengine
  10. Hapendi ugomvi "Peace man"
  11. Ni mchezaji ambae hana makuu na mtu..
Kwakweli sizani kama kutatokea mwenye sifa nyingi kama za huyu Kiumbe/mchezaji. God bless him!

So wanaomkataa ni baadhi tu ya wabongo,, hivyo wachukulie kawaida tu kiongozi..kuna ambao wanamchukia bila sababu yeyote na wapo ambao wanakiri moyoni kuwa Messi hana mpinzani mpaka now,, hao ndio wanaumia zaidi kusikia jina lake "MESSI" ndiomaana wanatumia kila njia kumfananisha na wakina Diego mara pele mara zidane mara requelme mara gaucho mara di lima mara Dybala. Wote hao kawapiga chini....Inshort wanalo jibu kuwa "MESSI HANA MPINZANI"
Inamana huyo messi mpira hua anachezea uvunguni!! Yan amejichora mitattoo kama gazeti na mablich kichwan halafu unasema sio sharobaro....mahaba yakizid yanaua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikumbuka mechi ya Barcelona vs Chelsea,alichezesha mwili Terry akaachia upenyo,hapohapo aki score,gaucho ni talented player,hakuwa na magori mengi lkn alikuwa na vitu vingi uwanjani,kuna mech vs Madrid alishangiliwa baada ya kuifunga,hakika jamaa wengine wakasome

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapomsifia mtu ana mbio, msifie na anaemkimbiza.

Messi ni zao la Gaucho ambae nae ni zao la Okocha.

Okocha ndie binadamu/mchezaji ambae alikua very talented, na ni mtu ambae alimpa ma ujanja Mengi sana Gaucho kipindi wakicheza wote pale PSG

Ndio,Gaucho pamoja na kuwa born talented lakini alijifunza mengi sana kwa kaka yake(Okocha) pale Psg, Maana unapozungumzia chenga za maudhi, Kuunasa mpira kama miguu ina sumaku Okocha ndio baba lao
 
Gaucho alipotoka Psg alienda Barca, huko akakutana na mtoto mdogo Messi, pamoja na Messi kuwa born talented lakini alilazimika kujifunza maujanja kutoka kwa Gaucho coz ndie aliekua staa

Hivyo basi tunavyomsifu Messi tukumbuke pia na watu waliorithisha maujanja.

OKOCHA - BABA

GAUCHO -MTOTO

MESSI - MJUKUU.
 
Back
Top Bottom