Mpaka sasa sijaona mchezaji Kama Ronaldinho (GAUCHO)

Huyu jamaa yuko well displined kuna event moja alipewa kadi nyekundu kwa uonevu alichofanya alicheka akatoka nje huku nyuma mashabiki walianza kuzomea mbaya ,na waliporeview mchezo ikathibitika ilikuwa si stahiki yake kutolewa!
 
Acha mahaba mkuu kuna wachezaji wazuri ambao wameweza kumaintain viwango vyao throughout their careers.
Kuna mtu kama Francisco Toti, Iniesta, Zidane etc.
Kwangu mimi Dinho atabaki kama greatest entertainer kwenye soka.
Mkuu hivi Leo FIFA iweke majina kumi ya wachezaji bora kuwahi kutokea duniani huwezi kuamini Ronaldinho anachukua nafasi ya Kwanza.

Hakuna ambaye hajui kiwango cha jamaa.

We angalia hata hapa JF uone jamaa uwezo wake unavyokubalika. Pia wachezaji wengine hufanya mambo ya kawaida ambayo hata mtanzania wa Timu ya Libolo huweza kufanya. Tofauti na Gaucho ambaye hufanya vitu ambavyo wengi sio rahisi kufanya.
 
Na hicho ndicho kinachomfanya watu wamuone bora kuliko wachezaji wengine kuwahi kutokea.

Unajua jamaa anamichezo ambayo mchezaji wa kawaida hata ajifunze miaka mia hawezi kuijua
Hiyo ya kusema ni bora kuliko wachezaji walio wahi kutokea sio sahihi maana kwenye top 5 tu ya wachezaji bora wa muda wote hayupo.
 
Mkuu hapa hatuzungumzii kuangushana uwanjani.

Yaani unamawazo ya kuangushana uwanjani ndio ufananishe hao wachezaji uchwara na Gaucho king of dribbling.

Kazi kweli kweli
 
Sina ushabiki kihivyo wa football ila sitakuja sahau siku ambayo huyu Ronadinho alipofunga goli mpira wa adhabu akiwa almost katikati ya kiwanja !na mm naunga mkono hakuna niliyepata kumuona kama huyu.
Upo vizuri mkuu
 
LIONEL MESSIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.

Fatilieni records na stats afu mrudi hapa. Tuweke hisia pembeni
 
Basi nakushauri uangale video zao.
Kwenye vipengele hizi;
1. Dribbling
2. Ball control
3. Pasi
hapo sasa unafosi nipende unachotaka wewe
pia hizo videos ziko kwa ajili ya biashara kule youtube ubora wa mchezaji unapimwa kwa mechi sio clips
sijakataa kuwa Ronaldinho si mchezaji mzuri don't quote me wrong braza
 
Huyu jamaa yuko well displined kuna event moja alipewa kadi nyekundu kwa uonevu alichofanya alicheka akatoka nje huku nyuma mashabiki walianza kuzomea mbaya ,na waliporeview mchezo ikathibitika ilikuwa si stahiki yake kutolewa!
Jamaa anajua mpira ni sanaa na mchezo wa burudani
 
wengi humu wamezaliwa juzi.

nataka waliowaona hawa wachezaji waje tuzungumze...zidane..stephen efernberg...dinho..
figo ...luis enrique...raul...rivaldo...nedved..batistuta....
Dinho Gaucho ni balaa Zizzou alikuwa mzuri lakini hajamkaribia Gaucho. Labda wale wazee wa Zamani wa Brazil waliocheza na Pelle akina Garrincha.
 
Hiyo ya kusema ni bora kuliko wachezaji walio wahi kutokea sio sahihi maana kwenye top 5 tu ya wachezaji bora wa muda wote hayupo.
Nimekuambia FIFA waitishe kura duniani uone Kama jamaa hachukui.

FIFA hubeba baadhi ya wachezaji wanaobebwa na Media.
 
Mkuu kwanza naomba uniambie team anayechezea kwa sasa mana namtafuta hapa taarifa zake sijazielewa.
 
Kwa kizazi cha karibuni cha wachezaji wenye vionjo uwanjani gaucho ndo kaondoka navyo maana wachezaji wa zama hizi wao nikukimbiza tu.ila hapo nyuma gaucho alitanguliwa na mafundi kama kina maradona,okocha,zidane,rivaldo nedved nawakali wengine we sema miaka iyo mafundi walikua wengi na hakukuwa na mbwembwe nyingi za kupambana kama miaka ya hivi karibuni ndo maana huwez kuwasikia sana au hata taarifa zao zinaonekana za kawaida.Hata hapa bongo miaka ya nyuma ndo kulikua na soka safi,kulikua na kina thomas kipese,madaraka suleiman,zamoyon mogela,edward chumila,nteze john,edibil lunyamila,geo masatu namafundi wengine ila ndo ivyo pamoja na soka lao kubwa bado historia yao inaonekana ya kawaida kwasababu ya zama.Kwaiyo naunga mkono hoja nikizingatia na wakati.
 
Mkuu kwanza naomba uniambie team anayechezea kwa sasa mana namtafuta hapa taarifa zake sijazielewa.
kwa sasa anachezea ile timu iliyopata ajali ya ndege yupo yeye pamoja na Juan Riquelme fundi la kiargentina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…