Mpaka sasa sijaona mchezaji Kama Ronaldinho (GAUCHO)

Nakuunga mkono asilimia buku 1000 si hawa akina Messi wanaobebwa na media.
anajua akina Gaucho, Zadane, Figo, Giggs, Nedved, Dunga na wengine wengi wameweka rekodi nyingi lakini Ronaldo na Messi wamekuja kuzivunja na kuweka zao ambazo kwa kizazi hiki sioni wa kuja kuzivunja halafu unasema wanabebwa na media....!!!
Ronaldinho, Zidane, Ronaldo De Lima kwa uwezo wao wote wamechukua Ballon d'O mbili mbili kila mmoja
Ronaldo CR7 na Messi wamechukua mara9 mfululizo kwa ujumla
don't take them for granted men kazi wanaifanya hao viumbe hata kama unasema wanabebwa hawabebwi kirahisi mtu anamaliza msimu ana goli 75+
 
Eti mashabiki hawajui mpira.

We si ndio unajua mpira.
Ila kaa ukijua Gaucho mpaka kesho atakuwa the best.
 
We unadhani ni vigezo gani vinamfanya mchezaji awe bora kuliko wengine?

Umesahau na suala la Promo, wachezaji wengi hufanyiwa promo na kusapotiwa akiwemo Ronaldo, messi.
Hawa hutumia bidii zao na wala si kipaji cha kuzaliwa
mpira unaangaliaga lakini
 
2004.

We unadhani kwa nini hata hapa JF Watu wengi hufikiri kuwa Gaucho ni mchezaji bora ambaye hana Spare yake.

2004 ni mwaka mzuri sana ambao ulimwengu ulikuwa bado remarkable players wengi, ni mwaka ambao hata ligi ya italia ilikuwa ni bora na ndio imetawala kwenye michuano ya ulaya. Kiufupi tu ni mwaka ambalo soka la ushindani ndio lilikuwa kwenye climax.

Sasa, kwa wachezaji wote waliokuwepo ukimuangalia Dinho, del Piero na Zizzou kuna kipi cha ajabu ambacho dinho alikifanya ambacho hao wengine hatukuwaona wakifanya? kwanzia entertaining hadi kuiweka timu begani pale inapobidi.

Wana JF wengi wanaweza kufikiri hivyo sababu ya vitu viwili either ni mahaba yao yaliopitiliza lakini wanafahamu fika wapo wanaomzidi au hawakupata nafasi ya kuwashuudia wachezaji wengine wanao mzidi dinho zaidi ya kuwaonea youtube.
 
Nakuunga mkono mkuu,huwa inafika muda nakumbuka aina ya mpira wa gaucho
 
Sina cha kukuambia ila utakuwa miongoni mwa wachache ambao utakuwa unaona wapo waliozaidi ya Gaucho.
 
Sina cha kukuambia ila utakuwa miongoni mwa wachache ambao utakuwa unaona wapo waliozaidi ya Gaucho.
Mkuu labda niulize ubora wa mchezaji una angaliwaje?

Kama ni kufunga mabao tu kwa nilowaona mimi sijaona anaemzidi Lionel Messi.

kama ni uwezo wa kudibble pekee Jay Jay okocha ni mwalimu wao na kuna baadhi ya chenga yeye ndio innovator.

Kama ni kuuchezea mpira tu hadi watu wakabaki midomo wazi basi ndio huyo Ronaldinho.

Kama ni uwezo wa kuibeba timu katika mazingira yoyote yale dhidi ya mpinzani yoyote yule basi hapa hakuna zaidi ya Zinadine Yazid Zidane Zizzou.

Sasa inategemea wewe mchezaji bora kwako una mdefine vipi.
 
Umeongea kweli Mkuu.

Lakini huyo Gaucho sio tuu kuuchezea mpira atakavyo pia Kwa Dribbling bado yeye anaongoza Mkuu.

Japo J.J Okocha ni kweli alikuwa vizuri alikuwa vizuri kwenye dribbling lakini suala ya kutumia nguvu hasa mipira ya juu hakuwa mzuri ukilinganisha na Gaucho. Gaucho alipenda mipira ya juu zaidi hasa kifuani kwani alikuwa na kontrol na nguvu/msuli wa kuwazuia maadui
 
We jamaa ndo unajua mpira sasa, sio hao wengine wanakurupuka tu
 
Kwa upande wa kuuchezea mpira atakavyo na madoido hata mimi nakiri kuwa hajatokea mwanaume kama Gaucho.

Ila kama tunaangalia dribbling, mimi sijaona kama Messi na Maradona.

Kwangu mimi mchezaji aliyekamilika na ni best kwa muda wote kwangu ni LIONEL MESSI.
 
Kuna kipindi nilikuwa naangalia AC Milan kwa ajili ya Gaucho tu, baada ya hapo sikutazama tena AC Milan. Gaucho alikuwa ni mtu mwingine ktk kuuchezea mpira vile atakavyo yeye.

Kipindi Gaucho yupo on form utatamani kila pasi imfikie yeye, pasi anavyopiga yeye ni tofauti kabisa na hawa wengine.

Yote kwa yote, tukija kimpira wa kazi sijamuona mnyama kama Messi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…