Mpaka sasa sijaona mchezaji Kama Ronaldinho (GAUCHO)

Mpaka sasa sijaona mchezaji Kama Ronaldinho (GAUCHO)

INAWEZEKANA! Jamaa alikuwa akishika mpira unapenda uendelee kumwona, mbwembe, matumizi ya mwili, chenga, aaaah ukweli hakuna kama Gaucho mpaka sasa.

Mkuu Kama upo na Mimi vile.

Jamaa anambwembwe sana.
Pia anacheza kibrazameni.
 
Gaucho alikuwa ni zawadi ya buridani toka kwa Mungu, alikuwa ni entertiner alikuwa ni zaid ya mwana michezo
Hakukuwa na anaye mfikia kipindi chake Ron
Umenena iliyokweli.

Jamaa anampira wa kuburudisha.
Jamaa hata awe timu pinzani lakini utashangilia akionyesha ujuzi wake.
 
Gaucho alikuwa mtamu sana, ni mcjezaji aliyekuwa akipendwa kuliko wote
Jamaa anaweza kuwa timu pinzani na yako lakini akipata mpira unaweza kumshangilia.

Pia ndiye Mchezaji pekee ambaye anayeweza kumfanya Refa asahau kupuliza vilimbi kwa mbwembwe zake
 
Hakika na sijui lini atazaliwa tena, yule jamaa alikua fundi bana
Mkuu wewe kweli unafuatilia mpira.

Unajua kuna watu huhadithiwa tuu habari za mtu kisha humshabikia bila kujiridhisha.

Nimeangalia Video za Wachezaji mahiri wa ulimwengu lakini bado jamaa anauchezaji wenye ladha ambayo hakuna mwenye nayo
 
wengi humu wamezaliwa juzi.

nataka waliowaona hawa wachezaji waje tuzungumze...zidane..stephen efernberg...dinho..
figo ...luis enrique...raul...rivaldo...nedved..batistuta....
Ni kweli mkuu wengi tumezaliwa miaka ya tisini lakini bado haiondoi ukweli kuwa Gaucho ni mchezaji Bora.

Hao wote nimewafuatilia kwenye you tube lakini bado wameendelea kushika mgongo wa Mr.Cheka(Gaucho)
 
ZIDANE NDIO ALIKUWA MWIBA ZAIDI YA WOTE
Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
ngoja nifanye uchungu kisha nitakuja kukupinga planetbongo.com
mkuu bado unatumia p5 mpaka leo.? aibu
kwani kuna ubaya gani?planetbongo.com
JJ okocha never seen
sio kweli planetbongo.com
Basi nakushauri uangale video zao.
Kwenye vipengele hizi;
1. Dribbling
2. Ball control
3. Pasi
mpira upo kwenye damu yako mkuu planetbongo.com
Mkuu kumbe na wewe wa juz tu
umejuaje kama ni wajuzi?planetbongo.com
 
Mtoto wa juz kwel ww na nilicho gundua huwa unaangalia mech kubwa tuu. Hv kwel wewe unamjua Jay Jay Okocha, Gaucho mwenyewe kwa kinywa chake anakili kujifunza mambo kwa Okocha
Mkuu ingia You tube mwenyewe ujionee. Achana na maneno ya umri hapa hayasaidii.

Okocha ni Mzuri pia kwa style lakini bado atasubiri Sana kwa huyu Mbrazili.

Pia kinachomfanya Gaucho kuwaacha wenzake nyuma ni namna anavyodrible kwa madaha na mbwembwe zake.

Unaambiwa ndie mchezaji ambaye aliweza kupendwa hata na timu pinzani. Anaweza kupata mpira akashangiliwa hata na upinzani.

Hao wengine sikatai wakishika namba 2,3,4+.
Ila moja kwa kweli hapana
 
Mada zake zimeshakua nyingi humu, ifike muda heshima yake ibaki kama ilivyo. Ni dhambi kumfananisha Gaucho, na kiumbe yeyote anaevuta au anaetumia oksijeni ni mmoja kati ya watu bora zaidi kutokea kwenye sayari hii. Nafahamu ni watu wachache ndio wataelewa nilichomaanisha.
 
gaucho alikuwa hatari sana!! control ya mpira hadi kwenye nywele
hakuna kama gaucho kiukwel!
 
Mkuu kama kuna wacheza wastaafu ambao kama kungekuwa na uwezo wa kuwapa uwezo hawa wa kurudi enzi zao za kusakata tena soka basi mimi ningemchagua huyu wa kwanza kurudi katika wachezaji wote duniani waliostaafu. Jamaa alikuwa hana mfano katika uwezo wake wa kuburuza kandanda kwa namna ambayo yeye aliitaka.









Habari Wakuu!

Tokea ninakua mpaka sasa bado sijawahi ona ona mchezaji Mpira anayemfikia GAUCHO kwa ubora.

kwa wanaomjua Gaucho wataungana na Mimi na hawatanishangaa nikimkubali huyu mchezaji ambaye wataalamu tunamuita Mchawi wa Soccer.

Gaucho alikuwa mahiri kwa kuukontroli Mpira. Alikuwa anauwezo wa kuuweka mpira sehemu yoyote ya mwili.

Aidha Mbrazili huyu kwenye swala za dribbling bado hakuna anayemkamata.

Hutotamani mpira uondoke mguuni mwake pindi afanyapo mambo yake.

Gaucho ni miongoni mwa Wachezaji wakali kuwahi kutokea duniani.


Je wewe unadhani ni nani anayemkaribia huyu Mchawi wa Soccer kwa maana kwa wakumzidi bado hayupo.
 
Sisi uku kigoma kuna vipaji zaidi y'a ao mnaowaona kwenye tv fatilieni ndondo za vijijini hakika mtasahau mambo ya LA liga
 
Mada zake zimeshakua nyingi humu, ifike muda heshima yake ibaki kama ilivyo. Ni dhambi kumfananisha Gaucho, na kiumbe yeyote anaevuta au anaetumia oksijeni ni mmoja kati ya watu bora zaidi kutokea kwenye sayari hii. Nafahamu ni watu wachache ndio wataelewa nilichomaanisha.

Umeongea vyema Mkuu.

Jamaa ni hatari Sana.

Mungu alimbariki Sana.
 
Back
Top Bottom