Usitafune maneno, mbona wananchi hawakuandamana alipokamatwa??? jibu hili sualiMkuu kinachoongelewa hapa logically ni kwamba
1.kusingekuwa na sheria Kali za kidini na kimaadili,kusingekua na askari wanaozurura mitaani kwa ajili ya reinforcement
2.kusingekua na hao askari,yule mwanamke asingekamatwa kwa inshu hiyo.
3.na kama asingekamatwa maana yake hill tukio La yeye kufia mikononi mwa polisi lisingetokea na maandamano yasingekuwepo
Kwahiyo hapo tunaona chanzo kabisa ni hizo sheria na ndizo ambazo wadau humu wanazipigia kelele na sio hivyo unavyodhani mkuu
Wananchi wamekuja kuandamana baada ya kufia mikononi mwa polisi, wanadhan kuna jambo lazima limefanyika kusababisha kifo chake.
Nchi ya Iran ipo miaka nenda miaka rudi tokea hujazaliwa wewe wala mimi na babu zako, na sharia zao zipo katika nchi lakini jiulize kwanini hili limetokea sasa? kwaiyo unaona si tatizo la sharia za kiislamu kwa sababu hizo sharia zilikuwepo miaka nenda miaka rudi na hakukua na maandamano.
Suali ni kwanini mwanamke amekufa mikononi mwa polisi? Na ndio mana rais na Serikali ya Iran wanachunguza kifo chake, kama sharia ilimuhukumu kungekuwa na haja gani Serikali kuchunguza kifo chake?
Wananchi wa Iran wanahitaji mabadiliko ya uongozi sasa kwa Rais aliyemadarakani wanahisi ni mzembe kwenye haki za watu na jambo hili linaweza kumtikisa sana.