Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Hii imani ndiyo Ina tufanye tusitangaze idadi ya maambukizi?
Wewe mwenyewe na ukoo wenu hakuna hata mmoja mwenye Dalili za zozote za Covd na tangu ugonjwa huu kuingia umekuwa ripota wa mitandaoni kila siku, hujawahi kuugua na hata kufa, ili Hali wewe unatangaza eti Corona inamaliza watu, Kwa nini Wao na sio wewe, hapo ndipo napoona uwongo wenu

Wakati huohuo unataka watu waendelee kupima, na Wakati Hakuna hata mwenye Dalili hizo Hadi kwenu, mkuu, mbona mnatuombea mabaya tu mkuu
 
Unaona basi? Sasa ungekuwa dereva ungepima kweli ikiwa unaambia kwa 25,000 unapewa cheti bila kupimwa?
 
Kenya wako sahihi,
Tanzania wana pima wapi wagonjwa
 
Hahahaha! You are not serious my brother. Serikali hii inayosema corona imeisha ndio nikaiambie kuna watu wenye corona wanapewa vyeti bila kupima?

Hapo mie ndio nitawekwa ndani.


Labda kama hao wanaotoa vibali ni wajomba zako, taarifa zinatolewa kwa njia nyingi, hata hapa jukwaani unaweza kutoa hiyo taarifa na watu waliopewa ikafanyika msako kwa hao maderva kazi itakuwa imeisha.
 
Kama hakuna anaekufa kwanini watu walizikwa usiku kule Unonio na wazikaji wakiwa wamevaa mavazi mwalimu?
 
Tatizo lipo Tanzania! Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu. Ukute madereva wote kutoka Tanzania wanapewa tu vyeti hata Corona hawapimwi tena kwa sababu Tanzania inaamini kuwa Corona ilishaisha!

Kama tatizo ni hilo jibu lake ni rahisi sana. Wafanyakazi wa Kenya Madaktari, Wafanyakazi wa mahabara, na manesi wakishirikiana na wafanyakazi wa Tanzania katika mahabara za upimaji covid- 19.

Katika cheti kuwe na sahihi ya daktari wa Tanzania na Kenya. Mchezo umekwisha, tatizo liko wapi.
 
Sioni logic kwenye andiko lako.Huwez kujua mtu ana corona bila kupimwa.
Si watanzania wote wana corona. Wapo wanaopita mipakani fresh tu tena wako cleared na vipimo.

Siwez jua uhuru aliongea nn na jpm. Wakaja na resolution kila mtu apimwe kwake apewe cheti.
Kama wanamashaka na vipimo vya tz. Wanaweza alert mamlaka za tz wakaja na mbinu ingine.
Uswahili hapa hautotusaidia..
Sisi tupeleke madkatari wetu mpakani. Ili na wao wakiingia kwetu haijalishi vyeti vyao. Sisi tunapima tu.
Kuwe na check and re-check.. hapa tutaenda sawa.
 
Kwa kusema wagonjwa wamebaki wanne tu Tanzania na sasa tunafungulia kila kitu ni sawa na kusema Corona imeisha. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu na kuthibitishwa na Waziri wa Afya.

Hatuwezi kujua idadi ya wagonjwa au wanaokufa kwa kuwa Tanzania ilsema haitatangaza kwa kuwa inapanikisha watu. Na pia hatuwezi kujua kwa kuwa Tanzania haipimi watu.

Inawezekana kabisa kwamba karibu 50% ya Watanzania wana virusi vya Corona, pamoja na mimi na wewe
 

Yaani maji yametufika shingoni.
 
Hapo umeongea point ndugu yangu!
 
Tanzania hawataki hilo!
 
Hawa Wakenya wanaimani zaidi na ubalozi wa Marekani TZ kuliko taarifa kutoka kwa maabara zetu! Huwezi kumlazimisha mtu kuamini wakati general infos ni shida kutolewa
Na sisi hatuwezi walazimisha waige style yetu. Na sidhan kama wanaiman na ubalozi wa marekani. Wana iman na vipimo vyao... ndio maana wana namba kubwa. Imewapa hofu sana na wako kwenye high alert.
 
Kama ndo hivyo nitapimwa naumwa
 

Attachments

  • VID-20200527-WA0000.mp4
    4 MB
Kama hakuna anaekufa kwanini watu walizikwa usiku kule Unonio na wazikaji wakiwa wamevaa mavazi mwalimu?
Ahaaah, kumbe unaongelea yaliyopita? Ijapokuwa sina uthibitisho wa Hilo mkuu, Basi nimekuelewa mkuu,
 
Sasa hao wanaochukulia serious kupambana na corona wapi wamefika na kupambana kwao, vip USA? Etc na Nchi zingine, hofu inaua kuliko corona, sisi tunajielewe sana kam Tz mpya tunalindwa na Mungu na sio mwandamu au maneno ya jirani,

Huwezi kujenga nyumba kwa kusikiliza meneno ya jirani lazima sisi Tz tujiamrie kama Nchi inayojitawala,

Mh. Dr JPM mbele kwa mbele 2020πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Labda kama hao wanaotoa vibali ni wajomba zako, taarifa zinatolewa kwa njia nyingi, hata hapa jukwaani unaweza kutoa hiyo taarifa na watu waliopewa ikafanyika msako kwa hao maderva kazi itakuwa imeisha.
Mkuu, kama Tanzania haikushughulika na taarifa za waliohusika na kutekwa na kuua watu tulizowapa, unafikiri kwa nini watachukulia taarifa za vyeti kwa uzito? Yaani forgery za vyeti vya Corona ni jambo la muhimu kuliko taarifa juu ya wauaji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…