Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Safi sana, nilikua napata hasira nikijaribu kuamini eti Kenya itaruhusu Watanzania waingie ingie kisa wana vyeti, na walivyo makajanja watafoji vyeti kariokoo na kuingia na corona.

Nchi inayodhamini uhai na afya ya watu wake lazima iwe makini, hata kama italazimu kufungiana mipaka kabisa. Miaka ya 1977 EAC ilivunjwa na kutupwa kule, mipaka ikafungwa na kila mtu akaishi kwake, na wala hakuna aliyekufa.
Kwan si mngetangaza tu kufunga kama sisi tulivyofanya hadharani, mlikwama wapi 🤣 🤣🤣🤣
 
Huu ulaghai wetu unatuharibia. Wahujumu uchumi namba moja ni viongoz wa tanzania hv mnafikiri watu wote ni waapuzi wataamini ulaghai wakat mambo yapo hadharan mmechukulia ugonjwa poa wakat wenzenu wapo sereous
U serious unakuja wapi mkuu,ushaambiwa corona haishi leo wala kesho tutaishi nayo, hii corona ni vita ya kiuchumi, tusipokaa sawa mataifa mengi yatadondoka kiuchumi,Mkuu unaijua TB?
 
U serious unakuja wapi mkuu,ushaambiwa corona haishi leo wala kesho tutaishi nayo,hii corona ni vita ya kiuchumi,tusipokaa sawa mataifa mengi yatadondoka kiuchumi,Mkuu unaijua TB?
Nyie mmechukulia mapambano dhidi ya Corona kienyeji sana, mnawaza pesa zaidi ya uhai wa watu wenu, sasa mmekutana na wanaojali uhai wa watu wao badala ya pesa bado mnapeleka mawazo yenu ya pesa kwa wasiohusika, mnawajibu kwa kuwaza pesa.

Ngoja watanzania wapukutike halafu tuone huo uchumi wenu mnaouimba kila siku utajengwa na nani!.
 
Kuna jamaa hakuingiaga kwenye paper ya namba kwa kujua kwamba akifanya mtihani ataambulia F
 
U serious unakuja wapi mkuu,ushaambiwa corona haishi leo wala kesho tutaishi nayo,hii corona ni vita ya kiuchumi,tusipokaa sawa mataifa mengi yatadondoka kiuchumi,Mkuu unaijua TB?
Hao jamaa ni wajinga sana!

Wanakimbizana kutoa takwimu sijui ili wamfikie USA?

Wanaumia sana kuona tz maisha yanaemdelea huku wao wamejifungia ndani kama mwali
 
Tanzania tunafanya mambo kiajabu sana, na hii yote inasababishwa na kufuata mawazo ya mtu mmoja, haiwezekani mseme vipimo vyenu vilikuwa vibovu baada ya kuvichunguza, halafu baada ya muda mnaanza kulazimisha idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua, mtu mwenye akili atajiuliza imepungua kwa vipimo gani mlivyowapimia?

Hao wakenya ni haki yao kugoma, kwasababu kwanza tulishajifunga wenyewe kwa kukiri vipimo vyetu vilikuwa vibovu, sasa kwanini waamini hivyo vyeti vinavyopelekwa na madereva wetu? waacheni watumie vipimo vyao kuwapima wajiridhishe.

Halafu kwa akili za viongozi wetu watakurupuka nao kuwazuia wakenya, sijui watawazuia kwasababu gani wakati wakenya hawakuwahi kukiri kama vipimo vyao ni vibovu hivyo tusiwaamini madereva wao.
Majibu potofu yanaeleza kisababishwa na vitu vingi ikiwemo aina ya vipimo, reagents, procedures nk. Baada ya Rais kung'amua tatizo aliunda tume na majibu yamewekwa adharani. Ninavyojua tumebadili aina ya vipimo.

Hata hivyo kwa hiyo kwa akili yako Kama tumekubaliana na Kenya kupima madereva, tusipime? Ongea vitu vyenye mantiki! Elezea mbadala ni nini, badala ya kupiga poyoyo.
 
MPAKA wa Namanga upande wa Tanzania umesitisha shughuli zote za kibiashara na nchi jirani ya Kenya kwa muda kutokana na nchi hiyo kutoamini vyeti vya ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya corona vya madereva wa malori wa Tanzania vinavyoonyesha kuwa hawajaambukizwa.
boda.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, ameiambia Nipashe jana kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa Kenya kukiuka makubaliano ya pande hizo mbili, waliyotiliana saini Mei, mwaka huu kwa kuzuia madereva wa Tanzania, kukataa vyeti ili wawaruhusu kuingia Kenya.

“Nadhani wenzetu wana ajenda ya siri kutuhujumu kiuchumi, tumeshakubaliana dereva anapopimwa upande wa Tanzania aruhusiwe upande wa Kenya kwa cheti, sasa wamekiuka makubaliano, wakifika upande ule wanataka wawapime tena sijui wana maana ipi nashindwa kuwaelewa kabisa, tumeamua kuchukua hatua na haturudi nyuma,” alisema.

Katika makubaliano hayo waliamua katika lori itaruhusiwa dereva na wasaidizi wawili kuingia katika nchi husika wote wakiwa wamepimwa kama wana maambukizo ya corona.
Hata hivyo, alisema upande wa Kenya wamebadilika juzi (Jumatatu) kwa kuzuia na kutaka kuwapima tena.

“Pamoja na juhudi za mimi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, kuwasiliana na viongozi wenzetu wa Kenya, lakini zimegonga mwamba na ndipo tukaamua kuzuia vyeti vyote na magari ya mizigo kutoka Kenya pamoja bidhaa zote zinazoingia kutoka nchini humo hadi hapo tutakapokaa tena na kufikia muafaka maana sote tunategemeana, Kenya wanatuhitaji kama soko na sisi wanatuhitaji pia ili kuuza bidhaa,” alisema Mwaisumbe.

Alisema mwezi Mei makubaliano ya kuruhusu kuaminiana pande mbili yalikaliwa kikao na mawaziri wa mambo ya nje za nchi, makatibu wakuu, wataalamu na viongozi wengine wa mikoa na wilaya wa kutoka nchi mbili katika mpaka wa Namanga, kufuatia mazungumzo ya Rais John Magufuli na Rais Uhuru Kenyata ambao waliwaagiza viongozi wanaohusika kukaa na kufanya vikao na makubaliano, huku wakichukua tahadhari za ugonjwa huo na kuona namna ya kuendelea na biashara kwa nchi hizo.

Alisema kama hali ya kutoaminiana itaendelea, itawalazimu kutoa uamuzi wa kuigeuza Namanga kuwa bandari kavu na majirani Wakenya watashusha mizigo au bidhaa upande wake na Tanzania kuichukua na pia hata Tanzania itapeleka wa Tanzania ili Kenya waifuate.

“Nchi yetu ni huru inayojitegemea haihitaji kubembeleza nchi nyingine kufanya biashara kwa sababu sisi tunategemeana, haiwezekani mambo ambayo yameagizwa na marais viongozi wa chini hawatekelezi…linaashiria dharau na ajenda ambayo wanadhani ni siri iliyofichika kumbe sisi tunaifahamu, hatutaweza kuivumilia hata kidogo,” alisema.

Alisema, nia ya Rais Magufuli ni kuwasaidia watu wa hali ya chini kwa kuwa uamuzi huo unapofanyika wanao umia ni watu wa chini.

“Nataka nikuhakikishie ndugu kupima kipimo cha Covid-19 sio lelemama kinaumiza sana, sasa haiwezekani siku mbili mtu amechokonolewa pua, halafu anatoka upande wa Tanzania anaenda upande wa Kenya anafanyiwa kitu kile kile, sasa hali hii kwa kweli sio sahihi, tunataka hiyo agenda yao ya siri ijitokeze hadharani tushughulike nayo kuliko kutumia ugonjwa wa Covid-19, sisi hatutakuwa tayari,” alisema Mwaisumbe.

Ujumbe murua tatizo hakuna lugha ya kidipolomasia wala communication skills
 
Sasa si wangesema tu wamefunga mpaka kama Tz alivyofanya,Au waliogopa nn
Hawana haja maana wao walikuwa wanapita na vyeti halali ila nyie mnapita na vyeti vinavyosoma joto la mwili. Kwani mumeambiwa kuwa joto linaunguza nchi?
 
U serious unakuja wapi mkuu,ushaambiwa corona haishi leo wala kesho tutaishi nayo,hii corona ni vita ya kiuchumi,tusipokaa sawa mataifa mengi yatadondoka kiuchumi,Mkuu unaijua TB?
Wachache sana watakuelewa.
Wengi hapa wako kiushabiki, hawafikiri zaidi ya pua zao.
 
Back
Top Bottom