Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Hakuna Mwafrika asiyejua kujifukiza, watu tunajifukiza na kuendelea kupukutika tu, kirusi kikishaingia kwenye damu hata ujifukize kivipi hamna chochote kitakusaidia.
Sa mbona huku kimesanda?😉
 
Mwanzoni ni kama ilikuwa hivyo. Madereva wa Tanzania wakaja juu kwamba karibu 6 katika 10 wanaopimwa wanaambiwa wana Corona. Wakasema hawaamii vipimo vya Kenya, wanaonewa nk, ndio ilaleta mgogoro.

Nadhani unaweza kuelewa kwa nini Kenya wanashituka ikiwa katika madereva 10 wa Tanzania waliokuwa wanawapima walikuta 6 wana Corona, kwa wastani. Leo Tanzania ikiwapima hao madereva wanaonekana karibu wote hawana Corona!
You have a point brother. Una logic nzuri sana.
Mwanzoni tulikiwa hatupimi madereva.
Sasa hiv tunapima.
Instead of kupima ndani ambapo uwezekano wa urasimu ni mkubwa.
Ipelekwe timu mpakani. Iwe inapima nje na ndani.
Kuwe na cheti kimoja ambacho kinaonyesha mtu kapimwa in both check points.
 
Ni Siasa. Next Election Laila Odinga lazima atachukua nchi!
Hakuna politics hapo. Serikal iko concerned since namba za corona cases zimeongezeka.rapidly in short time.
And kwa politics za kiafrika.. africa hii ninayoijua mimi. Raila atangoja sana.
 
Kwa kusema wagonjwa wamebaki wanne tu Tanzania na sasa tunafungulia kila kitu ni sawa na kusema Corona imeisha. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu na kuthibitishwa na Waziri wa Afya.

Hatuwezi kujua idadi ya wagonjwa au wanaokufa kwa kuwa Tanzania ilsema haitatangaza kwa kuwa inapanikisha watu. Na pia hatuwezi kujua kwa kuwa Tanzania haipimi watu.

Inawezekana kabisa kwamba karibu 50% ya Watanzania wana virusi vya Corona, pamoja na mimi na wewe
Tukiacha ushabiki na kutumia akili kidogo tutafika mbali. Kusema wagojwa wamebaki wanne hawajasema ugojwa umeisha sababu kumbuka hatua zilianza kuchukuliwa tukiwa na mgonjwa moja. Na hiyo assumption ya ugonjwa kuisha nimeiona ni yako kumbe hakuna kiongozi aliyesema. Kuhusu kua na wagonjwa wengi kama hakuna madhara makubwa yaletwayo nayo kuna haja gani ya kutoendelea na maisha kwa tahadhari? Inawezekana Mimi na wewe Tukawa na corona kweli lakini kama tunaweza kuendelea na mambo had unaweza bishana hapa lazima maisha yaendelee. Nataka kuona nchi itakayo endelea na lockdown hadi kuisha kwa corona.
 
Wachache sana watakuelewa.
Wengi hapa wako kiushabiki, hawafikiri zaidi ya pua zao.
Tz ni baba lao, Magufuri baba lao, wachache wenye mapenzi na Nchi yetu tunakuelewa, kwa huku kigoma hatujui kama hiyo kitu inayoitwa corona ipo, shughuli hapa town zinaendelea kama kawaida na barakoa hapa nilipo cjavaa aise, Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿 pia Mubariki Magufuri na watanzania wote hawa wale wasio weza kufikiri wanao fikiriwa na mabeberu wabariki pia
 
Sasa hao wanaochukulia serious kupambana na corona wapi wamefika na kupambana kwao, vip USA? Etc na Nchi zingine, hofu inaua kuliko corona, sisi tunajielewe sana kam Tz mpya tunalindwa na Mungu na sio mwandamu au maneno ya jirani,

Mkuu hebu niambie jambo moja kama kweli wewe sio mwendawazimu.

Unaweza kuniambia nyie ambao hamchukulii serious kupambana na Corona mmefikia wapi?

Hao Marekani waliokufa zaidi ya 100,000, unajua wangekufa wangapi kama wasingechukulia serious kupambana na corona? Brazil ambayo haikuchukulia serious, unaonaje kasi yake ya watu kufa? Brazil si ndio hiyo inaelekea kuipiku USA?

Unawezaje kusema hatuna wagonjwa ikiwa hatujapima watu? Wewe hapo ulipo unajuaje kama hauna virus wa Corona?
 
Tukiacha ushabiki na kutumia akili kidogo tutafika mbali. Kusema wagojwa wamebaki wanne hawajasema ugojwa umeisha sababu kumbuka hatua zilianza kuchukuliwa tukiwa na mgonjwa moja. Na hiyo assumption ya ugonjwa kuisha nimeiona ni yako kumbe hakuna kiongozi aliyesema. Kuhusu kua na wagonjwa wengi kama hakuna madhara makubwa yaletwayo nayo kuna haja gani ya kutoendelea na maisha kwa tahadhari? Inawezekana Mimi na wewe Tukawa na corona kweli lakini kama tunaweza kuendelea na mambo had unaweza bishana hapa lazima maisha yaendelee. Nataka kuona nchi itakayo endelea na lockdown hadi kuisha kwa corona.
Mkuu sisi wajuba tumekuelewa pua IQ yako kubwa sana
 
Labda wewe ndio unapaswa kutumia akili. Sio lazima uambiwe kila kitu.

Kama tunaamini ugonjwa haujaisha, kwa nini tuanze kufungua shule, kuruhusu watalii, kuruhusu ligi na kusema watu waendelee na maisha kama kawaida?

Wewe ukiwa sio mwendawazimu utaruhusu yote hayo ukijua bado tuna tatizo la Corona nchini?
 
Kama hakuna anaekufa kwanini watu walizikwa usiku kule Unonio na wazikaji wakiwa wamevaa mavazi mwalimu?

Jana sio leo, kuzikwa usiku juzi sio sababu watu kutokuwa na ugonjwa.
 
Safi sana. Nilikua napata hasira nikijaribu kuamini eti Kenya itaruhusu Watanzania waingie ingie kisa wana vyeti, na walivyo makajanja watafoji vyeti kariokoo na kuingia na corona.

Nchi inayothamini uhai na afya ya watu wake lazima iwe makini, hata kama italazimu kufungiana mipaka kabisa. Miaka ya 1977 EAC ilivunjwa na kutupwa kule, mipaka ikafungwa na kila mtu akaishi kwake, na wala hakuna aliyekufa.
Hahaha,msimamo uko palepale,hakuna mkenya kumpima Mtz,mark my words, kama tuliwashurutisha mwanzoni mkaturembulia,ndio imetoka hivyo, utaendelea kuumia sana kwa sababu tunavyoongea sasa hivi,viongozi wanakuja kumpigia JIWE magoti tena! I insist,hakuna mkenya kumpima MTZ,over.
 
Mbona New Zealand walipotangaza kuwa wamefanikiwa kutokuwa na wagonjwa wapya na pamoja na waliopo wamepona wote dunia haikutilia mashaka?

Kitu kikifanyika Africa basi media zitaanza kuwaandama.

Hebu tuwe tunatumia akili, tunaona nchi zenye lockdown watu wanavokufa (kwa mujibu wao), watu 200-1000 kwa siku wanakufa. Sisi tuliokuwa hatuna lockdown na kusongamana kila sehemu, tungekufa wangapi kwa siku? Mimi nipo Zanzibar, katika sehemu moja duniani ambayo watu hawajali basi Zanzibar imo, na hatusikii vifo vya idadi kubwa kama kwa wenzetu, WHY?
 
Sioni logic kwenye andiko lako.Huwez kujua mtu ana corona bila kupimwa.
Si watanzania wote wana corona. Wapo wanaopita mipakani fresh tu tena wako cleared na vipimo.

Siwez jua uhuru aliongea nn na jpm. Wakaja na resolution kila mtu apimwe kwake apewe cheti.
Kama wanamashaka na vipimo vya tz. Wanaweza alert mamlaka za tz wakaja na mbinu ingine.
Uswahili hapa hautotusaidia..
Sisi tupeleke madkatari wetu mpakani. Ili na wao wakiingia kwetu haijalishi vyeti vyao. Sisi tunapima tu.
Kuwe na check and re-check.. hapa tutaenda sawa.
😁😁😁
 
Attachments

  • VID-20200527-WA0000.mp4
    4 MB
Kigeu geu... amenigeukiaaa...kigeu geu!

This time tuchore mstari chini.
 
Labda wewe ndio unapaswa kutumia akili. Sio lazima uambiwe kila kitu.

Kama tunaamini ugonjwa haujaisha, kwa nini tuanze kufungua shule, kuruhusu watalii, kuruhusu ligi na kusema watu waendelee na maisha kama kawaida?

Wewe ukiwa sio mwendawazimu utaruhusu yote hayo ukijua bado tuna tatizo la Corona nchini?
[emoji3][emoji3]Mkuu una kichwa kigumu kweli... Tumeambiwa ugojwa umepungua kama unategemea ugonjwa huu kuisha endelea kusubiri . Kama umepungua lazima maisha yaendelee kwa tahadhari sio kama kawaida mbona kiswahili chepesi sana hiki au MKENYA wewe?
 
Mbona New Zealand walipotangaza kuwa wamefanikiwa kutokuwa na wagonjwa wapya na pamoja na waliopo wamepona wote dunia haikutilia mashaka?

Kitu kikifanyika Africa basi media zitaanza kuwaandama.

Mkuu New Zealand hawakutangaza hivyo baada ya maombi. Ni kwamba wanapima watu wao kwa kiwango cha juu, barabarani, majumbani nk. Wakipima watu 100 wakakuta labda ni mmoja tu au 0 katika waliowapima hawana Corona basi wana haki ya kutangaza Corona imeisha na dunia ikawaamini.

Sasa je, sisi Tanzania tulitangaza Corona imeisha baada ya kufanya kama walivyofanya New Zealand?

Kwa nini hata unashangaa kuaminika wa New Zealand iliyopima watu wake na kutoaminika kwa Tanzania iliyofanya maombi?

Kama unataka tuamini Tanzania Corona imeisha, waambie watu wa Maabara wapime watu angalau 50 kila siku kwa wiki moja Soko Kuu Kariakoo, Manzenze, Temeke Yombo, Arusha mjini, Dodoma mjini, Mbeya mjini na Mwanza.

Kisha watutangazie matokeo ndio tutajua Corona imeisha au la.

Kama katika kila 50 tutakaowapima tukikuta ni watu 10 wana Corona, basi mie nitaunga mkono Tanzania tutangaze Corona imeisha
 
Back
Top Bottom