Tanzania tunafanya mambo kiajabu sana, na hii yote inasababishwa na kufuata mawazo ya mtu mmoja, haiwezekani mseme vipimo vyenu vilikuwa vibovu baada ya kuvichunguza, halafu baada ya muda mnaanza kulazimisha idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua, mtu mwenye akili atajiuliza imepungua kwa vipimo gani mlivyowapimia?
Hao wakenya ni haki yao kugoma, kwasababu kwanza tulishajifunga wenyewe kwa kukiri vipimo vyetu vilikuwa vibovu, sasa kwanini waamini hivyo vyeti vinavyopelekwa na madereva wetu? waacheni watumie vipimo vyao kuwapima wajiridhishe.
Halafu kwa akili za viongozi wetu watakurupuka nao kuwazuia wakenya, sijui watawazuia kwasababu gani wakati wakenya hawakuwahi kukiri kama vipimo vyao ni vibovu hivyo tusiwaamini madereva wao.
Badala ya kufunga mpaka, kwanini na sisi tusiwapime Wakenya wanaoingia?