Kumekuwepo na ubishi mkubwa kati ya haya mabasi KIDIA ONE EXPRESS , EXTRA LUXURY COACH, BM COACH na Mengine kama wasindikizani. Ubishi wenyewe umejikita hasa katika ni BASI GANI LINAKIMBIA SANA..?
Binafsi nimeisha safiri nayo KIDIA ONE, BM na leo hii namalizia na EXTRA LUXURY COACH.
Hapa seafari imeanza saa 11:55 alfajiri tukiwa tumetanguliwa na mabasi karibu yote yanayoanzia safari zao nje ya stand ya DAR EXPRESS kwa wanao pajua Arusha. Kufika 12:25 tuko KIA EXTRA LUXURY COACH ikiwa umeisha zipita gari zote. Gari inakimbia hatari sana inaendeshwa na chalii kamoja kayankii fulani ni noma sana.
Wacha nisubiri nione DSM nitatoboa saa ngapi kwa KIDIA ONE nilifika saa 10:15 kwa BM nilifika saa 10:50 kwa EXTRA LUXURY COACH nitaleta mrejesho jioni ila usisahau kunijulia hali maana wenda nikapitiliza mbinguni maana si kwa speed/mbio hizi za Extra Luxury ni NOMA MNO.
LOVE YOU ALL JF CHIT-CHAT[emoji589][emoji589][emoji589]