Mpambano wa mabasi ya Arusha to Dar

Mpambano wa mabasi ya Arusha to Dar

bigmind

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Posts
12,457
Reaction score
12,689
Kumekuwepo na ubishi mkubwa kati ya haya mabasi KIDIA ONE EXPRESS , EXTRA LUXURY COACH, BM COACH na Mengine kama wasindikizani. Ubishi wenyewe umejikita hasa katika ni BASI GANI LINAKIMBIA SANA..?

Binafsi nimeisha safiri nayo KIDIA ONE, BM na leo hii namalizia na EXTRA LUXURY COACH.

Hapa seafari imeanza saa 11:55 alfajiri tukiwa tumetanguliwa na mabasi karibu yote yanayoanzia safari zao nje ya stand ya DAR EXPRESS kwa wanao pajua Arusha. Kufika 12:25 tuko KIA EXTRA LUXURY COACH ikiwa umeisha zipita gari zote. Gari inakimbia hatari sana inaendeshwa na chalii kamoja kayankii fulani ni noma sana.

Wacha nisubiri nione DSM nitatoboa saa ngapi kwa KIDIA ONE nilifika saa 10:15 kwa BM nilifika saa 10:50 kwa EXTRA LUXURY COACH nitaleta mrejesho jioni ila usisahau kunijulia hali maana wenda nikapitiliza mbinguni maana si kwa speed/mbio hizi za Extra Luxury ni NOMA MNO.

LOVE YOU ALL JF CHIT-CHAT[emoji589][emoji589][emoji589]
 
Tafadhali kuna ile hoteli pale juu ya stendi ya tanga ambapo mabasi husimama wale chakula....Hivi ni sifa au makusudiiiii
Kitumbua wanauza buku, sambusha wanauza 2000. Wali 8000 hizi bei sumatra hawazioni au vipi...
 
Unasema nini mpk hapa bado tumeshika kujiti kidia wakiingia sisi tunatoka.

Tutajie mbabe wako nikwambie tuliko muacha.. [emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa magari ya Kaskazini hao kina Kidia, BM, Ibra Line, Extra ni wasindikizaji tuu! Wababe wa hiyo ruti wanajulikana!
 
Back
Top Bottom