Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Kama unatafuta mtaji nadhani njia hiyo inasaidia, ila wito wangu ni kwamba inabidi vijana tujitajidi sana kutoka kwenye hizi njia za slowlane na tuingie kwenye njia za fastlane ili tuweze kubalance muda wa kuishi pamoja na kuacha alama tuzitakazo kwa hii Dunia.Ni sahihi ishu inakuja utapataje kipato cha ziada,ndio hapo pa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili upate mtaji
Njia nyingine unaweza kwenda na lunch box yako kibaruani kwako,watu kama hawa wapo ila huwa tunawaona ni wabahili sana,hivi karibuni nilibahatika kukaa na wabena fulani hivi,wakaniambia hawa jamaa kabila la Vunja bei ni kawaida kwao kwenda na lunch box katika shughuli zao (wakinga) na wana hela chafu
Kuna wakinga fukani nilishawahi kuishi nao utotoni ni family friend,hawa ugali unakaa hata siku tatu katika friji na unalika
Ubahiri ni jambo zuri kama utakuwa unafanya ubahiri kwaajiri ya kusave pesa ambayo unauhakika nayo baada ya muda fulani ambao unapimika, kwa maana huwezi kuweka ubahiri kwenye malengo yatakayotimia baada ya miaka 40 mbele ilihali wewe tayari uko kwenye third floor.
Lakini malengo ya miaka mitano, minne au hata saba sio mbaya as long as uko na uhakika kwamba baada ya huo ubahiri kuisha utaenda kuishi yale maisha ambayo umekua ukiyaota Kila siku angalau hata kwa asilimia 75.