Mpangaji anahesabika ni mvamizi mara tu kodi yake inapoisha

Mpangaji anahesabika ni mvamizi mara tu kodi yake inapoisha

Ahsante kwa mada nzuri mkuu JanguKamaJangu na Mwanasheria Bashir Yakub

Kwenye mada umeeleza suala la notisi ya kuondoka,
"Kuhusu notisi ya kuondoka, mpangaji ambaye kodi yake imeisha hapewi notisi isipokuwa kama mkataba wake unasema hivyo."

Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 inasema tofauti na kilichoelezwa hapo juu

Kisheria, in absence of an express term in the contract, the law has provided implied terms which binds
the parties and applies in the same way as express terms.


Kifungu Na. 88 (2) (b) kinasema kuwa,

"There shall be implied In every lease covenants by the lessor with the lessee empowering the lessor to terminate the lease by serving a notice of intention to terminate the lease on the lessee where any rent is unpaid for one month after the due date for payment whether or not a demand in writing for payment has been made by lessor or an agent of the lessor."

Hivyo, inamaanisha kuwa hata kama mkataba usipoeleza suala la kupewa notisi, bado kupewa notisi ni "implied term" (ni lazima notisi itolewe)

Nimeambatanisha na Kesi ya Rufaa Na. 153 ya mwaka 2018 kati ya Abraham Migeto (Appelant) vs Issa Rajabu (Respondent)

Kesi hii iliamuliwa mwaka 2020 na Jaji M. P. Opiyo kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania (Land Division)

Nawasilisha
 
Mimi navyojua ni kwamba mkataba wowote ni conset ridhaa baina ya watu parties zinazoingia mkataba any renewal of contract ni subjected to consensus ya hizo parties mbili sasa je mpangaji kama kodi imeisha alafu hajaingia makubaliano mengine kwanza huyo kashatokà kwenye status ya upangaji kwakua consideration ya kitu kwa huduma haipo kwaiyo parties zote zitoe ridhaa kumpa mwezi mmoja wakati ridhaa ya mwenye nyumba na mpangaji huo ni upungufu mkubwa wa kisheria
 
  • Thanks
Reactions: G4N
pale mpangaji kodi yake inapoisha na akawa hajaondoka katika nyumba ama eneo la pango, basi hadhi yake inabadilika na anakuwa mvamizi(trespasser).
Safi sana. Kuanzia sasa nitawafurusha wapangaji mpk dunia ishangae
 
Tarehe 5/10/2022 majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa kupitia Rufaa Na. 333/2019 kati ya Lawrence Magesa t/a Jopen pharmacy VS Fatuma Omary na Rimina Auction Mart wamesema kuwa pale mpangaji kodi yake inapoisha na akawa hajaondoka katika nyumba ama eneo la pango, basi hadhi yake inabadilika na anakuwa mvamizi(trespasser).

Kwa sheria zetu mvamizi anaweza kuondolewa ndani nyumba/eneo kwa nguvu yeye na mali zake bila hata kuhitaji notisi.

Na akiondolewa kwa nguvu yeye na mali zake hawezi kudai fidia ikiwemo ile ya kwamba nilikuwa na milioni 10 zangu ndani wakati naondolewa zimepotea.

Hukumu hii inasema hawezi kudai kwasababu kuendelea kwake kuwemo ndani wakati kodi yake imeisha ni makosa na hivyo hawezi kuwa mnufaika wa makosa yake mwenyewe(benefit from own wrongs).

Na huu ndio msimamo wa sheria hata kabla ya hukumu hii. Wapangaji wajifunze kuwa wapole kodi zao zinapokuwa zimeisha. Kodi inapoisha unapoteza haki za upangaji.

Kuhusu notisi ya kuondoka, mpangaji ambaye kodi yake imeisha hapewi notisi isipokuwa kama mkataba wake unasema hivyo.

Kama hausemi hivyo basi kodi ikiisha ni kuondoka, ama kuondolewa kwa nguvu, ama kuomba vinginevyo kutoka kwa mwenye nyumba/eneo.

Mahakama ya rufaa ndiyo mahakama kubwa na ya juu kuliko zote Tanzania, na ndiyo inaongea maneno haya.

Mwisho nasisitiza, ile habari ya kuondolewa kwa nguvu ukitegemea utasema milioni 10 yangu iliyokuwa kabatini nayo imepotea sahau. Ni maneno ya mitaani hayo achana nayo yatakupotezea muda.

Huwezi lipwa, kwani tangu kodi yako ilipoisha ulikuwa mvamizi na mvamizi halipwi manufaa na stahiki kama hizo.

Andiko la:
Na Bashir Yakub, WAKILI
+255714047241
Awe na 10M ndani lakini kashindwa kulipa kodi haizidi laki tano.
 
Back
Top Bottom