DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hamna shida hapo
Nyumba ni yako ila biashara inayo endelea humo ndani si yako
 
Tumia akili hiyo hiyo uliyotumia katika kutafuta kiwanja na kujenga nyumba.
Naomba mwenye mawasiliano na Viwanda vinavyotengeneza Konyagi,K Vant na hizi Pombe Kali za chupa anisaidie tafadhali Ili niwajulishe tushauriane cha kufanya

Nitashukuru sana wapendwa,siku njema
 
Amekiuka mkataba wa upangaji, mpe notice..
 
Sasa unataka kuharibu mchongo mpigie mpangaji mwambia ahame sababu anafanya nyumba kiwanda ....kazi kwisha mambo ya kuingilia michongo ya watu kama hao ndo mwisho wa siku mnapotea sababu ya umbea tu
 
Umesema upo Dodoma. Nenda FCC.. Fair Competition Commission ipo hapo jengo la PSSSF Makole ghorofa ya 6 hiyo ndio kazi yao Kudhibiti bidhaa bandia.
Wao watawasiliana na waliopo DSM watajua cha kufanya ila wewe utakuwa safe incase of anything.
Usipeleke taarifa polisi watakuzunguka na hata kukuharibia au kuhatarisha maisha ndio maana wanashirikiana na hao wahalifu.
 
Mkuu Nenda moja kwa moja ona na na rpc muliro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…