DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ningekuwa mimi, ningemtafuta mpangaji wangu kistaarabu nimwambie kuwa ahame kwani anachokifanya ni kinyume na makubaliano ya mkataba wetu ili sote tusije kuingia ktk matatizo, suala la kumripoti wakati polisi wanajua kinachoendelea kinaweza kkukuweka hatarini zaidi anaweza hata akaichoma moto usiku,na namwambia kuwa akiendelea kukaidi nitachukua hatua zaidi ili kujiwka salama!
 
Mimi huwa nashangaa mtu anatafuta msadda halafu anaficha taarifa. Weka eneo ilipo nyumba mtaa na namba ya nyumba labda utuambie mmeshindwana kwenye biashara yenu ndiyo unamchoma. Kama unahitaji msaada kweli toa taarifa iliyo kamili
 
Daah baba mwenye nyumba asiione hii taarifa 🤣🤣 mimi mwenyewe nna store ya nafaka sometime huwa nashusha mzigo haitoshei maana ni ndogo kwa hiyo baadhi ya magunia huwa nayahamishia nyumbani huko huko nayapanga !! Mpaka mzigo upungue store !!
 
Kuwa makini na unachotaka kufanya,kumreport polisi utakuwa umeharibu maisha yake na kucheza na maisha ya mtu ni kujiweka katika hatari ww na family yako.Kama Kuna uwezekano mtafutemwenyewe muongee nae kwanza
 
Jamani tumieni mitandao kwa uangalifu. Umejiexpose sana mwanadada. Yaani kwa taarifa hii umejiweka hadharani. Hii nchi kwa sasa imechafuka, hao manjagu sio wa kuwaamini. Kwa hali ilivyo unaweza kujikuta ni next Kibao......

Ungeweza kuitoa taarifa hii kwa style nyingine.
 
kuwa makini unaweza kuhatarisha maisha Yako, kama hao manjagu wanaokwenda kuchukua mpunga ndio watakumaliza.
Tafuta mwanasheria akuongoze ukikurupuka umekwisha
Ni kweli. Nyumba ni yake lakini akienda kichwa kichwa hata kuuawa mana watafuta pesa kwa njia haramu kama hizo hawana cha kupoteza.

Huyo mpangaji wako hapitagi huku JamiiForum?
 
Ukikurupuka umeisha watakutaifisha uhai wako mapema sana, nenda kwa hatua soma ushauri humu utakaokufaa pita nao
 
Njia pekee ni kutoa taarifa polisi, TBS, takukuru,TRA na kwa wazalishaji wa pombe husika. Kosa ulikofanya ni kuja mtandaoni na kwa kufanya hivyo utakuwa umempa alert na ataondoa ushahidi wote. By the time vyombo husika vina act hawatapata kitu na utaonekana mzushi na kubakia na uhasama na mpangaji wako.
 
Kwa usalama subiri Kodi iishe ahame Kwa Amani hv unajua hasira za kukatiwa mrija wa pes
Acha uboya ww.

Akae miaka miwili kusubiri Kodi iishe kweli? Kwaiyo kipindi chote IKO akae Kwa mashaka?

Hiyo Ni kesi mbaya mzee, Ni lazma hatua za haraka zichukuliwe.
Iwe Kwa kuongea na mpangaji wake ili ahame, au kutoa taarifa mamlaka zinazohusika.

Ila Kwa vyovyote hapaswi kuogopa wala kusubiri chochote. Unakuta iyo nyumba amejenga Kwa tabu then Iuje itaofishwe na serikali kiboya tu Tena haina ATA mwaka.
 
Sasa angepataje mawazo Kama haya Bila kuja mtandaoni, sababu inaonekana Ni suala linalomuumiza kichwa.
 
Boya mwenyewe ulikuwa na ulazima wa kunijb kwani ww ndo mtoa mada tafuta wa kukukuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…