kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,318
- 4,105
Ww una vinasaba na Musiba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yuko kwa Bashite huyu!we wala hauko Marekani, hongera kwa porojo
Na passport yake imeshikiliwa na Polisi. Huyu jamaa mtoa habari ajiongeze hapa kachemshaMbowe anatakiwa kuripoti mahakamani kila alhamis na hatakiwi kutoka nje ya mkoa bila kibali maalumu so huko Marekani ameendaje?
muulize kama spika wa china alitibiwa india miezi miwili,akikujibu nitaarifu.Ukilifikiria deni la matibabu ya nje lilivyokuwa na kutoonekana kwa trillion 1.5 basi hii thread haina mashiko kuwepo hapa kwa mifano ya kuiga uchina kama nao walipitia vipind hivyo.
Mkuu umechemsha ile mbaya. Hujui kwamba passport yake iko polisi na hatakiwi kutoka nje ya nchi bila kibali cha mahakama na kila Alhamis anatakiwa kuripoti polisi? Pole sana ukitaka kudangaya pia uwe na kumbukumbu*MPANGO MCHAFU WA MANGE KIMAMBI NA FREEMAN MBOWE WAVUJA!!!!!!!!*
• Wakutana Marekani kujadili mipango ya kuivuruga Tanzania
• Watanzania waishio Marekani watahadharisha.
Na Julius Bernard, Maryland USA.
Imethibitika, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ametua nchini Marekani na kufanya kikao cha siri na Mange Kimambi, Mwanadada anayetumia mitandao ya kijamii kuhamsisha maandamano haramu na kuishambulia Serikali ya Tanzania.
Mbowe ametua Marekani kutoka Tanzania, pasi kutolewa taarifa yoyote kwenye vyombo vya habari wala mitandao ya kijamii kama ambavyo viongozi wanasiasa wamekuwa wakifanya hasa ndani ya chama chake cha CHADEMA.
Nimemuona Mbowe akiwa na baadhi ya Watanzania wa hapa Marekani wakijadiliana mambo na baadaye akiwa na Mange Kimambi ambaye amekuwa akiunga mkono harakati za kisiasa za CHADEMA zenye mlengo wa kuichafua Serikali, viongozi wa Tanzania hasa Rais John Magufuli na nchi ya Tanzania.
Kwa sasa Mange anahamasisha maandamano haramu anayoyatangaza kuwa yatafanyika tarehe 26 Aprili, 2018 siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ninachokiona dhahiri ni njama halifu za kuichafua Tanzania, Mbowe anafanya mbinu zote hizi kuhakikisha nchi haikaliki na hili ni jambo ambalo Watanzania lazima walielewe.
Mange Kimambi anahamisisha maandamano tarehe 26 Aprili, zimebaki siku tatu kufikia tarehe hii na tayari Mbowe amekimbia Tanzania na kuja huku Marekani ili Watanzania watakaothubutu kuandamana wakutane na mkono wa dola wakati yeye akiwa salama salimini.
Hii ina maana kuwa Freeman Mbowe na Mange Kimambi wamechora mpango huu wa kutaka watu waandamane kiharamu, wakumbane na vyombo vya dola, waumizwe ama wapoteze maisha kama alivyosema yeye mwenyewe wafe kama 100 au 200 ilihali yeye na mhamasishaji wa maandamano Mange Kimambi wapo Marekani wanakula bata.
Watanzania waliopo Marekani ambao wamemshuhudia Mbowe akiwa hapa pamoja na Mange Kimambi katika mipango yao ya kuhamasisha maandamano wanaonya juu ya upuuzi huu, na wanasema watasema kila wanachokifanya hapa Marekani.
Na hii ndio imekuwa janja ya wanasiasa wengi kuhamasisha maandamano na kukimbilia mafichoni pale wanapoona mkono wa dola hautawaacha. Wengi wamekuwa wakijificha majumbani kwao au kusikojulikana ndani ya nchi, lakini safari hii Mbowe kaona akimbilie nchi nyingine.
Tulioko Marekani na tunaofuatilia hali ya nyumbani Tanzania tunajua hakuna cha maandamano wala mikusanyiko itakayofanyika kwa kuhamasishwa na Mange Kimambi, na itakuwa ajabu sana kama vyombo vya dola vitavumilia hata kwa dakika moja jaribio lolote la kuwaacha watu waandamane ama kukusanyika visivyo halali.
Nimalizie kwa kuwatakia heri Watanzania wenzangu wote huko Tanzania mnapoelekea katika maadhimisho ya siku ya Muungano Aprili 26, tuendeleeni kujenga nchi, tushikamane na serikali na Rais Magufuli ambaye ameonesha dhamira ya kweli ya kuitoa nchi katika mkwamo wa uchumi na kujenga uchumi imara, wa kujitegemea, wenye heshima na endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Nchi zote zilizoendelea zilipita katika kipindi hicho na watu kama akina Freeman Mbowe na washirika wake wanaotumiwa na wanyonyaji na mabepari walidhibitiwa kwa nguvu zote na bila kuona haya.
Kasomeni wakati Baba wa Taifa la China Mao Zedong (Mao tse-Tung) aliyeishi kati ya mwaka 1893 na mwaka 1976 alipoamua kuchukua hatua ya kuijenga china, alipata upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa lakini alikomaa nao na China ikapiga hatua kubwa zilizojenga msingi imara uliopelekea China ya leo.
Kwa heri.
Atakuwa ni Musiba huyo ........ anajifanya yuko US!!we wala hauko Marekani, hongera kwa porojo
Hii fake ID ni C Musiba .Hamna hii mijitu mingine IPO Tz inadanganya Marekani
Kiongozi akisafiri sio hadi chama kitangaze kwenyemitandao
Hatuogopi
Peoples Powerr
.we wala hauko Marekani, hongera kwa porojo