Mpango rahisi wa lishe ya kila siku kwa mgonjwa wa Kisukari

Baba Vladmir

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2021
Posts
413
Reaction score
726
Huu ni mpango bora na rahisi wa lishe kwa mgonjwa wa Kisukari( Type 2) ili kusaidia kudhibiti kiwango Cha sukari kwenye damu.

ASUBUHI (SAA 12- 1)
Uji wa dona au ulezi (usitie sukari, tumia maziwa kidogo ya mgando).
Mayai 1-2 ya kuchemsha au maharage kiasi.
Parachichi au kipande kidogo cha ndizi mbichi/ya kuiva vizuri

SAA 4-5 (Kifungua kinywa kidogo)
Karanga chache au njugu
Kikombe cha chai isiyo na sukari (unaweza tumia tangawizi au limao).

MCHANA (Saa 7-8)
Ugali wa dona/mtama au ulezi.
Mboga za majani (sukuma wiki, mchicha, mrenda).
Maharage, samaki wa kuchemsha/kukaangwa bila mafuta mengi.
Parachichi au matunda kama papai, apple n.k. (kidogo)

JIONI (Saa 12-1 usiku)
Supu ya mboga, maharage au ndizi za kuchemsha.
Kipande kidogo cha viazi vitamu au uji wa mtama/ulezi.
Tunda dogo (apple, nanasi kipande).

MAMBO YA KUZINGATIA;
Epuka sukari, soda, juice za viwandani, keki, vitumbua na chipsi.
Usile wanga mwingi kwa mara moja,gawanya kwa siku.
Punguza mafuta, hasa ya kupika mara kwa mara
Kunywa maji ya kutosha lita 2–3 kwa siku.
Fanya mazoezi mepesi kila siku (kama kutembea dakika 30).

Sanjari na lishe hiyo,unaweza kutumia mimea hii ambayo hupatikana kwa urahisi ili kudhibiti kiwango cha sukari mwilini;
1.MLONGE (Moringa)
Majani yake yanasaidia kupunguza kiwango cha sukari. Tumia kama chai au kausha na saga uwe unatumia kijiko 1 cha unga mara mbili kwa siku.

2. Majani ya mpapai
Husaidia kusafisha ini na kuweka kiwango cha sukari sawa.Chemsha majani 3-5 kwenye maji lita 1, kunywa kikombe mara 2 kwa siku.

3. Karafuu na Tangawizi
Husaidia kuongeza ufanisi wa insulin. Tumia kwenye chai au maji ya uvuguvugu.

4. Tikiti maji pori
Ina kemikali za kusaidia kupunguza sukari. Inapatikana kama mboga au unga.

Jambo mhimu ni kuwa,Zingatia ushauri wa daktari kabla ya kuchanganya dawa na mimea na pima sukari mara kwa mara kuona mabadiliko.
 
Mzee wangu Mungu arehemu alikuwa na huo ugonjwa, maisha yake hanywi masanga wala nini ilikuwa soda tuu.
Sasa huo ugonjwa na ratiba zake anazifuata fuata siku anajilipua paap anachukua sprite zake mbili anakaa huko bustanini na glass yake.
Anazinywa vizuri bi mkubwa anakupigia simu mshua wako leo kajichana soda mbili walah.
Ila nilikuwa naona sawa tuu maana hizo diet zinachosha sana aisee. Nae alikuwa analalamika mivyakula inamchosha sana.
 
vipi kuhusu tatizo la shinikizo la juu na chini la damu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…