Mpango wa LATRA kusitisha vibali vya daladala njia ya Mbagala kuingia mjini ili kupisha Mofat pekee ni kwa maslahi ya nani?

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Wadau, tutakumbuka kuwa wiki kadhaa zilizopita kampuni ya Mofat, inayotoa huduma ya usafiri wa Mwendokasi katika njia ya Mbagala, ilieleza mbele ya viongozi wa Serikali kuwa ina takribani mabasi 150 ambayo yamekuwa yameegeshwa kwa muda mrefu bila kutoa huduma.

Awali tulikuwa tukisikia tetesi kuwa kulikuwa na mpango wa kuondoa daladala zinazoingia moja kwa moja mjini kupisha kampuni ya Mofat. Hata hivyo, kutokana na kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mpango huo ulionekana kufifia na badala yake juhudi zikahamia katika kuongeza nauli.

Baada ya uchaguzi, sasa tunaona LATRA wameanza mchakato wa kusitisha vibali vya magari yanayoingia mjini. Sababu inayotolewa ni kwamba huduma hiyo inapaswa kutolewa na mwekezaji ambaye ni Mofat.

Soma Pia: Thread Kiama, Daladala Njia ya Mbagala Kupisha mwendokasi ifikapo July 1 2026

Nini kipo nyuma ya pazia?

Nimeshangazwa kusikia kuwa mwekezaji huyo amedai kwamba kama asingekuwa mzawa, tayari angekuwa amefungua kesi mahakamani dhidi ya Serikali.

Hoja hiyo inaibua maswali mengi. Je, Serikali iliingia makubaliano na mwekezaji huku ikimhakikishia kuondolewa kwa daladala zinazoingia mjini? Je, hatua hizo zilizingatia ushirikishwaji wa wadau na wananchi wanaotumia huduma hizo kila siku?

Tunajiuliza, iwapo mpango huo utatekelezwa, utakuwa kwa maslahi ya nani? Kwa sasa kuna wananchi wanaotoka maeneo ya Twangoma, Mbande na Kisemvule kwa kutumia magari ya moja kwa moja hadi Gerezani. Endapo vibali vya magari hayo vitasitishwa, wananchi hao watalazimika kushuka Mbagala na kupanda mabasi ya Mwendo Kasi ili kufika mjini.

Pia soma ~ Luhaga Mpina: Kwanini Mabasi ya Mwendokasi yanaondolewa kodi wakati Mabasi ya Masafa marefu hayana msamaha?

Hofu ya nauli kuongeza
Hatua hiyo itaongeza gharama za usafiri kwa wananchi kwa kuwalazimisha kulipa nauli zaidi ya moja. Kwa mfano, nauli kutoka Kisemvule hadi Gerezani kwa sasa haizidi shilingi 1,500. Hata hivyo, abiria akilazimika kushuka Mbagala na kupanda Mwendo Kasi, gharama ya safari inaweza kufikia au kuzidi shilingi 2,000. Hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa mpango wa kuongeza nauli za Mwendokasi utatekelezwa, kwani LATRA waliwahi kueleza kuwa nauli ya shilingi 1,000 ilikuwa ni kiwango cha kuanzia.

Wito kwa mamlaka

Natoa wito kwa LATRA kuzingatia maslahi ya umma katika suala hili. Aidha, wito wangu mwingine ni kwa Serikali kuhakikisha kuwa kabla ya kuingia makubaliano yoyote na wawekezaji, kunakuwa na ushirikishwaji wa wadau na wananchi ambao wanaweza kuathiriwa na maamuzi hayo. Hatua hiyo itasaidia kujenga uelewano, kuongeza uwazi na kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
 
Wadau, tutakumbuka kuwa wiki kadhaa zilizopita kampuni ya Mofat, inayotoa huduma ya usafiri wa Mwendokasi katika njia ya Mbagala, ilieleza mbele ya viongozi wa Serikali kuwa ina takribani mabasi 150 ambayo yamekuwa yameegeshwa kwa muda mrefu bila kutoa huduma.

Awali tulikuwa tukisikia tetesi kuwa kulikuwa na mpango wa kuondoa daladala zinazoingia moja kwa moja mjini kupisha kampuni ya Mofat. Hata hivyo, kutokana na kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mpango huo ulionekana kufifia na badala yake juhudi zikahamia katika kuongeza nauli.

Baada ya uchaguzi, sasa tunaona LATRA wameanza mchakato wa kusitisha vibali vya magari yanayoingia mjini. Sababu inayotolewa ni kwamba huduma hiyo inapaswa kutolewa na mwekezaji ambaye ni Mofat.

Soma Pia: Thread Kiama, Daladala Njia ya Mbagala Kupisha mwendokasi ifikapo July 1 2026

Nini kipo nyuma ya pazia?

View attachment 3610141
Nimeshangazwa kusikia kuwa mwekezaji huyo amedai kwamba kama asingekuwa mzawa, tayari angekuwa amefungua kesi mahakamani dhidi ya Serikali.

Hoja hiyo inaibua maswali mengi. Je, Serikali iliingia makubaliano na mwekezaji huku ikimhakikishia kuondolewa kwa daladala zinazoingia mjini? Je, hatua hizo zilizingatia ushirikishwaji wa wadau na wananchi wanaotumia huduma hizo kila siku?

Tunajiuliza, iwapo mpango huo utatekelezwa, utakuwa kwa maslahi ya nani? Kwa sasa kuna wananchi wanaotoka maeneo ya Twangoma, Mbande na Kisemvule kwa kutumia magari ya moja kwa moja hadi Gerezani. Endapo vibali vya magari hayo vitasitishwa, wananchi hao watalazimika kushuka Mbagala na kupanda mabasi ya Mwendo Kasi ili kufika mjini.

Hofu ya nauli kuongeza

Hatua hiyo itaongeza gharama za usafiri kwa wananchi kwa kuwalazimisha kulipa nauli zaidi ya moja. Kwa mfano, nauli kutoka Kisemvule hadi Gerezani kwa sasa haizidi shilingi 1,500. Hata hivyo, abiria akilazimika kushuka Mbagala na kupanda Mwendo Kasi, gharama ya safari inaweza kufikia au kuzidi shilingi 2,000. Hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa mpango wa kuongeza nauli za Mwendokasi utatekelezwa, kwani LATRA waliwahi kueleza kuwa nauli ya shilingi 1,000 ilikuwa ni kiwango cha kuanzia.

Wito kwa mamlaka

Natoa wito kwa LATRA kuzingatia maslahi ya umma katika suala hili. Aidha, wito wangu mwingine ni kwa Serikali kuhakikisha kuwa kabla ya kuingia makubaliano yoyote na wawekezaji, kunakuwa na ushirikishwaji wa wadau na wananchi ambao wanaweza kuathiriwa na maamuzi hayo. Hatua hiyo itasaidia kujenga uelewano, kuongeza uwazi na kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
Hiyo ndiyo inaitwa Monopoly Ukiritimba ambapo ni mbaya sana sokoni ,TANESCO inafanya madudu kwasababu ya hiyo monopoly kwamba tunakata UMEME na hakuna cha kufanya.

Sasa kama unawaacha Mofat watawale kilwa road kwani kila mtu anataka mwendokasi? Wakiacha peke yao watabweteka na pia wanafanya upumbavu sana hao mwendokasi.

Tutapanda bajaji za kushare tu kama kimara ,mambo ya kutegemea usafiri mmoja ni UJINGA.
 
Huyo mwekezaji atakuwa aliambiwa atafanya biashara bila ushindani wowote.

Na lazima mwekezaji atakuwa mwenzao kwenye kundi, wanalindana ili wapate wote faida.
 
Japo mwanachi atongezewa mzigo wa kulipa nauli mara mbili, hasa wale amabo safari haianzii mbagala, ila itasaidia kuondoa foleni za madaladala yanayoshusha na kupakia abiria hivyo hovyo katikati ya barabara bila mpangilio

Suluhisho: BRT phase Phase 7 iwe kwa ajili ya kufanya extensions za BRT zilizopo, ili zienda mbali zaidi. Mfano kwa Mbagala iende hadi huko Msongola, Kisemvule, Kilungule nk.
 
Route zote za Mwendokasi kuanzia Kimara, Mbezi, Morocco daladala ziliondolewa na zitaluja kuondolewa tu. Ukiona kunajengwa mwendokasi jua hicho ni kifo cha daladala
Mwendokasi njia ya Moroco mbona hatujaona kufutwa kwa ruti ya daladala za Kawe, Makumbusho na Tegeta?
Au kwa njia ya Ubungo Kimara mbona hawajaondoa daladala za Makumbusho kupitia Shekilango, Mabibo na Mawasiliano?
 
Daladala ni uchafu mjini... Ziondolewe zote hata sehemu ambazo mwendo Kasi haujafika
Sasa tukae mkao kuona MVUA ya BAJAJI maana BOSS anauza dala dala 1 anashusha bajaji 4 njiani yani hamna tajiri atauza daladala aweke hela bank

hela yote itarudshwa barabarani,nilimwambia mtu siku 1 Hizi bajaji DAR kuna muda zitapgwa marufuku kuonekana MJINI maana kwa namna bajaji zinanunuliwa sasa hivi

miaka mi 5 ijayo sijui itakuaje...Sasa wataangalia dala dala na bajaji kipi ni UCHAFU
 
Daladala ni uchafu mjini... Ziondolewe zote hata sehemu ambazo mwendo Kasi haujafika
Unaweza kuondoa daladala lakini mambo mawili yazingatiwe.
1. Fikisha mwendokasi Mbande, Kisewe, Kitonga mpaka Mvuti.
Fikisha mwendokasi Mwandege mpaka Kisemvule.
Fikisha mwendokasi Kongoe mpaka Toangoma
2. Gari za mwendokasi zitosheleze mahitaji ya abiria maeneo husika.
Kama haya hamuezi yafanya acheni wananchi watumie huduma zilizo zoeleka.
 
Back
Top Bottom