Mpango wa LATRA kusitisha vibali vya daladala njia ya Mbagala kuingia mjini ili kupisha Mofat pekee ni kwa maslahi ya nani?

Mpango wa LATRA kusitisha vibali vya daladala njia ya Mbagala kuingia mjini ili kupisha Mofat pekee ni kwa maslahi ya nani?

Mwendokasi njia ya Moroco mbona hatujaona kufutwa kwa ruti ya daladala za Kawe, Makumbusho na Tegeta?
Au kwa njia ya Ubungo Kimara mbona hawajaondoa daladala za Makumbusho kupitia Shekilango, Mabibo na Mawasiliano?
Kwani Kawe, Makumbusho na Tegeta zimekuwa zikienda?

Njia ya Morocco ungetakiwa utaje route ya Morocco-kimara, Morocco-Gerezani, Morocco-Kivukoni. Hizo ruti zina mwendokasi muda mrefu, je umewahi kuona daladala ikienda hizo route
 
Mbona ruti za mbezi - morocco, mwendokasi ilikuwa inaenda bene bene na daladala zinakuja kuachana studio ambapo mwendokasi inanyosha morocco kama km 1.8 na daladala inapinda mwananyamala hadi makumbusho.

Nafikiri soko lingeamua abiria achague usafiri anaotaka, anayeshindwa kutoa huduma nzuri ajifie kifo cha asili.
 
Tumeingia monopoly economy.Abdul anazidi kujimilikisha biashara nchi nzima.Maana magari ya mofat ni yake
Hii haimhusu Abdul wala Mama yake.
Utaratibu huo upo toka kubuniwa mradi wa BRT.
Umetekelezwa Morogoro road na Kawawa road.
Huko Kilwa road siyo barabara ya kipekee kwamba usiwaguse huo utaratibu.
 
Naongeza hii
 
Hii haimhusu Abdul wala Mama yake.
Utaratibu huo upo toka kubuniwa mradi wa BRT.
Umetekelezwa Morogoro road na Kawawa road.
Huko Kilwa road siyo barabara ya kipekee kwamba usiwaguse huo utaratibu.
Mnaona Raha sana kutuongopea? Huo utaratibu upo morogoro road ipi? Au hunijui Dar?
Daladala za kariakoo mabibo zinapita njia ipi? Daladala za kariakoo mawasiliano zinapita njia ipi?
Wanaotoka magomeni kwenda sinza wanatumia usafiri gani kama sio daladala zinazopita hapo morogoro road?

Daladala za mawasiliano kwenda mbezi zinapita njia ipi?
Morogoro road yote imejaa daladala za Kila aina unazizijua wewe, alafu unasema hakuna daladala.
 
Zilipoanza mwendokasi Kimara Gerezani na Kivukoni walifuta daladala za Kimara-Kivukoni, Kimara-Kariakoo.
Baada ya basi nyingi za UDART-BRT kufa na vurugu za MO29 kuchomwa vituo wakaruhusu gari chache kusaidia ruti hizo.
Zile zipo kwa muda na zitafutwa tena. Mkataba unasema hivyo.
Hizo za Sinza, Mabibo n.k. za njiani bado zilikuwepo.
Mradi ukikamilika nazo zitafutwa zitawekwa feeder buses za mwendokasi mfano wa Muhimbili -Gerezani.
Hivyo Shekilango kutakuwa na feeder za kwenda Sinza-Mwenge au Makumbusho. Ubungo- Mawasiliano n.k.
Mimi siyo mgeni hapa Dar.
Nina Hadi kadi za Mwendokasi zile za zamani za MAX-Malipo.
 
Back
Top Bottom