SoC04 Mpango wa miaka 25 wa kubadilisha Tanzania kutoka nchi maskini zaidi hadi nchi iliyoendelea kwa kuchukua mifano kutoka Korea Kusini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Professor Aaron Jackson

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2024
Posts
224
Reaction score
241
Umoja wa Mataifa unaiweka Tanzania katika kundi la Nchi maskini Zaidi (LDC). Hata hivyo, ikizingatiwa rasilimali nyingi na uwezo mkubwa wa nchi yetu, hadhi hii inaonekana kutofaa. Miaka ya 1950, Korea Kusini ilikuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani ikitegemea sana kilimo na haikuwa na misingi thabiti ya viwanda. Licha ya changamoto hizi, Korea Kusini iliweza kujijenga kutoka chini na kuibuka kama taifa lenye mafanikio. Kama Korea Kusini iliweza, Kwanini Sisi Tushindwe? Sisi pia tunaweza.

Je, Tanzania ifanye nini ili kutoka katika kundi la nchi duni mpaka kuwa nchi iliyoendelea?
Kwanza kabisa ni uwekezaji katika elimu na rasilimali watu. Kundi la wafanyakazi waliosoma vizuri na wenye ujuzi ni muhimu kwa ukuaji wa viwanda. Tanzania inapaswa kurekebisha mfumo wake wa elimu ufundishwe kwa kiingereza kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu, ili kuongeza ushindani wetu kimataifa. Nikiwa kama mmoja wa wanafunzi wanaotafuta Ufadhili wa kusoma shahada ya uzamili nje, nimegundua kuwa wanafunzi wengi wa kutoka Tanzania tunakosa fursa hizo sababu ya kufeli mitihani ya kiingereza kama IELTS, ukilinganisha na wenzetu Kenya ambao Kingereza kinatumika kama lugha ya kufundishia. Aidha serikali inatakiwa kubuni ufadhili wake “Tanzanian Government Scholarship” ambao utaruhusu wanafunzi wa nchi za nje kuja kusoma nchini. Na wakifika hapa ni lazima wasome Kiswahili(for beginners) kama sehemu ya masomo yao.Hii itasaida sana kuitangaza sio tu elimu yetu bali hata Kiswahili ulimwenguni. Wakati Kiswahili kinapaswa kudumishwa kama lugha ya taifa, kiingereza kinapaswa kuwa lugha ya kufundishia.

Elimu ya sekondari inatakiwa kuhusishwa karibu na viwanda. Wanafunzi wanapaswa kushiriki katika mafunzo ya vitendo wakiwa bado shuleni ili kuhakikisha wanakuwa na ajira mara tu wanapohitimu. Somo la ujasiriamali ni lazima lifundishwe kuanzia sekondari tena kwa vitendo. Hii itasaidia sana hata kwa wale watakaofeli kuwa na ujuzi wa kujiajiri. Mfumo wa Elimu unapaswa kuwa wa ushindani, kipaumbele kikiwa ni ubora juu ya wingi hasa katika udahili wa vyuo vikuu. Ubora utavipa vyuo vyetu hadhi kimataifa (Kwenye QS university world rankings).


Chanzo: Remix AI

Pili, serikali ya Tanzania inapaswa kutiliza mkazo uanzishwaji wa mazingira rafiki ya biashara yanayochochea ukuaji wa soko la ndani na kuvutia wawekezaji wa kigeni. Mazingira rafiki yanajumuisha urahisi wa kufanya biashara, uwepo wa umeme, upatikanaji wa mikopo, taratibu bora za biashara pamoja na kodi nafuu. Billionea Dangote alisema "Tanzania inabidi kutengeza sera nzuri Ili kuvutia wawekezaji wengi Zaidi". Pia utafiti unaonyesha kuwa makampuni makubwa kama Nike yanashindwa kuwekeza kwenye Nchi za kimaskini kama Tanzania Kwa sababu ya kodi kandamizi. Kwa kuiga mfano wa Korea Kusini, taifa ambalo linang’ara katika kuwezesha kuanzishwa kwa biashara kwa kiwango cha kimataifa, Tanzania inaweza kufaidika sana kwa kuboresha mazingira yake ya biashara ili kuvutia wawekezaji mbalimbali.


View: https://youtu.be/AAOs8EXq-qw?si=7-I-upNndk2ClNub
Tatu, ni muhimu serikali ya Tanzania kuendeleza teknolojia na kukuza ubunifu. Tanzania ina vijana wabunifu wengi Ila wameshindwa kushikwa mkono. Ubunifu na teknolojia vina jukumu muhimu katika kuinua nchi kutoka hadhi ya maendeleo duni hadi kuwa nchi iliyoendelea. Tanzania inapaswa kukumbatia mfumo thabiti wa Utafiti na Maendeleo (R&D), hasa katika teknolojia za viwanda. Ili kukuza ubunifu kwa ufanisi, ni muhimu kutambua kwamba ubunifu wenye mafanikio huimarika kupitia juhudi za pamoja kati ya vyuo vikuu, serikali na sekta binafsi. Aidha, teknolojia inajitokeza kama kipengele muhimu kitakachoweiwezesha Tanzania kupanda juu kwenye mnyororo wa thamani na kuongeza tija. Yote hayo yatawezekana kama Tanzania ikiwa na wizara maalumu ya sayansi, ubunifu na Teknolojia. Wizara hii itajikita kuwapa vipaumbele vijana wabunifu, kuongoza tafiti na kuendana na kasi ya Teknolojia ya Dunia (Robotics, Industrial 4.0 & artificial intelligence ).


View: https://youtube.com/watch?v=t3U5mcUfnso&si=I2g_OirBB7rP5UEA

View: https://youtu.be/3tJ7HLY-oe0?si=EN3wI9gky2IrpvN9
Serikali inapaswa kuunda sera ya kuhimiza viwanda vinavyolenga mauzo ya nje (export-oriented industrialization). Sera hii inatakiwa kulenga kuboresha ufanisi na ubora wa bidhaa za ndani Ili ziweze kushindana kimataifa. Kwa mkakati huu, kampuni za ndani zitabuni teknolojia mpya. Sambamba na hili, serikali inapaswa kuhakikisha kwamba kampuni zinapata ruzuku na uwekezaji ili kukuza masoko yao hasa masoko ya nje kupitia maonyesho ya biashara ya kimataifa na programu za uuzaji nje (export promotion programs).Kwa kuzingatia mauzo ya nje, kutakuwa na mtiririko wa mtaji wa kigeni, ambao utasaidia kuziba pengo la uhaba wa akiba za ndani. Kwa mfano, Korea Kusini ilikuwa kupitia sera za Seoul zilizolenga kuuza nje.


Chanzo: Remix AI
Mwisho serikali ingejitahidi sana kukuza sekta ya Sanaa hasa katika upande wa Sanaa ya kuigiza. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la umaarufu wa tamthilia za Korea Kusini nchini Tanzania. Tamthilia za ndani zimeonekana kukosa ubora hasa katika Teknolojia na maudhui huku nyingi zikiwa na hadithi za kufanana. Ili Tanzania iweze kukuza sanaa yake, inatakiwa kwanza ijikite kwenye maudhui ya kipekee na utamaduni. Mfano Korea Kusini inaingiza utamaduni wake katika tamthilia zake, jambo linalovutia watazamaji wa kimataifa. Tanzania pia ingejikita kukuza ubora wa watayarishaji wetu pamoja na Teknolojia ya uzalishaji kwa kushirikiana na Nchi zilizoendelea.

Mfano hatua aliyofanya Rais Samia kuwakutanisha watayarishaji wetu na wa Korea Kusini tarehe 01/06/2024 ni mwanzo mzuri. Ila tunatamani isiishie hapo. Tungependa kuona hapo mbeleni hata kazi za pamoja ( Korea Kusini na Tanzania) zikitoka. Pia ni kujenga miundombinu ya filamu. Mfano nchini Korea Kusini kuna maeneo maalumu (filming locations) ambayo hutumiwa na wazalishaji wa filamu za ndani na nje. Sanaa inawez pia kutumika kukuza utalii wetu. Mwisho serikali ingetengeneza mifumo mizuri kwajili ya kusambaza filamu na tamthilia na kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimataifa kama NETFLIX. Mauzo yatakayo tokana na Sanaa yanawez kuongeza pato la taifa.


View: https://youtu.be/WUIuLpqrVSo?si=2DDAwfqcipyxVobE

View: https://youtu.be/Qt8mVDwFpnQ?si=qlz_0lIqs-KJjGGy




Angalizo:

Tanzania inaweza kufikia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi kwa kujifunza kutoka kwa Korea Kusini, lakini kwa kutekeleza mikakati hiyo kwa njia inayoendana na misingi ya demokrasia na haki za binadamu na sio Njia za kibabe kama alizotumia Raisi Park Chung-hee. Pia ni muhimu kujua kuwa maendeleo yanaleta faida kubwa lakini yanakuja na changamoto mfano; madeni, uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti na uchafuzi (pollution).Hivyo basi, ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia utawala bora wakati wa hatua za maendeleo ili kupunguza hatari hizi.
Tanzania tuitakayo si Ile yenye hadhi ya Nchi duni,Bali Nchi iliyoendelea. Kwa pamoja tunaweza kufika huko💪


Tanzania Tuitakayo 2050.​
 
Upvote 336
Babu yangu aliwahi kuniambia "mazuri yetu yachukue, ila mabaya yaache hapahapa". Hii ndiyo adabu niliyokuwa nayo haswa ninapokuwa ugenini ama ninapojifunza kitu kwa mtu mwingine.
Ni sahihi kweli kujifunza mikakati yao ya kiuchumi pasi na kuiga njia hizo za kimabavu kwani ni kitu ambacho kinapingana na misingi ya kidemokrasia na haki za binadamu.

Naomba niunge mkono hoja.
 
Ahsante sana kwa kuunga mkono hoja🙏
 
Umasikini wa hii nchi asilimia 85 unasababishwa na sisi wenye watanzania na watendaji wa serikali ambao ni mazao ya jamii yetu wenye.

Tukiweza kudeal na maadili ambayo yatakuwa msingi wa watu na wanachi basi hii nchi itaoaa kwa kila kitu huko ulipotolea mfano koteee watu wao wana maadili kiwango cha sgr ndio msingi namba moja kwenye mafanikio yao makubwa kama nchi.
 
Ni kwel kabisa ulichosema 🙏
 
Bila political will ya viongozi hiI zitabaki stories tu. Baada ya miaka kumi tutaandika andiko tukajifunze BurkinaFaso. Africa shida yake kubwa ni uongozi mbaya fullstop kote huku tunazunguka tu. Leo Korea Kusini, kesho China, mara Botswana Hawa wengi walikuwa na uchumi mdogo ila Wana rise wakati sisi tuko palepale.
 
Ni kwel kabisa na ndomana mwishon navyomaliza nikasisitiza Sana kuhusu uongozi bora
 
Ni kwel kabisa
 
hili suala la lugha ni muhimu sana, watu tumesoma kiswahili miaka 7, ghafla tunakutana na lugha ya malikia, tunakwenda lakini chamoto tunakiona
 
Hakuna anaye zingatia unapoteza muda tu hapa kuandika machapisho mareefu.

Samahani lakini imenibidi niseme hivyo.
 
Kama Korea Kusini iliweza, Kwanini Sisi Tushindwe? Sisi pia tunaweza.
Wakorea kuweza haimaanishi waafrika weusi wanaweza kama wakorea.

Sisi ni watu tofauti, jamii tofauti tunatofautiana sana kuanzia kitamaduni, kiakili mpaka tunavyo yatazama baadhi ya mambo.
 
Ndani ya miaka 25 Tanzania haiwezi toka LDC to developed country.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…