Cunning
New Member
- Jun 12, 2024
- 2
- 3
Kwa miongo kadhaa tangu tumepata uhuru maendeleo ya Taifa letu yamekuwa yakitegemea ilani ya chama kinachotawa na maono ya kiongozi aliyepo madarakani. Hata hivyo muda mwingine utekelezaji wa baadhi ya miradi ulikuwa ukitegemea huruma ya viongozi waliopo madarakani, hali iliyopelekea baadhi ya mikoa na wilaya kutofautiana kwa kiasi kikubwa kimaendeleo kutokana na mfumo uliopo wa kutegemea ilani ya Chama cha siasa kitakachoshinda uchaguzi. Ukweli ni kwamba lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa chama cha siasa kilichopo madarakani kikatumia mwanya huo kujitengenezea utaratibu na kupitisha sheria za kuendelea kubaki madarakani tofauti na dhima inayotegemewa na wananchi ya kuleta maendeleo.
Kwa muktadha huo wakati umefika sasa kwa nchi yetu kuanzisha Mpango wa utekelezaji wa Taifa (MUT) ili uondoe matumizi ya ilani za vyama vya siasa katika kutekeleza shughuli za maendeleo ya taifa letu. Dira ya maendeleo 2050 lazima izingatie uanzishwaji wa chombo hiki muhimu ambacho kitaharakisha kufikia maendeleo yenye tija zaidi. Vyama vya siasa vitakuwa vinaomba ridhaa kila kipindi cha uchaguzi ili kutekeleza mpango huo wa utekelezaji wa taifa. Hivyo kila chama cha siasa kitaeleza namna kitakavyoweza kutekeleza miradi mbalimbali iliyopo kwenye Mpango wa utekelezaji wa taifa (MUT) kwa kipindi husika cha uongozi wananchi watawachagua na kuwapima kutokana na sera zao dhidi ya mipango ya taifa iliyoandaliwa itakayokuwa inatekelezwa kwa kipindi hicho. Ili tuweze kuendana na kasi ya uchumi wa dunia hatuna budi kuhakikisha tunafanya mabadiliko ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kutumia ilani ya chama cha siasa kinachoshinda uchaguzi. Kwa kipindi chote cha miaka zaidi ya sitini ya Uhuru wa taifa letu tumeshuhudia kila awamu inayoingia madarakani ikiwa na vipaumbele tofauti hivyo kukosa mwendelezo mzuri wa miradi inayoibuliwa hali inayopelekea baadhi ya miradi hiyo kushindwa kutekelezwa pindi awamu nyingine ikiingia madarakani kutokana na kutokamilika katika awamu ya uongozi uliopita.
Mataifa mengi makubwa ambayo yameendelea yanaandaa Mpango wa taifa wa utekelezaji ambayo wanasiasa na vyama vyao wanaandaa sera ambazo zinatekelezeka dhidi ya mipango ya muda mfupi, wa kati pamoja na mipango ya muda mrefu. Chama ambacho kitakuwa na sera na mipango mizuri katika kuleta maendeleo ndicho kitakachopewa nafasi ya kuiongoza nchi, hata hivyo serikali hiyo ikishindwa kutekeleza sera na kuleta maendeleo yaliyotarajiwa wananchi wanakuwa na uwanda mpana wa kuchagua viongozi wengine ambao wataonesha nia ya dhati na mwelekeo wa kuleta maendeleo.
Yafuaatayo ni baadhi ya mapungufu ambayo yamejitokeza kutokana na kuendelea kutumia ilani ya chama cha siasa kama muongozo wa kuibua na kutekeleza shughuli za maendeleo katika taifa letu.
1. Miradi mingi ambayo haikamiliki ndani ya kipindi cha utawala wa awali inatelekezwa kutokana na kukosa kipaumbele kwenye awamu mpya ya utawala hali inayopelekea upotevu wa fedha nyingi.
2. Kuna mapungufu makubwa ya uwajibikaji na uwajibishwaji kutokana na kujipangia shughuli za kutekeleza katika kipindi chote cha utawala.
3. Kuendelea kuwa na mzunguko wa umasikini kwa miaka mingi zaidi ijayo ukilinganisha na rasilimali tulizonazo kutokana na kila awamu kuwa na vipaumbele ambavyo serikali hiyo inauhakika wa kutekeleza.
4. Tishio kubwa kwa rasilimali za nchi kutokana na kujipangia namna ya kuendesha nchi na kutekeleza ahadi ambazo hazitekelezeki.
5. Serikali kushindwa kutekeleza vipaumbele vya wananchi katika kuleta maendeleo kutokana na serikali inayoingia madarakani kuwa ilishaandaa vipaumbele vyake.
Mwaka 1999, Tanzania ilizindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo ni nyenzo ya kuunganisha juhudi za Taifa katika kufikia malengo ya maendeleo yanayotarajiwa ya kijamii na kiuchumi Uzinduzi huo ulifuatiwa na hatua za maboresho mbalimbali ya kisera, kitaasisi na kimfumo katika miaka ya 2000. Maboresho haya yalikuwa muhimu kutokana na hali ya kiuchumi ambayo Tanzania ilipitia katika miaka ya 1980 na 1990. Katika kipindi hicho, nchi ilikabiliwa na kiwango kidogo cha ukuaji wa uchumi, uhaba mkubwa wa bidhaa na huduma muhimu, mfumuko mkubwa wa bei, upungufu wa mapato yatokanayo na mauzo nje, madeni makubwa na yasiyohimilika, na makusanyo madogo ya mapato ya Serikali. Katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali ilichukua hatua kadhaa za maboresho ya kiuchumi ambapo kabla ya kuzindua Dira ya Maendeeo ya Taifa. Maboresho hayo yaliungwa mkono na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kupitia Programu ya Maboresho ya Mfumo wa Uchumi (The Enhanced Structural Adjustment Facility - ESAF).
Dira mpya ya maendeleo 2050 inatakiwa kuambatana na chombo kipya kitakachotambuliwa kama Mpango wa utekelezaji wa taifa (MUT) ambacho kitaondoa matumizi ya ilani za vyama vya siasa. Mpango huu wa utekelezaji wa taifa unatakiwa kuundiwa sheria na utambuliwe na katiba ili ndio uwe muongozo wa utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo ya taifa. Vilevile mpango huu utasaidia taifa letu kwenda sawa na kasi ya maendeleo ya dunia ya sasa kutokana na kuongeza uwajibikaji. Dira mpya lazima ihakikishe inabeba dhumuni la kuwa na majumuisho ya mahitaji yote kuanzia ngazi zote na kuyapanga katika mfumo ambao utarandana nchi nzima ili kuondoa mfumo wa vyama vya siasa kuwa na mipango yao ambayo ndiyo wanayokusudia kuitekeleza pindi wanaposhinda uchaguzi. Dira hiyo mpya itakuwa ni nyenzo muhimu katika kujihakikishia maendeleo yenye tija zaidi katika nchi yetu, pia utekelezaji wa mpango huu utakuwa mwanzo mzuri wa kuheshimu matakwa ya raia na kuhakikisha kunakuwepo na matumizi mazuri ya rasilimali za nchi.
Miongoni mwa faida za Dira ya maendeleo 2050 kuzingatia matumizi ya Mpango wa utekelezaji wa taifa (MUT) ni kama ifuatavyo;
1. Mwendelezo wa utekelezaji wa miradi ambayo haikukamilika awamu iliyopita.
2. Kuongeza uwajibikaji wa serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi kutokana na hofu ya kutorudi madarakani pindi serikali hiyo iliyopo madarakani ikishindwa kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa katika Mpango wa utekelezaji wa taifa.
3. Kuharakisha maendeleo ya taifa kutokana na kuzingatia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika mpango wa taifa.
4. Itaongeza ulinzi na usalama wa rasilimali za nchi kutokana na mamlaka yote ya matumizi ya rasilimali yatarejeshwa kwa wananchi.
5. Utekelezaji wa mpango huu utakuza demokrasia zaidi pamoja na utawala bora.
6. Mpango huu utapunguza usumbufu kwa watendaji wa serikali kulazimika kutekeleza matakwa ya wanasiasa ambayo muda mwingine ni kinyume na taratibu za utumishi hivyo muda mwingi watatumia kutekeleza Mpango wa utekelezaji wa taifa.
Mwisho nashauri wananchi, asasi za kiraia, wadau wa maendeleo pamoja na serikali tuukubali uanzishwaji wa Mpango wa utekelezaji wa Taifa (MUT) kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.

Upvote
3