Mpapai na Gunzi vina uhusiano gani?

Mara nyingi gunzi kuna mvutano mkubwa sana ina maana uchawi mtupu
Ni falsafa za kishirikina
 
Hahaha hata sie kwetu tulikuwa tunafunga sana gunzi za mahindi yaani mpapai unaacha wenyewe kutoa maua na kuanza kuzaa mpapai hadi Leo sijajua why zaidi ya kupata hisia kuwa ule mbinyo unapoufunga kamba na gunzi hubadilisha kitu
kwanini gunzi la mahindi tu?jaribu kufunga mawili uone
 

Wakuu hiyo imesibitishwa kisayansi.. Ipo hivi kuna mipapai dume (male plant) hii haizai matunda, na kuna mipapai jike (female plant) na yenye jinsia zote mbili (hermaphrodite) hii ndio inayozaa matunda isipokua dume tu! Sasa kuna mimea inaweza kubadili jinsia yake (sex labile plant) moja wapo ni mipapai na inabadilika pale mazingira yatakapokua magumu kwa yenyewe kuishi sasa ili uendeleze kizazi chake ni lazima ubadilike kutoka dume kuwa jike ile uweze kuacha kizazi chake

Kufunga bunzi/gunzi ni watu wameaminishwa tu ila unaweza kufunga chochote kile ata ukipigilia misumari ilimradi mmea upate shuruba (stress) hapo mmea utahisi kuwa upo kwenye mazingira magumu na unaweza kufa muda wowote . Hapo mmea utachukua hatua ya kubadili jinsia na kuzaa matunda haraka sana kabra haujafa ili uache kizazi chake.. [emoji3][emoji3][emoji3] kama binadamu tu akinusurika na ajari utasikia sina hata mtoto.

Siku moja tu ya uumbaji ila mimea ina physiology nyingi na zakustaajabisha![emoji1544]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ignulaasm, We ndio umetoa jibu sahihi na sio mpapai tu sisi nyumbani ilikua mkitaka mti uzae mapema mfano mparachichi unachukua kipande cha nondo au msumari wa nchi 6 unagongelea pale shinani basi mapema sana utaona mparachichi unatoa mauwa na kisha matunda, hii pia kwa mwembe na jamii za miti mingi ya matunda .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha mbali kinoma! Nimefanya sana hizi mambo kwa miparachichi, michungwa n.k ilisiyozaa na inayodondosha matunda yakiwa machanga.

Kuna mlimao mmoja uliwahi kunigomea kwa kutumia msumari mara mbili; mwaka was tatu nikagonga msumari mkuukuu hivi nikaung'oa; kisha nikaupaka msumari mavi meusi ya kuku (yale yanayonuka), na kuugongea tena. Tulikula malizao mpaka ukajizeekea zake.
 
Nafikiri ndio ulikua umefikia mwaka wake wa kuzaa, hata kama usingeyafanya hayo.

Mfano, unaumwa unatumia dawa za kila aina, huponi, mara unapewa dawa za miti shamba unakunywa, afu unadhani ndio zimekuponya pekee, kumbe huenda hizo dawa na zile zilizokua zimesalia mwilini zimetengeneza combination ya matibabu ndo ukapona, au zile dawa za awali ndio zimefikia muda wake wa kukuponya.
 
Nimewahi kuona minazi ikigongelewa vipande vikubwa vya nondo....sikuwahi kuelewa sababu....

Leo ndiyo nimejua...thanks to JF, kisima cha maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mani.na walah. Haahaha
 
Nikiwa shule ya msingi nilipanda mpapai nyumbani, likawa dume wakati nasikitika mama akaniambia libebeshe gunzi, nikafanya hivyo baada yamiezi mitatu nikaona linaanza kuweka maua na kisha likazaa mapapai swaafi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…