Mpapai na Gunzi vina uhusiano gani?

Aisee nimepata maarifa ya kuustress mmea dume, safi sanaa, sisi tushawahi kuwa na mpapai dume na hakuna aliyekua anajua kuhusu kubebesha gunzi ama misumari ,tukaamua kuukata tu utoke. Sahivi ni mwendo wa magunzi tu mpaka kieleweke.

Ila vipi ikitokea labda mmea jike wenye matunda ukachomwa misumari ama gunzi pia utabadilika na kuwa dume?, au hii inaapply kwa mimea dume pekee?

Jf ni kisima cha maarifa.😍
 
Hapa ndio ile and vice versa is true inakua applied....binadamu akiwa na stress ni mzgo ila kwa mmea ndio mpango mzima
 
Tafiti zinaonesha mipapai ina jinsia zaidi ya mbili.
1.jike(female)
2.dume(male)
3.jikedume( haemoprodite).
 
Hii ni kweli, hata mimi nilijaribu mpapai dume ukaanza kutoa mapapi hadi nakula!

Sijui kuna sababu gani kisayansi! Inashangaza kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Vitu ni vya kienyeji, ila vinafanya kazi vizuri kuliko vya kisayansi.

Kule Mtwara, Newala kuna watu wanajua dawa ya mbuzi kuzaa mapacha, na mbuzi wengine huzaa mpaka mapacha wa tatu.
Kwa mbuzi akisha anza kuzaa mapacha, kama ni watatu, ama wawili huzaa hivyo mpaka ukomo wake wa kuzaa.
 
Ipo ivi mimea kama mpapai inatabia ya kubadilisha jinsia yake yani kutoka ya kiume na kuwa ya kike endapo itakuwa under stress yan ikifungwa kamba au ikitobolewa na kitu chenye ncha kali kama vile msumali nia ya kufanya ivyo ni kuacha kizazi chake kabla ujafa sio.
NB sio lazima kamba ifungwe na kibunzi ata jiwe linaweza kuleta mabadiliko kwasababu ukifunga na kamba unazuia chakula na maji yasiende bahazi ya sehemu ya mmea kwaiyo mmea unakuwa under stress kwaiyo inapelekea mmea kubadili jinsia maana unaofia kufa kabla ujaacha kizazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…