Tetesi: Mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Kwa namna huyu "Jasusi mbobezi" Bernard Kamilius Membe, anavyoendelea kushika "chart" humu kwenye mitandao ya kijamii, ni dhahiri kuwa huko kwenye hicho chama, wanachodai wenyewe kuwa ni chama kikubwa, hivi sasa kunatokota na sisi wananchi tusubiri, kwa kuwa yajayo yanafurahisha au kukarahaisha...

Membe ametoa madai mazito sana kuwa Katiba ya CCM haikufuatwa katika kufukuzwa kwake ndani ya Chama

Kwani amedai kuwa ni takwa la kikatiba, anapofukuzwa kiongozi yeyote wa ngazi za juu katika chama hicho ni LAZIMA jambo lake lingejadiliwa ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, ndipo uamuzi ufikiwe.

Jambo ambalo halikufanyika katika kufikia uamuzi wa kufukuzwa kwake. Kwani mwenyewe anadai kuwa "process" ilikuwa haijakamilika, kwa kuwa kikao kilichomjadili kilikuwa ni kikao cha Kamati Kuu pekee, wakati mchakato ulikuwa haujakamilika, kwa kuwa kikao chenye uamuzi wa mwisho, ambacho ni kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilikuwa hakijakaa.

Jambo linaloshangaza ni kuwa tokea madai hayo yatolewe na Membe, hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa CCM, aliyejitokeza kujibu tuhuma hizo

Kwa madai mazito kama hayo, ni kwanini hadi sasa chama cha CCM, kimeamua kukaa kimya, kisitoe majibu yoyote, kwa madai hayo ya Membe?

Inaelekea kuna mfukuto mkubwa sana huko kwa majirani zetu wa CCM

Ni dhahiri sasa kama alichoongea mwenyewe Membe, kuwa tufanye subira kati ya mwezi huu wa June hadi October ya mwaka huu, lolote lisilotegemewa na wananchi wengi litatokea katika nchi hii na litaleta kishindo kikubwa sana!

Subira yavuta kheri, ngoja tusubiri ili tuyashuhudie yatakayojiri
 
Ulikuwa unaota mpasuko wa sketi au underskate a.k.a shumizi.

Yaani membe ndio wa kuleta mpasuko CCM? Mtu pekee alijipanga na kusumbua CCM ni LOWASSA huyu hata mtikisiko hawezi sababisha. Huo ubobezi wa ukachero alikuwa nao akiwa kwenye system. Sasa hivi ni sawa na samaki nje ya maji anatapata tu hana lolote.
 
Jibu hoja ya utaratibu ndani ya CCM.
 
Fomu tuli print moja tu... [emoji3][emoji3][emoji3]
Na ile Jumatatu aliyoisema Membe, kuwa atatinga Dodoma, kwenda chukua fomu yake ya Urais ndiyo ishafika...........

Ngoja tusubiri tuone kama Dkt Bashiru, kama tulivyowazoea mbinu zao, watatia komeo geti kuu la kuingilia, tena ndani ya ulinzi mkali!
 

Mbobezi hakuweza kuzuia katiba kuvunjwa????

Wasipomjibu utawafanya nini??

Jenga kwako

Nguvu ya JPM haina mpinzani ndani au nje

Sio vizuri kukosa upinzani ndani au nje, ila hawapo

Mwenzio anakanusha maneno yake umebaki gizani
 
Ni kwanini swala la Membe halikufika katika kikao cha Halmashauri kuu ya chama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…