Tetesi: Mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM

Tetesi: Mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM

Nakumbuka alisema niguse nikinukishe

Badala ya kuguswa akapapaswa mpaka munyeo akawa kimya mpaka leo.

Alishasema USIMCHEZEE SIMBA ALIYELALA

JPM msikieni tu.
 
Kwa namna huyu "Jasusi mbobezi" Bernard Kamilius Membe, anavyoendelea kushika "chart" humu kwenye mitandao ya kijamii, ni dhahiri kuwa huko kwenye hicho chama, wanachodai wenyewe kuwa ni chama kikubwa, hivi sasa kunatokota na sisi wananchi tusubiri, kwa kuwa yajayo yanafurahisha au kukarahaisha...

Membe ametoa madai mazito sana kuwa Katiba ya CCM haikufuatwa katika kufukuzwa kwake ndani ya Chama

Kwani amedai kuwa ni takwa la kikatiba, anapofukuzwa kiongozi yeyote wa ngazi za juu katika chama hicho ni LAZIMA jambo lake lingejadiliwa ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, ndipo uamuzi ufikiwe.

Jambo ambalo halikufanyika katika kufikia uamuzi wa kufukuzwa kwake. Kwani mwenyewe anadai kuwa "process" ilikuwa haijakamilika, kwa kuwa kikao kilichomjadili kilikuwa ni kikao cha Kamati Kuu pekee, wakati mchakato ulikuwa haujakamilika, kwa kuwa kikao chenye uamuzi wa mwisho, ambacho ni kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilikuwa hakijakaa.

Jambo linaloshangaza ni kuwa tokea madai hayo yatolewe na Membe, hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa CCM, aliyejitokeza kujibu tuhuma hizo

Kwa madai mazito kama hayo, ni kwanini hadi sasa chama cha CCM, kimeamua kukaa kimya, kisitoe majibu yoyote, kwa madai hayo ya Membe?

Inaelekea kuna mfukuto mkubwa sana huko kwa majirani zetu wa CCM

Ni dhahiri sasa kama alichoongea mwenyewe Membe, kuwa tufanye subira kati ya mwezi huu wa June hadi October ya mwaka huu, lolote lisilotegemewa na wananchi wengi litatokea katika nchi hii na litaleta kishindo kikubwa sana!

Subira yavuta kheri, ngoja tusubiri ili tuyashuhudie yatakayojiri
Apumzike tu kwani yaonyesha hawamtaki hugo. Akajiunge na Chauma
 
Hapiti hata asimame na Kingwendu
Panapokuwa na Free & Fair election, ni kweli kabisa huyo Jiwe wao hata asimamishwe kwa kupitia matangazo yote ya vyombo vya habari halafu awe VS Kivuli, basi wananchi wataona bora wapigie kivuli hiko kuliko kumpigia huyo Jiwe wenu!
 
Kwa kujifariji hamjambo
 
Magu tatizo sio kwa watanzania hata mimi nampa kura ya Urais ila shida ipo ndani ya CCM...!! Huo ndio ukwelii...
 
Hakuna mpasuko sema Membe Anakomaaa tu ila hata yeye anajua yuko alone ananohesha mziki tu
 
Ulikuwa unaota mpasuko wa sketi au underskate a.k.a shumizi.

Yaani membe ndio wa kuleta mpasuko CCM? Mtu pekee alijipanga na kusumbua CCM ni LOWASSA huyu hata mtikisiko hawezi sababisha. Huo ubobezi wa ukachero alikuwa nao akiwa kwenye system. Sasa hivi ni sawa na samaki nje ya maji anatapata tu hana lolote.
Angekuwa hana lolote msimngemletea Zengwe kwenye kuchukua form......MTU FURANI kasoma mchezo kaona bora ampige chini KIBABE bila kufuata taratibu ila kati ya june - October Lolote litatokea JASUSI MBOBEZI KASEMA.
 
Litokee sasa kwanini asubiri October.

Farijianeni kwa ndoto za mchana za Membe.

Aminini katika yeye awatiaye ujinga kuamini alifanyiwa zengwe kwani zengwe ndio umebaki mtaji pekee kuwa kwenye siasa za mitandaoni.

Kesheni mkisubiri kati ya october lolote litokee kwa kachero wenu mbobezi wa kwenye ndoto.
 
Savimbi Jr
Eti kweli mtu ambaye siyo tishio kivile, iweje CCM yote imuogope utadhani ugonjwa wa ukoma?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Acha tu mkee ndo yale ya Nkurunzizaa anaongeza miaka ya urais lafu anakufaa...!! Uafrika ni laana yani mtu anafanya mambo as if ataishi milelee...
Waafrika hawawezi kujiongoza
 
Litokee sasa kwanini asubiri October.

Farijianeni kwa ndoto za mchana za Membe.

Aminini katika yeye awatiaye ujinga kuamini alifanyiwa zengwe kwani zengwe ndio umebaki mtaji pekee kuwa kwenye siasa za mitandaoni.

Kesheni mkisubiri kati ya october lolote litokee kwa kachero wenu mbobezi wa kwenye ndoto.
Kwanini mmemfukuza kama sio threat? Ruhusuni watu wachukue form!!
 
Back
Top Bottom